johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,599
- 141,416
Rais Magufuli amewataka wananchi wafanye kazi na kwamba uzazi wa mpango ni swala linalotafskarisha.
Amesema baadhi ya nchi huko ulaya zinaujutia mpango huo kwani umezikosesha nguvu kazi.
Rais amesema ameishi Uingereza Kwa mwaka mmoja pia amekaa Ujetumani, Canada, Norway nk hivyo anaelewa vizuri Athari za mpango huo.
Source: TBC
======
Rais Magufuli amepingana na sera ya Serikali yake ya uzazi wa mpango akidai kuwa sera hiyo inapunguza nguvu kazi kwa Taifa
Ameyasema hayo leo Septemba 9, 2018 akiwa mjini Meatu katika mkoa wa Simiyu huku akiongeza kuwa Watanzania waendelee kuzaa lakini wachape kazi ili kukidhi mahitaji ya watoto wao
Amesema ”Najua Waziri wa Afya Ummy Mwalimu hapa angependa kuongelea mambo ya uzazi wa mpango lakini mimi mengine huwa sikubaliani nayo sana, utapangiwaje kuzaa?"
Rais aliendelea kwa kusisitiza kuwa ''Najua kesho watapinga sana lakini ukweli ndio huo watu wamejazwa mawazo ya ajabu, huwezi kuwa Mwanaume kisha ukubali kufungiwa kizazi! Yaani ng'ombe wako umtoe kizazi na wewe tena ukatolewe kizazi? Mimi sikubali''
Aidha, alitolea mfano katika nchi mbalimbali alizowahi kuzitembela akisema “Mimi Ulaya nimekaa, nafahamu madhara ya kutokuzaa, nchi gani sijaenda, Japan nimekaa, Uingereza nimekaa mwaka mzima, Ujerumani nimekaa, Canada nimekaa na nikachaguliwa kuwa 'co-chair' wa mawaziri ardhi duniani, Denmark, Norway, utanidanganya wapi, China nimefika."