MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mwandishi na Mhariri wa magazeti, Absalom Kibanda aliwahi kusema Jumapili iliyopita tarehe 2 April katika akaunti yake ya twitter, ‘’Tanzania requires one strong opposition party before they think of ousting the ruling state party - CCM. We aren't there yet’’.
Uchaguzi wa wabunge wa The East African Legislative Assembly (EALA) umeendelea kutoa angalizo hilo na sasa uteuzi wa Prof. Kitila Mkumbo unawavuruga zaidi wapinzani nchini na kuibua sura zao halisi.
Tunaotumia benchmark ya kilichofanywa na UKAWA tarehe 28 Jul 2015 ambapo Edward Lowassa alijiunga Rasmi CHADEMA hatuwezi kushangaa kuona upinzani bado sana nchini.
Niliposoma Gazeti la propaganda la CHADEMA, Tanzania Daima ambalo kichwa cha habari kilisema, JPM awaunganisha CCM, UKAWA bungeni nilicheka sana. Wapinzani wenyewe hawajaungana itakuwaje waungane na CCM.
Toka lini wanasiasa wanaofanya siasa za kinafiki wakaungana na wabunge wengi kutoka chama ambacho kimejengwa katika msingi wa Imani? Ningeelewa kama wangesema wanaungana na baadhi ya wabunge wa CCM kwa sababu kwenye safari ya mamba, kenge hawakosekani.
Wanasiasa wanafiki huja na misemo inayosema, ‘’Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu au rafiki wa kudumu’’ ili waendeleze unafiki wao.
Chuki iliyopo kati ya vyama vya upinzani haiwezi kumalizwa na rhetoric zinazotoka midomoni mwa wanasiasa wanafiki bali zitamalizwa na matendo yao wakati wa majaribu ya kisiasa.
Rais Magufuli amewaminya kidogo tu kati yao kwa sasa wameanza kurushiana maneno wakishutumiana kuhusu usaliti na kununuliwa.
Hii inanikumbusha mwaka 1995 wakati Mwl. Nyerere alipozungumza na vyombo vya habari akikemea udini na ukabila nchini na kusema kuna watu wanajidanganya kuwa ukabila haupo lakini ukiwaminya kidogo tu utakuta ukabila wao uko palepale.
Mwl. Nyerere alienda mbali zaidi na kutolea mfano wa Marehemu George Kahama ambaye alikuwa amemtuma kwenda Zaire kikazi. Wakati wanarudi, ndege ikaanza kuleta matatizo ya kuruka ruka.
Ndege ikaruka mara ya kwanza, George Kahama akasema, ‘My God, My God’, iliporuka zaidi, akasema ‘Mama yangu wee’ na iliporuka zaidi zaidi, akapiga kelele na kusema ’Mawee, Mawee’. Mawee ni neno la kabila la Marehemu George Kahama.
Hoja ya Mwl . Nyerere ilikuwa ni kueleza kuwa wakati wa hali ngumu ukabila hujitokeza pamoja na kwamba tunadhani haupo.
Tumeona kwa wapinzani wakionyesha sura zao halisi za chuki kati yao baada ya kutikishwa kidogo na Rais Magufuli alipomteua Prof. Kitila Mkumbo.
Ninawaza siku ambayo Prof. Mwesiga Baregu atakapoteuliwa na Rais Magufuli. Hii siku ipo mbioni! Just get ready!