Rais Magufuli aongoza wananchi wa Dar kuaga mwili wa Dk. Didas Massaburi, atoa neno

kilaza mjanja

JF-Expert Member
Jun 2, 2016
654
1,143

Katika hali ya kushangaza na kutia shaka ni pale msemaji wa familia ya marehemu alipo kuwa akisoma historia ya familia na kusema kuwa marehemu ameacha mke mmoja na wajane wawili ambapo kauli hiyo imeleta utata na kuleta miguno kwenye msiba huo.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza rais magufuli alikuja na kukanusha na kusema kuwa masaburi alikuwa na wake 4 ama 5 na alikuwa na watoto zaidi ya 20 hivi.

je hii inamaana gani kwa jamii?

==========



RAIS John Magufuli akiwa miongoni mwa watu walioshiriki kuuaga mwili wa Dk. Didas Masaburi, aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam (2010-2015), amezua jambo.

Akishiriki kuaga mwili huo leo asubuhi katika Viwanja vya Karimjee, Rais Magufuli amesema ingawa wasifu wa marehemu umemtaja Janeth Masaburi pekee kama mke lakini yeye anawafahamu wake wengi wa marehemu.

“Katika wasifiu ametajwa mke wa marehemu mmoja lakini mimi nawafahamu wake wa marehemu wengi sana. Na katika tabia zetu za kiafrika hilo suala la wake wengi ni kawaida tu. Hata vitabu vitakatifu vinasema Mtume Suleiman alikuwa na wake zaidi ya elfu moja.

“Nilikuwa naongea pale na Mheshimiwa Kikwete nikasema na sisi tungefurahi sana kama tungekuwa na wake wengi kama hawa,” amesema na kusababisha vicheko na miguno kutoka kwa waombolezaji.
Rais Magufuli ameeleza kuwa, historia ya Masaburi haiwezi kufutika katika Jiji la Dar es Salaam ushahidi wa hili ni watu wengi waliojitokeza katika msiba wake.

“Tunazungumza hapa kuwa watoto wa marehemu ni 20 lakini wanaweza kuwa hata zaidi ya 20.
“Niwaombe sana nyie watoto msifarakane, mshikamane na mtoto wa kwanza akawe kiongozi wa familia, palipo na umoja Mungu atawatangulia, sisi sote tu njia moja na kila mmoja ataionja mauti na si mimi, Kikwete wala Lowassa atakeyekwepa mauti,” amesisitiza.

Baada ya mwili huo kuagwa Karimjee, msafara wa waombolezaji umeelekea eneo la Chanika kwa ajili ya mazishi.

Viongozi mbalimbali walijitokeza kuuaga mwili huo pamoja na wananchi mbali na Rais Magufuli ni Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu; Rais Mstaafu Kikwete; Spika Mstaafu, Anne Makinda na Gharib Bilal, Makamu Mstaafu wa rais.

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam; Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam; Charles Kuyeko, Meya wa Manispaa ya Ilala; Abdallah Bulembo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM; mawaziri, wabunge mbalimbali pamoja na Wakuu wa Wilaya za Dar.

Ramadhani Madabida, Mwenyekiti wa CCM amesema kifo cha Masaburi ni pigo si tu kwa familia yake bali pia Chama Cha Mapinduzi.

Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliojitokeza kuuaga mwili wa Masaburi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana Masaburi alichuana vikali na Kubenea katika kinyang’anyiro cha ubunge katika Jimbo la Ubungo ambapo (Masaburi) alishindwa alishindwa kwa tofauti ya kura 28,000.
 
Amekosea,alitakiwa aendelee na mambo mengine,Dr.Didas Masaburi ni mkristo na ukristo unamtambua make mmoja tu,kwa Yohana kubisha inamaana anakosoa hata viongozi wa kanisa waliokuwepo hapo msibani kua no wanafiki,watakujaje kumzika mtu mwenye wake zaidi ya mmoja wakati hiyo haikubaliki kwa baadhi ya madhehebu ya kikristo.
 
Katika hali ya kushangaza na kutia shaka ni pale msemaji wa familia ya marehemu alipo kuwa akisoma historia ya familia na kusema kuwa marehemu ameacha mke mmoja na wajane wawili ambapo kauli hiyo imeleta utata na kuleta miguno kwenye msiba huo.

Alipopewa nafasi ya kuzungumza rais magufuli alikuja na kukanusha na kusema kuwa masaburi alikuwa na wake 4 ama 5 na alikuwa na watoto zaidi ya 20 hivi.

je hii inamaana gani kwa jamii?

Mke mmoja na wajane wawili? Inakuwaje?
 
Yohana Fungi amekosea,alitakiwa aendelee na mambo mengine,Dr.Didas Masaburi ni mkristo na ukristo unamtambua make mmoja tu,kwa Yohana kubisha inamaana anakosoa hata viongozi wa kanisa waliokuwepo hapo msibani kua no wanafiki,watakujaje kumzika mtu mwenye wake zaidi ya mmoja wakati hiyo haikubaliki kwa baadhi ya madhehebu ya kikristo.
umenena vyema
 
Japo sipo kwenye eneo la Msiba, lakini hakuna mabishano yoyote! .

Wenye haki kutoa historia ya marehemu misibani ni wafiwa tuu na haswa msemaji wa familia na sio mfariji.

Rais Magufuli sio familia ya Masaburi, kama msemaji amesema ameacha mke mmoja, wawili or whatever, hakuna mwingine mwenye uwezo wa kubalisha hilo usimsingizie rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mara nyingi Wakristu wanakuwa na ndoa moja tuu rasmi ya kanisani inayotambulika rasmi, ya mke mmoja tuu na hao wanawake wengine wawili ni vimada tuu japo wote wanaweze kuwa na vyeti vya ndoa za kiserikali.
Vimada kwa kwa kawaida hawanaga hesabu, wengine wamezalishwa tuu ila nao wanataka kujiita wake! .
Pasco
 
Back
Top Bottom