Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,386
Jamani kwa maoni yangu tuna Rais anayeonekana anaishi kwa hofu akiwa haamini mtu yeyote, siyo watu wa chama chake, siyo viongozi wa upinzani, siyo bunge, siyo mahakama na sasa hali inavyoonekana haamini hata baraza lake la mawaziri na tukikaribia mwaka 2020 atakuwa haamini hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kama alivyo Trump...kwa maoni yangu tukifika hatua hiyo ni hatari sana kwa Taifa;
Nashauri basi asaidiwe kujiamini kuwa watu katika jamii kutofautiana mawazo na misimamo ni jambo la kawaida hasa katika masuala ya uongozi wa nchi...mimi naamini kiongozi smart angejielekeza zaidi katika kujenga umoja na stability ya taasisi kuliko kukimbilia kufukuza wanachama maarufu ambao wamekitumikia chama cha mapinduzi kwa muda miaka mingi, hawa wanaofukuzwa walikuwa na haki ya kumwunga mkono Lowassa kuwania Urais kama wengine walivyokuwa na haki ya kumwunga yeye mkono.
Nawasilisha!