Rais Magufuli anaweza kuenda tofauti na mzee Mwinyi, mzee Mkapa na Kikwete lakini hawezi kuenda tofauti na Nyerere

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Messages
512
Points
1,000

inchaji

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2019
512 1,000
Mwaka 1992 tukiwa wadogo sana mwalimu Nyerere alinyoosha mikono mbele ya ubepari na kuamua kuupokea kwa mikono miwili mfumo wa vyama vingi. Chama dume Chadema kwa bara likazaliwa na chama dume CUF upande wa Zanzibar likazaliwa.

Mzee Mkapa na ndugu Kikwete hawakuwa na nongwa na mfumo huu. Waliuendeleza vilivyo, walicheza na upepo kama bendera. Kama dunia inautaka ubepari na mfumo wa demokrasia sisi Tanzania ni nani?

China na Urusi ni super powers. Kuwafuata ni sawa lakini wao wana teknolojia sisi hatuna. Kuwafuata ni kujipendekeza. isitoshe inchi kama China ina raia wengi sana kiasi raia wa Tanzania ni sawa na raia wa jimbo moja tu huko China. kusema wachina wanaweza kutusaidia ni sawa na kusema jirani yako aache kuwapa wanae chakula awape wa kwako, pathetic. Kumbe kumtegemea mchina ni kupoteza muda tu.

Urusi kwa mfano biashara yake kubwa ni gesi. Na wateja wake wakubwa ni ulaya, Afrika huku joto, mbu, malaria, hana maslahi. Aache kuhangaika na biashara yake ya gas aje kukupatia wewe mkazi wa Chato chandarua cha mbu? thubutu!

Rais Magufuli lazima aelewe kuwa nchi hii haiwezi kuwa ya chama kimoja. Juzi nimekereka sana sijapiga kura serikali za mitaa kwa sababu ya siasa chafu za awamu hii. We have to stop kwa sababu hakuna point ya kulazimisha mfumo wa chama kimoja kwenye Tanzania ya leo ambapo raia wanapata habari kwa njia mbadala hata pale state inabojaribu kizuia.

Chama cha kijani mshaurini vyema mwenyekiti wenu muache kumpotosha.
 

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
4,551
Points
2,000

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
4,551 2,000
Hizi ni stress sio bure
Mkuu lala muda umeenda sana kumshauri wameshashauri sana na aliwahi kusema ukishauri tu umepoteza kama wewe ulivyoshauri hapa umepoteza mazima
Pumzika bhana hasara roho pesa makaratasi
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
2,695
Points
2,000

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2018
2,695 2,000
Haya CCM wanayofanya yalishafanywa na wenzao huko miaka ya nyuma, ila yaliwatokea puani, leo hii wako wapi???

Yuko wapi;
1) Saddam Hussein.
2) Muammar Ghadaffi.
3) Omar Al Bashir.
4) Adolf Hitler.
5) Mao Zedong.
6) Mobutu Sesseseko Kuku Gbendu Wa Zabanga.
7) Patrice Lumumba.
8) Idi Amin Dada.
9) Thomas Sankara.
10) Brigadier David Lansana (Utawala wake ulidumu siku 2 tu).
11) Bokassa.

Na wengine wengi.

CCM wajipange kisaikolojia, watayakuta na wao.
 

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,650
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,650 2,000
Alexander The Great,
Kila chenye mwanzo ni lazima kiwe na mwisho..........

Tunachoamini hapa duniani ni Mungu pekee ambaye ni Alfa na Omega, hana mwanzo wala mwisho............

Binadamu mwingine yeyote kujilinganisha na Mungu ni kufuru kubwa..........

Mwisho wake utakuwa mbaya na wa aibu. Take my words
 

Forum statistics

Threads 1,379,247
Members 525,347
Posts 33,739,758
Top