Rais Magufuli, ashauriwe aache kuchomeka chomeka maneno ya kizungu katika hotuba

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,323
29,584
Habari!

Hii haionyeshi hali nzuri, Rais wa nchi ambaye huwa anajinadi kukipigia debe kiswahili katika anga za kimataifa, yeye ndio yuko mstari wa mbele kutokukitumia kwa ufasaha.

Rejea hotuba yake Uganda hapo jana, kwa kweli mie ananikinaisha sana anavyotumbukiza tumbukiza maneno ya kizungu wakati kaamua kuongea kiswahili, kama vipi, apige tu kizungu mwanzo mwisho.

Kama ni kiswahili basi asichanganye.
 
Habari!
Hii inatia kinyaa, rais wa nchi ambaye huwa anajinadi kukipigia debe kiswahili ktk anga za kimataifa, yeye ndio yuko mstari wa mbele kutokukitumia kwa ufasaha.
Rejea hotuba yake Uganda hapo jana, kwa kweli mie ananikinaisha sana anavyotumbukiza tumbukiza maneno ya kizungu wakati kaamua kuongea kiswahili, kama vipi, apige tu kizungu mwanzo mwisho. Kama ni kiswahili basi asichanganye.
 
Wakuu.
Raisi wetu mpendwa kiingereza ni tabu kidogo lakini kutokujua kiingereza haina shida kwani tuna utajiri wa lugha, adhimu ya kiswahili hivyo isichukuliwe kua watanzania wote hawajui kiingereza.
Waganda mtuheshimu sana kwenye hilo.
 
Kwani Waganda wamesemaje!?

Alafu ili kudhibitisha hili ungeandika kizungu..
 
Ndio ushamba unaoongelewa huo.... alafu anakipenda kitu ila chenyewe hakimpendi.. hivi sio kuna yule mtoto wake juz matokeo yake ya std 7 yaliwekwa humu kamaliza Feza? Sasa kwanini mshua asimgande huyo dogo angalau abrush ngeli kimtindo?

Maana wanasema practice makes perfect
 
Back
Top Bottom