Rais Magufuli anaweza kufanya kama Botswana na Namibia...Inawezekana ni jambo la kuamua tu!!

Nchi ya ya Botswana na Namibia waliweza kuwa na 50/50 shares Katika migodi ya nchi zao kwanini Tanzania tushindwe??

Ni kuamua tu kukaa meza ya majadiliano na wawekezaji na kufikia makubaliano ya kila mmoja anufaike na inawezekana kabisa.

Hapa hatutaki tena watu wa kujifungia ndani ya mahoteli makubwa na kujificha na mikataba.

Wakina Tundu Lissu,Prof Issa Shivji,Reginald Mengi,Prof Kabudi,Ester Matiko,Mzee Mpinga na wengine wengi tu kwa kuanzia ni muhimu ktk timu ya majidiliano

Tunaweza kufanikiwa kabisa kuwa shares 50/50 kama nchi zingine na tukanufaika na madini.

Kama hizo attachment 2 chini zinavyoonyesha

Hata hao wanapigwa tu na Wazungu, sema unaona Botwasna na Namibia wako mbali kiuchumi kwa sababu wako wachache, nchi zote mbili zina wakazi chini ya milioni 2, hata sisi tungekuwa tuko watu milioni 1.5 pia tungekuwa tuko mbali, lkn Botswana wanapigwa sana kwenye Almasi fikiria Botswana ni nchi inayoongoza kwa kutoa Almasi Duniani kwa hali ya kawaida ilipaswa iwe tajiri kama Uswisi lkn bado ni poor developing country, ukiangalia Rasilimali zinazatolewa Namibia ukilinganisha na hali yao ya maisha haziendani kabisa, Namibia ni moja kati ya nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa Almasi na uraniun Duniani lkn bado ni masikini tu, wametupita ndiyo lkn walipaswa wasiwe third world, hivyo kwangu hakuna cha kuiga hapo!
 
Ushauri wako ni UPI Sasa kama haina haja ya kuiga Namibia na Botswana!?
 
Ushauri wako ni UPI Sasa kama haina haja ya kuiga Namibia na Botswana!?

Tujipange sisi wenyewe tu, kama vile Serikali inavyotaka kufanya kujenga smelter tukifanikiwa hilo tutakuwa tumekwenda mbali sana, kwani itatuletea changamoto nyingine nyingi ambazo itatulazimu kuzitatua kama Umeme mwingi na wa uhakika wa kuweza kuendesha smelter, Reli ya uhakika, bandari lazima iongoze ufanisi na hizo zote zitazalisha ajira nyingi tu!
 
Smelters zenyewe bado unataka kujengewa na hao hao Barrick na usifikiri unajengewa bure.

Ndugu yangu biashara ya uchimbaji madini sio kazi ya Serikali ni kazi ya makampuni makubwa.

Serikali inachotakiwa kufanya ni kuwa na sheria nzuri na Taasisi dhabiti za usimamizi na kudhibiti.
 
Afuate utaratibu wa kivunja mijataba na ajiondoe kwenye MIGA na billateral agreements nyingine ili awe salama.
 
Smelters zenyewe bado unataka kujengewa na hao hao Barrick na usifikiri unajengewa bure.

Ndugu yangu biashara ya uchimbaji madini sio kazi ya Serikali ni kazi ya makampuni makubwa.

Serikali inachotakiwa kufanya ni kuwa na sheria nzuri na Taasisi dhabiti za usimamizi na kudhibiti.

Ujengaji wa smelter unawezekana sana tu kama tukijipanga vizuri, kwa kushirikiana na hao hao wawekezaji, swala la maongezi tu na makubaliano au win -win situation kwa pande zote mbili!
 
Tangu lini Ccm ikaitakia mema hii nchi? Usitegemee jambo kama hilo kutokea chini ya kiongozi wa Ccm.
 
Ujengaji wa smelter unawezekana sana tu kama tukijipanga vizuri, kwa kushirikiana na hao hao wawekezaji, swala la maongezi tu na makubaliano au win -win situation kwa pande zote mbili!
Kumbuka comment yako No 41 inapingana Sasa na comment yako No 48.

Umerudi pale pale 50/50 kama ilivyo Namibia na Botswana ulipokataa awali.

Anyway thank you kwa comments zako.
 
Kumbuka comment yako No 41 inapingana Sasa na comment yako No 48.

Umerudi pale pale 50/50 kama ilivyo Namibia na Botswana ulipokataa awali.

Anyway thank you kwa comments zako.

Kwa maoni yangu binafsi wala sioni kama Botswana au Namibia ni mfano wa sisi kuwaiga, kwa sababu nilizozitoa hapo juu, 3/4 ya Almasi inayouzwa Dunia hii inatoka Botswana na Namibia, sasa kama kweli wangekuwa wananufaika leo hii wangekuwa karibia sawa na nchi ya Katar, lkn bado wako nyuma sana, ingawaje wanaonekana wameendelea kama ukiwalinganisha na sisi lkn Kidunia Botswana ni nchi masikini, usisahau wako chini ya watu milioni 2!
 
Hivi kwa mini Mwinyi, Nkapa na JK walishindwa? Ina maana walipata pacent? Hili jambo linawezekana lakini sins hakika kama CCM wanaweza. Hawakufanya kwa miaka 20 iliyopita. Tunawaaminije?
 
Kwa maoni yangu binafsi wala sioni kama Botswana au Namibia ni mfano wa sisi kuwaiga, kwa sababu nilizozitoa hapo juu, 3/4 ya Almasi inayouzwa Dunia hii inatoka Botswana na Namibia, sasa kama kweli wangekuwa wananufaika leo hii wangekuwa karibia sawa na nchi ya Katar, lkn bado wako nyuma sana, ingawaje wanaonekana wameendelea kama ukiwalinganisha na sisi lkn Kidunia Botswana ni nchi masikini, usisahau wako chini ya watu milioni 2!
Mimi sijaongelea maendeleo ya nchi zao.Mimi nimeongelea kufikia 50/50 kati ya Serikali na wawekezaji.

Issue ya maendeleo ya nchi hiyo ni suala lingine wala halimhusu mwekezaji bali viongozi na wanainchi wa nchi husika.
 
Ukitaifisha Kuna mahali utakwama tu....kumbuka majority ya madini huna cha kuyafanyia ndani ya nchi yako mfano, dhahabu na almasi unafanyia nini hapa Tanzania!?!

Ni lazima uyauze huko huko ktk masoko yao ya Ulaya na America.Sasa unaweza ukawekewa ban au vikwazo tu vya kununua dhahabu na almasi yako then yatakuwa hayana thamani tena!!

Haya jamaa lazima tu ushiriki wao uwepo tu ktk ukanda wa nchi masikini kama hizi zetu.Huwezi kujilinganisha na nchi kama China au Urussi.
Asante kwa kunikumbusha mkuu. Ni kweli hawa jamaa wana tentacles everywhere.

Ila Kama negotiations zikikwama, tuka fall apart, kila mtu akaenda kivyake, than tunaweza kutumia opportunity hiyo kuchimba wenyewe.Mbona mtaji unaohitajika sio mkubwa kihivyo.Jambo ambalo haiwezekani anyway.
 
..CEO wa Barrick amesema wako tayari kurekebisha mkataba wao kama walivyofanya ktk mkataba wao na Dominican Republic.

..someni taarifa ya Barrick kuhusu nini kilichoendelea baina yao na Dominican Republic kuona kama huo ndiyo muelekeo mpya ambao Tanzania tunautaka.
... JokaKuu, namna walivyoingia na aina ya mkataba huko inatofautiana na yetu. Huo mgodi -Pueblo Viejo- ulikuwa mali ya Serikali, na ulifanya kazi toka miaka ya 70 na baadae mwaka 1991 ukasimama baada ya bei kushuka na ukosefu wa teknolojia muafaka ya kuchenjua. Hiyo SLA inaipa Serikali ya Dominican Republic nafasi nzuri ya kunufaika kwa kuwa PVDC haikuanza from scratch.

... Among other things, would prefer buying Acacia shares, sit on the Board and become part of decisions made.

... Rekebisha, taarifa ni ya Goldcorp.
 
..ndugu yangu umepotea sana.

..thank u kwa maboresho. Umenielimisha.

..suala la barrick na dominican republic mara ya kwanza kulisikia ni kwenye press conf ya Raisi na Ceo wa barrick.

..kama una info zaidi tuwekee hapa ili tuweze kuona mafundisho yoyote tunaweza kuyapata toka huko.

..kununua shares za barrick is one of the options. Sasa wakati mwingine ni vigumu serikali hii kuwekeza kibiashara kwasababu matatizo nchi hii yako mengi mno na yote ni ya dharura.
 
Nani aliwapa hayo mamlaka ya kusaini kwa niaba yao wakati Serikali ilikuwepo tena ikiwa na Maraisi kamili wa nchi Dr Kikwete na Ben Mkapa?!?

Tanzania as a acountry haikushindwa, ila viongozi hao uliowataja ndiyo chanzo na ndiyo maana wananchi tulio wengi kwa sasa tunataka wakamatwe na kunyongwa.
 
Ndiyo maana tunaomba katiba ipitiwe tena ili hawa viongozi wakamatwe kabla hawajajiua.
Kujua au kunyongwa kwa viingozi sio suluhu ya kunufaika na madini na rasilimali zingine.

Hapa la msingi ni kuwa na sheria nzuri na Taasisi imara za kulinda rasilimali za nchi kwa faida ya wenye nchi yaa wanainchi.
 
Back
Top Bottom