Rais Magufuli aongeza muda kwa usajili wa laini kwa alama za vidole

TUNAMSHUKURU MH.RAIS,LAKINI BADO PIA HUO MUDA NI MDOGO MNO,SPEED YA JAMAA WA NIDA NI NDOGO MNO.
#TUNAOMBA AONGEZE MIEZI 3,
#USAJILI WA LINE KWA NJIA ZA KADI YA KITAMBULISHO CHA TAIFA TU NDIO UKUBALIKE.
#WANAOPOTEZA SIMU ZAO IWE NI LAZIMA KUZI RENEW KWA KITAMBULISHO CHA TAIFA.
#GHARAMA ZA AFIDAVITY ZIONDOLEWE KABISA PAMOJA NA AINA ZOTE ZA TOZO NDOGONDOGO ZIFUTWE,KWANI VITAMBULISHO HIVI VIMETENGENEZA DILI TAYARI KWA BAADHI YA WATENDAJI WA NGAZI MBALIMBALI.
#
Atuongeze Miaka Mingine Minne
 
Hivi inakuwaje kwa wale watu ambao wanaidhi Tanzania lakini sio watanzania,kwahyo wao watasajili kwa kutumia kitambulisho gani?...ninavyojua wenyewe hawana kitambulisho cha NIDA,au hawataruhusiwa kuwa na laini za Tanzania? Mfano Mwinyi Zahera,Niyonzima ,Juma sharobaro,mabalozi n.k?,...ufanunuzi please!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii dah, ni vyema kushuku kila kauli inayotoka katika kinywa cha mwanadamu, maana huwezi kujua kesho atazungumza nini.

Watu wanakana maandiko yao (Serikali 2 Vs 3); wengine wanalaumu mkuu kuwatumia wana zuoni. kwenye nafasi za uongozi leo lakini kesho nao wakiwa kama wanazuoni wanateuliwa kuwa viongozi wanaishukuru mamlaka ya uteuzi.

Wengine leo hasifungiwe mtu hadi Dec, mara kama A hajakamilisha kazi yake basi B hasimnyime mnyonge mawasiliano sababu ya uzembe wa A mara baada ya 20 tu fungia wote.

Haya baba, tutajitahidi tusajiri line zetu kwa jasho na damu ili tuendelee kuwasiliana. Ikishindikana basi tutakupa tena mi 5 mingine kwa ahadi ya kuturudishia tena mawasiliano yetu.

Lakini hongera sana baba kwa kuonesha njia, maana tulikuwa tunajificha kwenye kichaka cha kauli ya Mbeya na Moro na kile cha msaidizi wako wa ndani kule mjengoni Dom ndio vimeshachomwa moto.
 
The President acts like a high school PREFECT!

Hii nchi haina sheria?

Bunge mpaka muda huu halijatunga sheria za usajili wa laini za simu?

TCRA hawana miongozo na kanuni mpya za usajili wa alama za vidole?

Yaani Rais wa nchi anaweza tu kutoa hisani na kuelekeza lolote na kutoa sanctions kuhusu lolote jinsi apendavyo?

So much politics and abuse of power (potential abuse of power).

Hivyo, baada ya tarehe 20 kupita, hapatakuwa na watu watakaosajili laini mpya zingine?

What do they mean by "deadline"?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The President acts like a high school PREFECT!

Hii nchi haina sheria?

Bunge mpaka muda huu halijatunga sheria za usajili wa laini za simu?

Yaani Rais wa nchi anaweza tu kutoa hisani na kuelekeza lolote na kutoa sanctions kuhusu lolote jinsi apendavyo?

Hivyo, baada ya tarehe 20 kupita, hapatakuwa na watu watakaosajili laini mpya zingine?

What do they mean by "deadline"?

Sent using Jamii Forums mobile app
Deadline kwa maana ya kwamba hautaweza fanya mawasiliano itakapofika hiyo siku iliyotangazwa kama haujasajiri kwa alama za vidole. Haimaanishi zoezi la usajiri halitaendelea usajiri utaendelea kama kawaida ila usipokamilisha kwa alama za vidole upande wako utasitishiwa mawasiliano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli leo Dec 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwataka Watanzania kusajili laini zao kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na TCRA, JPM ametangaza kuongeza siku 20 kwa ambao hawajakamilisha zoezi hilo.
_
Rais Magufuli amefanya usajili huo wa laini yake kwa alama za vidole Chato, Mkoani Geita ambapo ameongeza siku 20 kuanzia Jan 01, 2020 hadi Jan 20, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia December 31, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.
_
Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya siku 20 alizoongeza kukamilika hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa “usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi, unaepusha uhalifu”
Strange, Mr president, kama mtu hana kitambulisho cha NIDA anafanyaje kukipata. Limiting step ni ipi? Huyu amesoma chemistry, anajua mambo ya rate limiting step/rate limiting step katika chemical reactions! The slowest step is the one that detrmines the end of the reaction. sasa kama NIDA hawatoi vitambulisho, hizo 20 days ni useless!
 
Rais John Magufuli ameongeza siku 20 kuanzia kuanzia Januari 1-20 kwa watu wote watakaoshindwa kusajili laini zao za simu ifikapo Desemba 31.

Pia, leo Desemba 27 Rais amefanya usajili wa laini yake kwa kutumia alama za vidole

Mwananchi

====
View attachment 1304669

Muda wa kukaa madarakani anaongeza lini?

Hii nchi bila Dr John P. Magufuli tungeipoteza kabisa kwa mafisadi na vibaraka wao.
 

hilo liko wazi ndugu ukitaka kujua ukweli, tafuta card ya voda iliyokwishasajiliwa mpigie mwenye namba ya voda inaanza sauti kuwa 'laini yako haijasajiliwa kwa alama ya vidole kama inavyotakiwa kisheria.....'

niliudhika nikawapigia eti najibiwa samahani hiyo sauti imewekwa kimakosa lkn baadae wataitoa. nikamuuliza dada pamoja na wasomi wa it mlionao wameshindwa kuweka mfumo thabiti wa kutifautisha cards zenye usaili na zisizosajiliwa iki kutuondolea kero ya kusubiri dk nzima kupisha tangazo lenu? alibaki kuuma midomo.

nahisi site tutapigea pini watuambie tena tukaunge foleni maduka yao awamu hii tukiwa na kitambulisho na barua ya kiapo cha mahakama. huwa najisemea tu, teknolojia inatukimbiza tofauti ma mwendo wa gari letu

Sent using Jamii Forums mobile app
They are not serious, tutashuhudia vituko!kumbuka inshu ya simu fake..
 
Back
Top Bottom