Dar: Madaktari wamuangukia Rais Magufuli, amwaga ajira 1,000 za Madaktari, aelezea alivyozimia siku mbili mbele ya Zainabu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 20, Febuari, 2020 anazungumza na Madaktari pamoja na watumishi wa Sekta ya Afya katika Hafla Maadhimisho ya Siku ya Madaktari Nchini inayofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dsm.

======

UPDATES:

=> Rais anakutana na Chama cha Madaktari Nchini katika Mkutano unaoendelea kwenye Ukumbi wa JNICC, Mkutano huo unafanyika kuelekea maadhimisho ya miaka 55 ya Chama cha Madaktari Tanzania.

=> Rais wa Chama cha Madaktari nchini, MAT, Dkt. Elisha Osati, amemuomba Rais Magufuli kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti katika huduma za Afya, ili kuepuka kila Mtoa huduma kujipangia bei na kusababisha usumbufu.

Dkt. Osati, Rais MAT: "Sisi tuna madaktari vijana ambao wako tayari kufanya maeneo yote mijini na vijijini,tunachokiomba ni kwamba katika hospitali ambazo tumejenga na kwa upungufu ambao tunao tunaomba kuongeza vibali vya ajira "

Dkt. Osati, Rais MAT: "Kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuamrisha watoa huduma za afya kuwekwa ndani pale wanapokosea. Hii imekuwa ni changamoto sana kwetu, inatuvunjia heshima watumishi wa kada ya afya”

Dkt. Osati, Rais MAT: Tabia ya Viongozi wa kisiasa kuwaweka ndani Madaktari, Wafamasia na Manesi inatudhalilisha sana, inaondoa heshima kwenye taaluma yetu, Sheria ya kuwaweka watu ndani saa 48 imekuwa mwiba kwetu, Rais Magufuli tunaomba utoe maelekezo Viongozi wafuate miongozo”-

Naibu Waziri wa Afya - Dk Faustine Ndugulile: Sekta ya afya sasa inafanya vizuri, hongera Mhe. Rais Magufuli kwa uwekezaji mkubwa ulioamua kuufanya katika sekta hii muhimu kwa watanzania”

Naibu Waziri wa Afya - Dk Faustine Ndugulile: “Sasa hivi nchi imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya kwani kuna baadhi ya magonjwa hayapo kwa sasa yakiwemo ya donda koo, kifaduro, pepopunda na kuharisha, tumefunga baadhi ya wodi za magonjwa hayo”

Naibu Waziri wa Afya - Dk Faustine Ndugulile: “Mtoto anayezaliwa sasa hivi Tanzania ana uhakika wa kuzaliwa na kwa afya njema, wenye kumbukumbu miaka ya 40/50 kina mama walikuwa wakipata ujauzito ilikuwa ni pata potea ,mama anapata ujauzito mara 10 anaishia kupata watoto watatu, sasa tumepiga hatua sana".

Godfrey Mnyaga: Mwaka 2016 walileta tena mitihani hiyo, nikauliza kama utaratibu ni ule wa mwaka 2015. Waliposema ndio, nilikataa kupokea mitihani. Walichukua Wanafunzi wangu na kuwapeleka katika Vyuo vingine lakini haikuwa mwisho. Nikamwandikia Katibu Mkuu, hakujibu. Godfrey Mnyaga: Nikaenda kwa Mkuu wa Mkoa, alinisaidia sana aliwaandikia wahusika, hawakujibu. Suala langu likaenda TAKUKURU, wakafanya uchunguzi Wizara ya Afya wakakuta kuna kasoro na hoja yangu ilikuwa ya msingi. TAKUKURU walinipa mrejesho wa maandishi ninayo.

Godfrey Mnyaga: Nikaandika barua kwenye ofisi yako (Rais) na ofisi ikamwelekeza Katibu Mkuu wa Afya. Katibu aliniita na niliongea naye akaona nilikuwa nimeonewa, akasema nirudi Mwanza. Baada ya muda akaniandikia barua ambayo ni tofauti na tulivyokuwa tumefanya kikao. Lakini watu wa Serikali hawatumi Watumishi wala vitendea kazi na tunaingia gharama. Tuna kodi nyingine Serikalini. Ombi langu kubwa naomba unisaidie malalamiko yangu

Rais Magufuli: Leta hizo nyaraka na unadai kiasi gani?

Mnyaga: Nadai Milioni 24. Ninachoomba hawa Watendaji wa Wizara ya Afya wanifidie kwani nimepoteza hela zangu na nilikata tamaa kuwekeza katika eneo hilo. Hoja nyingine, Kwenye Vituo Binafsi tunaambiwa tutoe baadhi ya huduma bila malipo lakini mimi naamini zimefadhiliwa sehemu. Kwanza nilifunga kabisa Chuo. Nilikuwa na mkopo Benki, imenitia msukosuko mpaka leo nimefilisika. Naishi maisha si yangu. Wale wahusika bado wanaendelea na ajira zao. Taarifa ya TAKUKURU ilisema itawachukulia hatua lakini bado

Dkt. Rahma Ingola: Sisi watu wa maabara tunakutana na 'risk' nyingi sana. Mimi ni Radiologist lakini tunahitaji 'protective gears'. Mimi siku chache ziliopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho kwa kukaa sana kwenye kompyuta. Tunaomba tulindwe kwenye haya

Dkt. Wilson Chotamganga: Nina uchungu na mama wajawazito wanaokufa Vijijini na watoto wachanga. Nakuomba kule zijengwe nyumba wajawazito wawe wanasubiria pale. Vijijini nimeona wakina mama wanavyoteseka kutokana na mazingira, Wanatoka mbali na kujifungua njiani

Dkt. Emmanuel Swai: Kuna shida kuwa, utakuta MD wa Sinza hapati 'house allowance' lakini wa Muhimbili anapata. Suala lingine ni kuhusu NHIF, utakuta 'Specialist' anayefanya kazi 'Sinza Hospital' kuna dawa hawezi kutoa kutokana na sehemu alipo lakini utaalamu anao

Physiotherapist Pricila Msele: Mimi nimeajiriwa kwenye Utumishi wa Umma mwaka 2007 na sijawahi kupanda daraja hata 1. Sababu ni kwamba hatujafanyiwa categorization nimepoteza madaraja 4. Wiki iliyopita nimejibiwa kuwa eti mpaka wewe(Rais) usaini barua za categorization

Rais Magufuli: Leo nina furaha kubwa sana kwa sababu nimekutana na watu muhimu sana katika Afya za Watanzania. Nina historia nzuri sana na Madaktari kwa sababu nimeshashughulikiwa na Madaktari.

Rais Magufuli: Nakumbuka nikiwa Naibu Waziri nilitolewa jino Muhimbili. Niliamka baada ya siku 2 nikiwa ICU, hivyo ninafahamu wasingekuwa madaktari nisingepona. Lakini pia niliwahi kuwa ICU nikiwa Dodoma nilipoamka nikakuta nahudumiwa na Dokta Zainabu.Hivyo Dokta Zainabu ananijua kila kitu ingawa mimi simjui kila kitu.

Rais Magufuli: Rais wa MAT amezungumza hapa wanahitaji jengo kwa ajili ya shughuli zao. Nimemuuliza hilo jengo la ghorofa ngapi, akajibu 3. Nikamuuliza mmekadiria kiasi gani, akasema bilioni 3. Nikashangaa ghorofa 3 bilioni 3! Nikaona hapo kuna ufisadi wa aina fulani. Milioni 500 zinajenga Kituo cha Afya, kwenye hiyo hela kuna Vituo vya Afya sita maana yake mtachangishwa ninyi wanachama mpaka mchoke. Kama MAT wanahitaji jengo, mimi nitawapa jengo bure. Tutatafuta hata hapa Dar, ofisi nyingi zimehamia Dododma.

Rais Magufuli: Sijawahi kutoa jengo kwa bodi nyingine kama kwa Wahandisi lakini natoa kwa Madaktari kwa kuwa natambua kazi kubwa mnazofanya kwa Watanzania. Madaktari oyeee, Madaktari safiiii. Msiwe na wasiwasi ninaposema oyeee, sitasema CCM ni Madaktari tu leo

Rais Magufuli: Serikali imeajiri Watumishi 13,479 katika kada ya Afya na kufanya Watumishi wa Afya hadi Julai 2019 kufikia 98,987 wakiwa wanalipwa Bilioni 830. Sekta binafsi imeajiri watu 18,094. Serikali imewasomesha Watumishi wa Afya ndani na nje ya Nchi wapatao 923

Rais Magufuli: Tunahitaji kufanya upasuaji hadi wa kichwa. Nakumbuka Askofu Ruwa'ichi alikuwa apoteze maisha lakini amekuja pale mimi sikuamini. Lakini hawa watu Wahaya, Wachaga na wanani waliopo pale wakasimamia kazi mpaka akapona kwa sababu palikuwa na vifaa

Rais Magufuli: Mmezungumza kuhusu Bima ya Afya, nakubaliana na ushauri wenu. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na watu Milioni 3.2 sasa wamefikia karibu milioni 4.9. Tunaangalia namna gani tunaweza kuboresha Sheria katika hilo ili kila mtu awe na Bima ya Afya.

Rais Magufuli: Ninachosema ni kuwa Madaktari hawatakiwi kupata 'frustrations' yoyote inayoweza kutekelezwa na Wizara husika. Inatakiwa shida zao zishughulikiwe kwa haraka na udharura kwa sababu wao pia wanawashughulikia wangojwa kwa morali hiyo.

Rais Magufuli: Nakubaliana na ninyi, haiwezekani mtu ambaye ni 'professional' kila mahali unamuona mtu mwingine anatishia kumweka ndani tu. Haiji wala haifurahishi. Unafanya upasuaji unatoka kule bahati mbaya damu zinavuja unawekwa ndani. Si atakufa na unayemtibu?

Rais Magufuli: Najua siku hizi hamuwekwi ndani sana, sisi tumeambiana huku kwetu wala msiwe na wasiwasi. Najua akikuweka ndani kesho akija anaumwa na wewe utamuweka ndani. Ila msifanye hivyo kwa kuwa utakuwa unabeba dhambi kwa Mungu, kazi yenu mkaifanye vizuri.

Rais Magufuli: Nafahamu kuna Madaktari takriban 2,700 hawajaajiriwa bado, hili nalifanyia kazi. Nafikiri tunaweza kuanza polepole hata kuchukua 1,000. Waziri wa Utumishi tunaweza?

Waziri Mkuchika: Ndio tunaweza

Rais Magufuli: Basi tuanze na kuajiri Madaktari 1000 sasa





Aidha, katika maadhimisho hayo baadhi ya Madaktari walipata fursa ya kueleza masuala mbalimbali yanayowakabili mbele ya Rais Magufuli.

Katika hilo baadhi ya Madaktari walieleza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao. Mathalani, Dokta Emmanuel Swai alieleza kuwa Madaktari bado wanakosa pesa ya makazi 'house allowance' kwa Madaktari wa hospitali ya Sinza huku Madaktari wa Muhimbili wakipata. Sambamba na hilo, Dokta Emmanuel Swai Aliongeza kuwa, katika suala la Bima ya Afya (NHIF) kuna Madaktari wakufunzi wanafanya kazi Sinza lakini kuna dawa hawawezi kuzitoa kutokana na sehemu alipo ilihali utaalamu anao.

Naye, Daktari Pricila Msele, anaeleza kuwa tangu ameingia kwenye utumishi wa umma mwaka 2007 hajawahi kupandishwa daraja hata moja ameajiriwa mwaka 2007 kwa sababu ya kutofanyiwa 'categorization' huku wakiambiwa wanasubiri Rais apitishe jambo hilo.

Kwa upande wake Rais Magufuli, alieleza furaha yake kukutana na Madaktari huku akieleza namna anavyotambua mchango wao mkubwa katika suala zima la kushughulikia afya za Watanzania.

Akiongelea kuhusu kuwapa jengo bodi ya Madaktari Rais Magufuli alisema kuwa "Sijawahi kutoa jengo kwa bodi nyingine kama kwa Wahandisi lakini natoa kwa Madaktari kwa kuwa natambua kazi kubwa mnazofanya kwa Watanzania".

Sambamba na hilo, Rais Magufuli alieleza kuwa, Rais wa MAT amezungumza hapa wanahitaji jengo kwa ajili ya shughuli zao. Nimemuuliza hilo jengo la ghorofa ngapi, akajibu 3 - Nikamuuliza mmekadiria kiasi gani, akasema bilioni 3. Nikashangaa ghorofa 3 bilioni 3! Nikaona hapo kuna ufisadi wa aina Fulani. Hivyo, Rais Magufuli alifafanua kuwa "Milioni 500 zinajenga Kituo cha Afya, kwenye hiyo hela kuna Vituo vya Afya sita maana yake mtachangishwa ninyi wanachama mpaka mchoke - Kama MAT wanahitaji jengo, mimi nitawapa jengo bure. Tutatafuta hata hapa Dar, ofisi nyingi zimehamia Dododma"

Aidha, kuhusu Bima ya Afya Rais Magufuli alisema "Mmezungumza kuhusu Bima ya Afya, nakubaliana na ushauri wenu. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na watu Milioni 3.2 sasa wamefikia karibu milioni 4.9 - Tunaangalia namna gani tunaweza kuboresha Sheria katika hilo ili kila mtu awe na Bima ya Afya"

Kuhusu suala la Watumishi wa wizara ya afya Rais Magufuli alisema kuwa "Serikali imeajiri Watumishi 13,479 katika kada ya Afya na kufanya Watumishi wa Afya hadi Julai 2019 kufikia 98,987 wakiwa wanalipwa Bilioni 830 - Sekta binafsi imeajiri watu 18,094. Serikali imewasomesha Watumishi wa Afya ndani na nje ya Nchi wapatao 923"

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli amesisitiza kuwa Madaktari hawatakiwi kupata 'frustrations' yoyote inayoweza kutekelezwa na Wizara husika - Inatakiwa shida zao zishughulikiwe kwa haraka na udharura kwa sababu wao pia wanawashughulikia wangojwa kwa morali hiyo
 
Back
Top Bottom