Rais Magufuli ataka TAKUKURU ifumuliwe. TAKUKURU ifumuliwe au sheria ifumuliwe kuipa nguvu TAKUKURU?

Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
386
517

rais_magufuli_ataka_takukuru_ifumuliwe_h22657_1a62b.jpg


18 hours ago

RAIS Dk. John Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna wa Polisi (CP) Diwani Athumani, kufumua muundo wa taasisi hiyo ili watendaji wanaojihusisha na rushwa wachukuliwe hatua.
Alitoa kauli hiyo jijini hapa jana baada ya kumwapisha CP Athumani kuwa mkurugenzi mpya wa Takukuru ikiwa ni siku chache tangu atengue uteuzi wa Valentino Mlowola aliyekuwa bosi wa taasisi hiyo.
Wiki iliyopita, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Mlowola huku akieleza sababu ya uamuzi wake huo kuwa ni pamoja na taasisi hiyo kutoshughulikia vitendo vya rushwa mkoani Mara.
“Nimekwenda pale Musoma mtu amenunua Musoma Hotel kwa miaka kumi hashughuliki, anapewa kazi za kandarasi hamalizi. Waziri Mkuu alipita hapa Mara akatoa maagizo kwa Takukuru kwamba washughulikie.
“Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara alilishughulikia na akamaliza tangu mwezi wa nne na akapeleka faili makao makuu, lakini hadi leo mwezi wa tisa makao makuu bado hawajalishughulikia,” alisema.
Alisema makao makuu kulikalia faili hilo ndiyo sababu iliyomfanya aone kuwa Mlowola lazima akae pembeni akafanye kazi nyingine.

HOJA: TAKUKURU ifumuliwe au sheria ifumuliwe?
Utangulizi:
TAKUKURU ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, yaani tuseme kwamba maswala yote ya kesi zinazohusu kupokea na kutoa rushwa yaliundiwa Taasisi pekee, maana yake ni kwamba mamlaka pekee inayochunguza kesi za rushwa na kuipeleka mahakamani maswala ya rushwa, kutoa elimu dhidi ya athari za Rushwa, kuzuia Rushwa isitokee pale wanapopata taarifa za kuwepo mianya za Rushwa.

Kwanini TAKUKURU iliundwa?
Iliundwa ili kupunguzia polisi mzigo wakuchunguza kesi ya Rushwa, kutokana na kwamba rushwa ilihitaji nguvu ya pekee kutokana na athari zake, hivyo basi mamlaka yakiuchunguzi yalitolewa Polisi nakupewa TAKUKURU.

TAKUKURU inafanyaje kazi zake?
OFISI:
Takukuru ina ofisi zake wilaya zote za Tanzania, ofisi za kisasa. Ofisi zote zimeunganishwa na network mmoja, kesi zote zinazosajiliwa takukuru mahala popote makao makuu haziona siku hiyo hiyo.

Upelelezi wa kesi na uwasilishaji wa kesi mahakamani:
Upelelezi wa kesi

Upelelezi wa kesi za rushwa baada ya kesi kusajiliwa, unafanywa na maafisa upelelezi(Investigators). Wapelelezi wote wa TAKUKURU wana elimu yakuanzia Bachelor, Masters na wangine wana Phd, hii ndiyo sifa ya kwanza ya wapelelezi wa PCCB lazima uanzia na Degree.
Jalada za Upelelezi: baada ya kesi kusajiliwa TAKUKURU jalada ya upelelezi hukabidhiwa kwa Mpelelezi, kwa kuwa TAKUKURU imeundwa kitaalam zaidi mwenendo wote wa uchunguzi wa kesi hatua kwa hatua huingizwa kwenye mfumo wa upelelezi(Investigation system ) hivyo basi kuirahisishia makao makuu kufahamu mwenendo wa upelelezi wa kesi zote za Rushwa. Kwa mfumo huu wa uchunguzi (investigation software) za TAKUKURU jalada la upelelezi huhamishwa kutoka kwa mpelelezi mmoja kwenda kwa mwingine bila kuathiri mwenendo wa uchunguzi, hii husaidia kupunguza mianya ya rushwa kutokana ukweli kwamba kesi mmoja inaweza kuchunguzwa na investigators tofauti kulingana na kusuasua kwa mwenendo wa uchunguzi:

Uwasilishaji wa kesi Mahakamani
Baada ya uchunguzi kukamilika TAKUKURU hupeleka kesi mahakani kwa kibali cha DCI.

Hapa ndipo panapohitaji kufumuliwa:
Hapa ndipo tunaposema TAKUKURU ilinyiwa meno makusudi na viongozi wa serikali kupitia sheria, wana JF embu fikiria kesi ichunguzwe na TAKUKURU ushahidi wote ukusanywe alafu DCI aseme hii iende na hii isiende, hapa ndipo palipo na TATIZO yaani SHERIA. kama kweli Rais anadhamira afumue hapa. Sheria isiseme mmoja kwa mmoja kuwa TAKUKURU inaweza kuchunguza maswala yote ya rushwa bila kuhitaji kibali cha mtu yoyote, kwa wasiofahamu kwa wateule wote wa Rais hauwezi kumchunguza bila kibali cha Rais, sheria ndiyo inataka hivyo.

Hitimisho:
PCCB ni kati ya taasisi bora ya kiuchunguzi katika Africa ilijengwa vyema. Sioni kwa jinsi gani TAKUKURU inaweza kuwa na nguvu nje na sheria.
 
Back
Top Bottom