KadamaKadama
Member
- Oct 9, 2013
- 86
- 65
Dakt.Magufuli akihudhuria Mkutano wa 28 wa Nchi za Africa huko Addis -Ababa, Ethiopia, ameujulisha Mkutano kuwa haungi mkono taarifa ya kuongeza mapato kugharimia shughuli za Umoja wa Afrika/AU iliyowasilishwa na Rais Kagame, badala yake amesema ni vyema Sekretariati ya AU ikawa na Ufanisi zaidi kwa kujibana na kushauri kiasi cha fedha kielekezwe hasa katika shughuli za Ulinzi zinazotekelezwa na umoja huo.
Mapendelekezo yalikuwa bidhaa zinazoingia katika Nchi za Afrika zitozwe asilimia 0.2 na fedha hizo zichukuliwe kwa shughuli za kiutawala na mambo mengine ya Umoja wa Afrika. Ukipiga hesabu kama nchi zote zitachangia utakuta inakuwa mara tatu ya fedha ambazo umoja unahitaji.
Na rais kapendekeza hili swala liangaliwe Vizuri. Na kwa Tanzania pekee ambayo inatakiwa ichangie Dola Mil 2.8 inakwenda kuchangia dola zaidi ya Mil 17 ambazo ni pesa nyingi ambazo kwa tanzania zingefanya kazi kubwa
Taarifa zaidi zaja.....