Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
Kwa jinsi anavyochukua mamuzi hana tofauti na wakati akiwa kwenye mambo ya ujenzi wa mabarabara kama mnakumbuka alivyofanya katika mambo ya samaki. tuache hayo.
Leo hii inaonekana wazi kuwa hana washauri au haambiliki na kushaurika ,wananchi wengi wanaonekana kuteseka na utawala wake na madai yao wanarudishwa katika umasikini.
Tunaona sheria za kusimamisha wanaosafiri kutoka sehemu moja kuelekea nyingine wakisimamishwa na vyombo vya ulinzi likiwemo JWTZ,kushushwa na kuamriwa kufanya usafi ,hivi hakuna mabaraza ya miji na wanalipwa au hawalipwi ,hujui watu wanaelekea wapi kama hospitali kupelekea chakula wagonjwa au kuwahi basi lingine ,huu ni udhalilishaji na kama haitoshi sehemu zingine za miji unatakiwa ulipe hela si chini ya elufu kumi kama hutaenda au kuonekana katika kufanya usafi ,hivi hii nchi tupo huru ?
Hadi sasa hakuna la maana ambalo kitaifa litaonyesha serikali imefanya jambo kubwa na kuleta maendeleo ,miezi mitatu imeshapita au wataalam wanasema siku mia ,hivi ni kweli shule zimekuwa na elimu bila ya malipo ?
Kubwa ambalo linaonekana kushika kasi ni wananchi kuingia na kujawa na hofu kwani mauaji ya njenje yameshika kasi ya ajabu na sasa inaonekana wazi Tanzania si shwari tena.
Kila kukicha Mheshimiwa Raisi John P.Magufuli amekuwa kama anaeamka na kuzuka na wazo jipya ,akizungumza na kujenga matumaini mapya kwa Wananchi wanaosubiri maendeleo huku miezi ikikatika sasa imebaki kama miezi minne atimize mwaka tokea aingie madarakani na kasi ya kutumbua majipu .
Ubaya sio wake ila chama chake ndicho kilichosheheni uwoza kiasi ya kwamba wanashindwa hata kumkabidhi uenyekiti wa Chama ,haijawahi kutokea raisi kutokea Ccm akaa kwa muda mrefu hajakabidhiwa sukani ya Chama je hili sio jipu.
Kwa jinsi alivyoziteka akili za watz kila unaemsikia anaomba Raisi magufuli aingilie kati kati hapa inaonyesha wazi wananchi wamejenga matumaini kwa Raisi binafsi na sio serikali yake kwa maana CCM ni ileile na hawana jipya la kuwakomboa ,kila kitu Magufuli hivi atapanga na kutekeleza mangapi ,kitu ambacho kinamfanya awe anakurupuka huku na kule bila ya hata uchunguzi wa kina.
Anahamisha huyu anafukuza wale anasimamisha hawa alimuradi ni vurugu mechi wafanyakazi wanafanya kazi kwa hofu na woga kwamba kama hatasimamishwa na mh.mgufuli basi hata mkuu wake wa kazi kwa kujionyesha tu kuwa anaendana na kasi ya Raisi na yeye anaweza kufukuza bila ya uchunguzi wala shutuma ni fukuza na hakuna kuhoji kwa nini .
Kila nikiangalia maafa yameongezeka tokea Magufuli awe Raisi kuanzia ajali za barabarani na hata mauaji ya mapanga na sime au vitu vyenye ncha kali ,Je Mheshimiwa alishinda kihalali hapa sasa tunaangalia baraka za mtu anaeshinda kihalali mbele ya mwenyezi Mungu ,Je mwenyezi Mungu anakuwa pamoja na wenye kudhulumu.
Tanzania hatuhitaji kiongozi anaetumia njia za panya kushinda labda awe hajui kama ushindi ulipatikana kwa mizengwe kwani sote ni waumini na katika wimbo wa Taifa tunasema Mungu Ibariki ,sasa ni Mungu gani huyo tunaemuomba ! Na viongozi hula viapo kwa kumtaja huyu huyo Mungu awasaidie ,Je Mungu huyo anawasaidia wanaoshinda kwa kupitia Lubuva na jecha.
Je mungu huyo yupo na wale wanaotengeneza njia za ushindi zisizo alali ? Inapotokea kiongozi kukaa madarakani kwa njia za panya basi matatizo ndani ya nchi hayatamalizika itakuwa ni kusukumana tu kwani hakuna razi za Mungu hapo !
TAFAKARI.