Rais Magufuli ashiriki kuaga Mwili wa Marehemu Christina Lissu katika ukumbi wa Karimjee

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Marehemu Christina Lissu anaaagwa leo katika ukumbi wa Karimjee. Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum toka Singida, Christina Mughwai Lissu(CHADEMA) limefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa. Alifia Hospitali ya Aghakhan Dar. Alifariki Alhamis iloisha.
13015159_461351760724094_5160598043623060475_n.jpg
13000145_461351707390766_165063810508359866_n (1).jpg
12974301_461351637390773_8322007641741121629_n.jpg

12936613_772098009592995_798120804966882464_n.jpg

Wabunge wakisaini kitabu cha maombolezo ya marehemu Christina Lissu anayeagwa leo katika ukumbi wa Karimjee

======================

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA VITI MAALUUM WA CHADEMA JIJINI DAR LEO
IMGL0173.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
IMGL0034.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
IMGL0124.jpg

IMGL0127.jpg

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
IMGL0133.jpg

Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
IMGL0141.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.
 
Back
Top Bottom