Rais Magufuli anaweza kuwa mpango wa Mungu kututawala

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,114
kwa wale wana dini watanielewa haraka nikisema kila jambo hutokea kwa faida. ukiumwa ni ibada kwamba wewe si mkamilifu. ukifiwa ni ibada kwamba wewe si wa kudumu. ukilala njaa ni ibada kwamba wewe ni mhitaji. yaani kila jambo lina faida yake hata kama lina maumivu.

kwa vile mimi sio nabii nitasema inawezekana rais huyu ni mpango wa Mungu atutawale. sina hakika kwa vile sijaongea na Mungu. ila kwa akili za kawaida naweza sema ni mpango wa Mungu maana tulibweteka.

kuna wakati Mungu anakupatia jaribu, mtihani ili kukumbusha wajibu wako. namkubali Muumba maana anasema anatupa na mlango wa kutokea hilo jaribu. naam hapa pia tutapa mlango wa kutokea.

mara nyingi tulisahau kuchagua viongozi kwa kutumia akili tulikua tunatumia uchama!!

kama taifa hatuandai misingi ya kuendesha nchi bali tunategemea upeo wa kiongozi ndio uongoze nchi. yaan kadri ya mtawala atakavyo ndivyo na taifa liwe. akiwa wa hovyo taifa hugubikwa na viongoz wa hovyo. akiwa mwenye busara taifa hujaa viongoz waliowengi wenye busara . yaan tunakua hatujui tunaenda wap itategemea nani atakuja hiyo kesho.

kwa utawala huu nina hakika si ccm wala wapinzani wakipata fursa ya kuanda misingi ya kuongoza nchi watatulia na kuandaa vizuri. japo kwa wakati huu hiyo fursa siioni kama itatokea. lakn wakipata hiyo nafas watakuja wakiwa na mtizamo mpana wa kundaa mifumo ya kutuongoza hata kama wao hawapo.

na ikitokea kupiga kura hatutaangalia chama tutaangalia mtu ana mwono gani hadi kufaa kupewa ridhaa ya kuongoza taifa. yaan kama bado kuna watu wataongozwa na uchama watakua na matatizo ya kiakili. nina hakika nchi tunazoona zinabadirishana vyama kutawala walipita huku wakaumia na sasa hawachagui vyama, bali humsikiliza mtu na hufatilia historia yake ndipo huumpa kura.

yaan huyu rais wetu mimi naamin ni mpango wa Mungu ili kuharakisha mageuzi katika nchi yetu ambayo yangechukua miaka mingi kuyafikia. yaani sasa tukidai katiba bora tutaeleweka zaid kuliko zamani. huyu kwangu mimi ni mkombozi . ni bora huyu anang’ata kabisa kuliko viongozi waliotangulia waliokua wanang’ata na kupuliza. tulikua tunawaona ni wema huku hata wao wanatusahaulisha tusijue wajibu wetu.

twende rais wetu tunyooshe hadi watanzania tulio wengi tuwe wamoja.
 
Mh. Rais ana nia njema kabisa kwa wananchi wake. Hata kama ana mapungufu yeye kama binadamu ila kazi anazopiga ni dhahiri anatamani nchi isonge mbele kimaendeleo.
 
Nazani umemaanisha kinyume maana hakuna mungu wa kuwaletea watu wake jinamizi aka mumias ama mnyonya damu ili liwatese watu nchini mwao huu utakuwa ni mpango wa shetan
 
Mungu anachukizwa na kiongoz mwenye kiburi, majivuno na mkosefu wa hekima. Mungu hafurahishwi na ukiukwaji wa haki za watu wa nchi yake (e.g: kubomolea wananchi makazi yao bila ya kuwalipa fidia). Mungu wa Isaka, Ibrahim na Yakobo, anataka kudhihirisha kitu juu ya watawala kama hawa, ambao wamekua wakilumbana na makanisa na watumishi wake (eg; Maaskofu na Wachungaji) Ni suala la muda tu.
 
Toka lini Mu..aji,Mwenye ro...ho mbaya,mropok...aji,mwenye vis...asi akawa mpango wa Mungu?Labda ni mpango wa ibilis shetwani.
 
Mh. Rais ana nia njema kabisa kwa wananchi wake. Hata kama ana mapungufu yeye kama binadamu ila kazi anazopiga ni dhahiri anatamani nchi isonge mbele kimaendeleo.
Nia njema kuongeza Kubomoa nyumba za masikini?
Nia njema kukuta sukari inauzwa 1800@kg na sasa ni 2500+@kg
Nia njema watu kupotea,kupigwa hadharani na jeshi la polisi,kuvamiwa vituo vya radio, wabunge na wanafunzi kumiminiwa risasi na mkuu bila kutoa karipio lolote ndio nia njema?
Nia njema kukuta wananchi wanaangalia bunge laivu na kuzuia?
Nia njema kutoendeleza mchakato wa katiba mpya mbayo ndio matakwa ya raia?
Eti ndio nia njema?
Au nia njema ni kusema,"nina nia njema"
 
Aweza kuwa kiongozi bora,tatizo watangulizi hawakutimiza wajibu wao mfunda ama hakuwapa nafasi.
 
Mamlaka yote yatoka kwa Mungu lakini kuna watu baadhi hutumia mabavu kuyapata mamlaka na wakiyapata basi hujiona wao ndio miungu.

Mwisho wa ubaya aibu.
 
kwa wale wana dini watanielewa haraka nikisema kila jambo hutokea kwa faida. ukiumwa ni ibada kwamba wewe si mkamilifu. ukifiwa ni ibada kwamba wewe si wa kudumu. ukilala njaa ni ibada kwamba wewe ni mhitaji. yaani kila jambo lina faida yake hata kama lina maumivu.

kwa vile mimi sio nabii nitasema inawezekana rais huyu ni mpango wa Mungu atutawale. sina hakika kwa vile sijaongea na Mungu. ila kwa akili za kawaida naweza sema ni mpango wa Mungu maana tulibweteka.

kuna wakati Mungu anakupatia jaribu, mtihani ili kukumbusha wajibu wako. namkubali Muumba maana anasema anatupa na mlango wa kutokea hilo jaribu. naam hapa pia tutapa mlango wa kutokea.

mara nyingi tulisahau kuchagua viongozi kwa kutumia akili tulikua tunatumia uchama!!

kama taifa hatuandai misingi ya kuendesha nchi bali tunategemea upeo wa kiongozi ndio uongoze nchi. yaan kadri ya mtawala atakavyo ndivyo na taifa liwe. akiwa wa hovyo taifa hugubikwa na viongoz wa hovyo. akiwa mwenye busara taifa hujaa viongoz waliowengi wenye busara . yaan tunakua hatujui tunaenda wap itategemea nani atakuja hiyo kesho.

kwa utawala huu nina hakika si ccm wala wapinzani wakipata fursa ya kuanda misingi ya kuongoza nchi watatulia na kuandaa vizuri. japo kwa wakati huu hiyo fursa siioni kama itatokea. lakn wakipata hiyo nafas watakuja wakiwa na mtizamo mpana wa kundaa mifumo ya kutuongoza hata kama wao hawapo.

na ikitokea kupiga kura hatutaangalia chama tutaangalia mtu ana mwono gani hadi kufaa kupewa ridhaa ya kuongoza taifa. yaan kama bado kuna watu wataongozwa na uchama watakua na matatizo ya kiakili. nina hakika nchi tunazoona zinabadirishana vyama kutawala walipita huku wakaumia na sasa hawachagui vyama, bali humsikiliza mtu na hufatilia historia yake ndipo huumpa kura.

yaan huyu rais wetu mimi naamin ni mpango wa Mungu ili kuharakisha mageuzi katika nchi yetu ambayo yangechukua miaka mingi kuyafikia. yaani sasa tukidai katiba bora tutaeleweka zaid kuliko zamani. huyu kwangu mimi ni mkombozi . ni bora huyu anang’ata kabisa kuliko viongozi waliotangulia waliokua wanang’ata na kupuliza. tulikua tunawaona ni wema huku hata wao wanatusahaulisha tusijue wajibu wetu.

twende rais wetu tunyooshe hadi watanzania tulio wengi tuwe wamoja.
Mkuu umesahau namba yako ya simu.
 
Back
Top Bottom