Rais Magufuli apunguze kuonekana Hadharani, kupenda Kuongea yale yale kwani yanamshushia mno Hadhi yake

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kama kuna ambao nitawakwaza katika hili nawaombeni Radhi ila nikiwa kama Mzalendo na Mtanzania wa kweli nadhani nami pia nina Wajibu katika Kuwasilisha yale ambayo kiukweli nakumbana nayo 24/7 humu Mitaani ( Changanyikeni ) ambako ndiko maisha yetu yalipo.

Kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Rais JPM kwa Juhudi zake za kuiletea Tanzania Maendeleo na nimtie tu Moyo kuwa aendelee hivyo hivyo kwani kidogo kuna Mabadiliko ya Kimsingi ambayo tumeshaanza Kuyaona na tuna Imani kuwa kwa Mipango yake atatufikisha mbali Kimaendeleo.

Hata hivyo baada ya Kuyasema haya naomba nami leo niseme machache juu ya mienendo ya Mheshimiwa Rais JPM ili kama kuna uwezekano basi Wasaidizi wake wamsaidie kwani Mrejesho tunaoupata na tunaouona huku Mitaani Kwetu haina Taswira nzuri Kwake kama Rais sana sana tunaona tu Watu wengi sasa wakianza Kumpuuza, kuonekana anawaboa huku wengine nao wakimdhihaki kwa maneno ya Kejeli ya hapa na pale.

Wasaidizi wa Rais hebu fanyeni kila muwezalo mpunguze Ratiba za Rais ambazo zinamfanya kila mara au kila Siku awe tu anaonekana Yeye tu na si Wasaidizi wake ama Makamu au Waziri Mkuu kwani nisiwaficheni kwa hali iliyofikia sasa Mheshimiwa ameanza Kuwaboa Watu kwa kila wakati akiwa anasikika Yeye tu.

Basi bora hata akiwa anaonekana mara kwa mara awe anakuja na Kauli mpya na zenye Mantiki na Kueleweka lakini bahati mbaya mno kila akiwa anaonekana tu Kauli zake ni zile zile ambazo zinajulikana na pengine hata zimeshaanza Kuzoeleka na Watanzania wengi hivyo zinamfanya awe anawaboa wengi japo wanaweza wakawa hawamwambii ila Kimoyomoyo Wanamsanifu.

Hoja yangu ya Msingi hapa ni kwamba sikatai wala sipingi Mheshimiwa Rais kufanya Ziara zake au Kuzungumza ila naomba kama inawezekana basi awe anapangiwa tu Ziara za mambo Muhimu, Makubwa na Mazito ambayo hata kila Mtanzania akisikia yupo anaweza kuweka attention Kubwa Kwake na pia awe anachagua maneno yenye Tija na Mantiki ya Kuyaongea mbele ya Hadhira ambayo yatazidi Kumjengea Heshima.

Ni Rais mzuri sana na ana Mipango mikubwa na mizuri kwa Tanzania yetu hii na Sisi Watanzania kwa ujumla ( kwani Kiasili ni Mpambanaji mzuri na Mtu wa Matokeo mema ya Kiufanisi ) ila nadhani ama hapati Ushirikiano wa Kutosha kutoka kwa Wasaidizi wake au Wasaidizi wake wanamuyumbisha Makusudi ili akosee na azidi Kudharauliwa au Kupuuzwa au Kuchokwa na Watanzania au labda anahitaji sana Mafunzo ya Kiitifaki ( Protocol ) ili auvae Urais Kiuhalisia wake.

Nakumbuka ni jana tu nilipanga Usafiri wa DalaDala na lilikuwa limejaa kweli kweli ambapo kuna muda Dereva sikujua ama yalikuwa ni matakwa yake tu Binafsi au alikuwa nae anataka Kupima Upepo kwa Abiria kwa Mheshimiwa Rais ambapo kwa Mshangao mkubwa kabisa kuna muda Dereva aliweka Idhaa ambayo Rais alikuwa akiongea ambapo nakumbuka alipoweka tu Abiria wengi wakajawa na Hasira na Kumuamuru aondoe hiyo Idhaa na Dereva akafanya hivyo upesi. Na matukio kama haya nimeshakumbana nayo mara kadhaa tu hali ambayo imekuwa ikinishtua sana.

Namalizia tena kwa Kuomba Rais apunguze sana Kuonekakana onekana Hadharani ( bali awe anaonekana tu kwa mambo ya Msingi, Muhimu na Nyeti kwa nchi ) na Kuzungumza yale yale tu ( ambayo yanaboa sana ) kila akipata Fursa ya Kuzungumza na Watanzania kwani yanampunguzia sana Hadhi yake kama Mtu wa Juu na mwenye Mamlaka ya mwisho Kimaamuzi katika nchi hii kwa mujibu wa Katiba yetu.

Yangu ni hayo tu na namtakia Utendaji mwema wa Majukumu yake. Watanzania ( wakiongozwa na Mimi ) tunampenda na tunamkubali.
 
Wasaidizi wa Rais hebu fanyeni kila muwezalo mpunguze Ratiba za Rais ambazo zinamfanya kila mara au kila Siku awe tu anaonekana Yeye tu na si Wasaidizi wake ama Makamu au Waziri Mkuu kwani nisiwaficheni kwa hali iliyofikia sasa Mheshimiwa ameanza Kuwaboa Watu kwa kila wakati akiwa anasikika Yeye tu.

Watu gani hao wanaoboreka kisa mheshimiwa kuonekana mara kwa mara kuwasikiliza wananchi?

Binadamu huwa hatuna jema na tunakasumba ya kuwaza mabaya kuliko mazuri. Kuonekana katika jamii ni kitendo cha kishujaa kwani Mh. Rais ni mtu wa watu na mwenye upendo kwa watu wake.
 
Hii aliambiwa na Mzee Mangula pale kwenye corridor za ikulu akatahamaki, sana,
Mpaka sasa yeye na Mangula hawashauriani tena, aisee tulobahatika tunaona mengi

Kuna shida Wasaidizi wake tunaomba wamsaidie katika hili tafadhali. Hata kama akiwa haonekani sana Hadharani ila tunaojua Utendaji wake mzuri tunajua anaiongoza nchi vyema kabisa kuliko akiwa anaendelea Kuonekana mara kwa mara kiasi cha hadi Watu wengine wanamzoea na kuchoka pia Kumuangalia na kibaya zaidi hata akiwa anazungumza ( anahutubia ) huwa anapenda tu kurudia rudia maneno yale yale na hata akisema abadilke basi maneno yanayomtoka pia huwa siyo ya Kistaha na hayana Hadhi ya Rais kuyatoa.

Tunampenda na ndiyo maana tunamrekebisha hivi ili abadilike na azidi kuwa Rais / Kiongozi wetu bora, makini na mchapakazi.
 
Watu gani hao wanaoboreka kisa mheshimiwa kuonekana mara kwa mara kuwasikiliza wananchi?

Binadamu huwa hatuna jema na tunakasumba ya kuwaza mabaya kuliko mazuri. Kuonekana katika jamii ni kitendo cha kishujaa kwani Mh. Rais ni mtu wa watu na mwenye upendo kwa watu wake.

Heshimu Ushauri wangu kama ambavyo na Mimi pia nauheshimu huu wako sasa. Halafu tambua ya kwamba si kila anayemshauri au kumkosoa Rais basi ama ni Mpinzani au Hampendi au ana Chuki nae Binafsi. Na kwa Kukusaidia tu ni kwamba hakuna Rais ambaye Mimi ( Mleta Uzi ) huu namkubali na nina matumaini nae makubwa ya Kuifikisha Tanzania yetu hii katika Kilele cha Mafanikio kama Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Joseph Magufuli. Tunamkosoa kwa Kumjenga zaidi na siyo Kumbomoa Kisiasa kama nyie Wanafiki wengi mnavyodhani.
 
Kelele zimezidi kuhusu Chato City sasa anatafuta kuifunika funika. Lakini it's too late, anajaribu kupima upepo lakini duu...
Ndo maana hakuna mvuto...

Na siyo Siri amepoteza Mvuto wa Kijamii kwa sasa pengine hata kuliko Yeye anavyojua au Watu wake wa karibu wanavyomdanganya. Ajirekebishe katika hili tafadhali.
 
Heshimu Ushauri wangu kama ambavyo na Mimi pia nauheshimu huu wako sasa. Halafu tambua ya kwamba si kila anayemshauri au kumkosoa Rais basi ama ni Mpinzani au Hampendi au ana Chuki nae Binafsi. Na kwa Kukusaidia tu ni kwamba hakuna Rais ambaye Mimi ( Mleta Uzi ) huu namkubali na nina matumaini nae makubwa ya Kuifikisha Tanzania yetu hii katika Kilele cha Mafanikio kama Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Joseph Magufuli. Tunamkosoa kwa Kumjenga zaidi na siyo Kumbomoa Kisiasa kama nyie Wanafiki wengi mnavyodhani.

Mkuu mbona sijakutukana ndugu yangu.

Nimehoji tu maana napenda sana kuhoji kuliko kukubaliana na ushauri wa mtu bila kuhoji
.
 
Nilijua ni Mimi peke yangu kumbe anatuboa wengi da! Yaani jamaa kila akisimama tunajenga reli esijiara, stiegler, tumenunua ndege
 
Back
Top Bottom