MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Tukio hili limetokea wakati Rais Magufuli akielekea Ikulu baada ya kuhudhuria Ibada katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililoko Oysterbay jijini Dar es salaam.
Rais Magufuli alisimamisha msafara wake na kushuka kuwafuata walemavu ambao walikuwa wamekusanyika lakini haikufahamika sababu iliyowafanya kukusanyika.
Ingawa mazungumzo ya Rais na walemavu hayakuweza kunaswa na shuhuda wa tukio, kitendo cha kushuka na kuzungumza na walemavu hao kiliwafanya watu waliokuwapo jirani na eneo hilo kushangaa na alipomaliza kuongea nao alipanda tena katika gari yake na msafara huo kuondoka kuelekea Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akisalimiana na kuongea na watu wenye ulemavu.