Rais Magufuli aombwa kuteketeza meno ya tembo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
JPM aombwa kuteketeza meno ya tembo.jpg

Kwa ufupi

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kampeni hiyo, Shubert Mwarabu amesema, endapo meno hayo yatauzwa yatachochea ujangili kwani itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida.

By Colnely Joseph, Mwananchi Digital

Dar es Salaam. Wanahalakati wa Okoa Tembo wa Tanzania wamemshauri Rais John Magufuli kuteketeza shehena ya meno ya tembo yaliyohifadhiwa ghalani ili kuepuka gharama za uhifadhi na ulinzi.

"Taiwan na China ambao ni miongoni mwa wateja wakubwa wa meno hayo wamefunga biashara hiyo kwenye masoko ya ndani hivyo haina sababu kutafuta wateja bali yachomwe," alisema.

Mwarabu amesema ili kuthibitisha kuwa biashara hiyo ni haramu, serikali haina budi kuonesha mfano wa wazi kwa kuteketeza meno hayo. chanzo.JPM aombwa kuteketeza meno ya tembo

KUCHOMA MOTO MENO YA TEMBO HAKUTAZUIA WAWINDAJI HARAMU WA MENO YA TEMBO KUTOWAUWA HAO TEMBO USHAURI SIO MZURI ALIOTOWA MWENYEKITI WA KAMPENI SHUBERT MWARABU.
 
Hayawezi kuwekwa makumbusho za taifa kama vivutio vya utalii?
 
Watayaiba wajanja wapo wengi Tanzania.

Itapigwa kelele sana lakini hayo meno ya Ndovu yatabaki hivyo hivyo bila kuteketezwa, unajua kwanini?!
Kuna wajanja wamekuwa wakipiga hela kwa muda mrefu sana na wakatajirika mno.
Wajanja hao wamekuwa wakitumia mwanya wa serikali kujua tu idadi ya hayo meno na sio urefu wake, kwa hiyo wamekuwa wakiyakata kama kuyapunguza urefu na kuyauza.
Huwa wakikata vipande vidogo vidogo sana, ila kutokana na uwingi wa hayo meno huwafanya wapate kilo nyingi sana.
Ndio maana kila mtu anayepelekwa pale Ivory Room kufanya kazi ni lazima atajirike. Kama ilivyokuwa kwa Fikiri Madinda ambaye alikuwa dereva tu.
Au Juma Ngida aliyekuwa akiitwa Nyamihela. Kwa hiyo wenye kufaidika nayo wala hawataki yateketezwe.

Ova
 
Hivi kama wanyama wenyewe wameshauawa ambayo tayari ni hasara imeshapatikana kuna ubaya gani wa kuyauza kwenye soko halali (kama lipo) ili angalau kujipunguzia hasara? Kwani hayo meno yachomwe au yasichomwe ukweli wa kuwa yana thamani na kuna soko lake utabaki palepale. Ile kusema kuwa kama yakiuzwa yatachochea ujangili kwa vile itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida ni habari ya kiharakati tu kwa sababu ukweli kuwa faida na soko vipo ni kitu kinachojulikana siku zote. Sana sana juhudi zielekezwe kwenye kuzuia ujangili lakini pale inapotokea kuwa majangali yanakamatwa baada ya kuwa yameshawaua hao tembo basi angalau tukubali tu kupunguza hasara kwa kuyauza meno yaliyokamatwa kwenye soko halali.
 
Ya kwetu yahifadhiwe tu. Huko kwingine, wanateketeza robo wakati wameuza robo tatu kimagendo.
 
Akayatunze ikulu. Hakuna kuteketeza. Wanaoshinikiza kwa hakuna hata chura.
 
View attachment 343198

Kwa ufupi

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kampeni hiyo, Shubert Mwarabu amesema, endapo meno hayo yatauzwa yatachochea ujangili kwani itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida.

By Colnely Joseph, Mwananchi Digital

Dar es Salaam. Wanahalakati wa Okoa Tembo wa Tanzania wamemshauri Rais John Magufuli kuteketeza shehena ya meno ya tembo yaliyohifadhiwa ghalani ili kuepuka gharama za uhifadhi na ulinzi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kampeni hiyo, Shubert Mwarabu amesema, endapo meno hayo yatauzwa yatachochea ujangili kwani itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida.

"Taiwan na China ambao ni miongoni mwa wateja wakubwa wa meno hayo wamefunga biashara hiyo kwenye masoko ya ndani hivyo haina sababu kutafuta wateja bali yachomwe," alisema.

Mwarabu amesema ili kuthibitisha kuwa biashara hiyo ni haramu, serikali haina budi kuonesha mfano wa wazi kwa kuteketeza meno hayo. chanzo.JPM aombwa kuteketeza meno ya tembo

KUCHOMA MOTO MENO YA TEMBO HAKUTAZUIA WAWINDAJI HARAMU WA MENO YA TEMBO KUTOWAUWA HAO TEMBO USHAURI SIO MZURI ALIOTOWA MWENYEKITI WA KAMPENI SHUBERT MWARABU.

Yachomwe moto tuu
 
Itapigwa kelele sana lakini hayo meno ya Ndovu yatabaki hivyo hivyo bila kuteketezwa, unajua kwanini?!
Kuna wajanja wamekuwa wakipiga hela kwa muda mrefu sana na wakatajirika mno.
Wajanja hao wamekuwa wakitumia mwanya wa serikali kujua tu idadi ya hayo meno na sio urefu wake, kwa hiyo wamekuwa wakiyakata kama kuyapunguza urefu na kuyauza.
Huwa wakikata vipande vidogo vidogo sana, ila kutokana na uwingi wa hayo meno huwafanya wapate kilo nyingi sana.
Ndio maana kila mtu anayepelekwa pale Ivory Room kufanya kazi ni lazima atajirike. Kama ilivyokuwa kwa Fikiri Madinda ambaye alikuwa dereva tu.
Au Juma Ngida aliyekuwa akiitwa Nyamihela. Kwa hiyo wenye kufaidika nayo wala hawataki yateketezwe.

Ova
Shikamoo JF, hapa kila issue lazima apatikane insider!
 
Hivi kama wanyama wenyewe wameshauawa ambayo tayari ni hasara imeshapatikana kuna ubaya gani wa kuyauza kwenye soko halali (kama halali kama lipo) ili angalau kujipunguzia hasara? Kwani hayo meno yachomwe au yasichomwe ukweli wa kuwa yana thamani na kuna soko lake utabaki palepale. Ile kusema kuwa kama yakiuzwa yatachochea ujangili kwa vile itaibuka imani miongoni mwa watu kuwa meno hayo yana soko na faida ni habari ya kiharakati tu kwa sababu ukweli kuwa faida na soko vipo ni kitu kinachojulikana siku zote. Sana sana juhudi zielekezwe kwenye kuzuia ujangili lakini pale inapotokea kuwa majangali yanakamatwa baada ya kuwa yameshawaua hao tembo basi angalau tukubali tu kupunguza hasara kwa kuyauza meno yaliyokamatwa kwenye soko halali.
Umesema jambo la muhimu sana
Lengo la kuyachoma ilikuwa ni Kutoa u kuonyesha hisia kwa jumuiya za kimataifa kwamba Tembo ni bora zaidi na muhimu kuliko pembe zake.. Lakini kwa hali iliyopo sasa ya ukuaji wa technology ni wazi mambo yote yanafahamika kuanzia masoko mpk matumizi.. Ni vyema yangeuzwa halafu zile pesa ziende direct kwenye jitihada za kupambana na ujangili
Mfano Kutoa ekimu
Kununua vifaa
Kulipa wale wanaowalinda wanyamapor
 
Back
Top Bottom