Rais Magufuli anatuhimiza wananchi tukachape kazi, wakati makampuni yakiendelea kuwapunguza wafanyakazi wao kutokana na ugonjwa wa Corona!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Tulimsikia wenyewe Rais wetu Magufuli wakati akilihutubia Taifa siku chache zilizopita, akituhimiza wananchi tukachape kazi na kuwa tusitishwe na vyombo vya habari vya kibeberu, kwa kuwa ugonjwa wa corona siyo tishio kiasi hicho wanachotuaminisha!

Kwa kweli nilishangazwa sana na maelekezo hayo ya Rais wetu, wakati nchi nyingi, zikiwemo nchi jirani zimechukua hatua ngumu sana, zikiwemo za kuwafungia majumbani, wananchi wao, ili wasitoke

Ninachojiuliza hivi Rais anawezaje kutuhimiza wananchi tukachape kazi, wakati yeye mwenyewe anajua kuwa kazi hizo hazipo, kutokana na wananchi hao kupoteza kazi zao kutokana na ugonjwa huo wa corona?

Hivi Rais hajui kuwa shughuli nyingi za kibiashara zimeathirika sana kutokana na ugonjwa huo?

Hivi Rais hajui kuwa Hoteli nyingi zimefunga biashara na kuwaambia wafanyakazi wao waende majumbani kwao kwenda kupumzika kwa lazima?

Hivi Rais wetu hajui kuwa mashirika mengi ya ndege "yanapumulia mashine" kutokana na mashirika hayo kusitisha huduma zao za usafiri, kwa ajili ya wageni wengi kutoweza kusafiri kutokana na ugonjwa huo wa corona?

Sasa atawahimazaje wafanyakazi hao wakachape kazi, wakati waajiri wao wamewapumzisha kutokana na janga hilo la corona?

Serikali nyingi za nje zishaanza kuwafidia wananchi wao kutokana na madhara makubwa sana waliyoyapata kutokana na jinamizi hili la corona nchini mwao, ikiwemo nchi jirani ya Kenya.

Ningependa nimuulize huyu anayejiita Rais wa wanyonge, je ni lini atawafidia wananchi wake wanyonge, kutokana na madhara makubwa waliyoyapata kutokana na janga hili la corona?

Ni makosa makubwa kwa serikali yetu kuendelea na "business as usual" katika kipindi hiki kigumu sana cha ugonjwa huu wa corona

Maswali yako mengi, lakini itoshe tu kusema, kwa hayo màswali machache niliyoyauliza hivi leo
 
Shuguli za uchumi nyingi zimesimama au zinakwenda taratibu. Corona haina chama.
Nachoshangaa watu wanafosi serikali iwaambie wakae ndani, kama hautaki kufanya kazi jifungie tu na familia yako sio lazima serikali ikuambie
 
Tuombe sana hili gonjwa lisisambae sana maana self isolation itakuja kwa lazima
Tahadhari na kufuata masharti ni muhimu sana
Zingatieni ushauri tu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mystery,
Mkuu,
Hapo juu umeeleza ugumu wa kuchukua hatua"...nchi nyingi zimechukua hatua ngumu..." na ukumbuke kuwa hata hatua ambazo hizo nchi ulizozitaja za kuwalipa fidia wananchi pia ni ngumu! Kwani nifedha za walipa kodi, hao hao wanyonge unaodai kuwatetea, ni hatua ngumu...ina ukweli...kuchukua!
Lakini kuchonganisha Raisi au Serikali yako na wananchi sio mbadala wa kupambana na kirusi hicho.

Mkuu, Kuwaomba wananchi...Kuchapa kazi kwa tahadhari, na kupunguza jazba zinazotokana, ni haki ya kiongozi yeyote anayejali wananchi!

...kazi kweli kweli.
mchana mwema
 
Kwaiyo kama ni hatari, tusifanye kazi na shughuli za kiuchumi visimame?

Kwa taarifa yako juzi nilikuwa Arusha eneo la mto wa mbu, niliona wafanyabishara waliokuwa mnadani wakipigwa na jeshi la polisi kwa maelezo kuwa mikusanyiko hairuhusiwi. Hivyo hiyo hadithi ya kuwa rais amesema watu wachape kazi ni hadithi ya jukwaani, lakini utekelezaji sehemu kubwa ya nchi ni tofauti.
 
Kwa taarifa yako juzi nilikuwa Arusha eneo la mto wa mbu, niliona wafanyabishara waliokuwa mnadani wakipigwa na jeshi la polisi kwa maelezo kuwa mikusanyiko hairuhusiwi. Hivyo hiyo hadithi ya kuwa rais amesema watu wachape kazi ni hadithi ya jukwaani, lakini utekelezaji sehemu kubwa ya nchi ni tofauti.
Ok sawa

Labda ni utekelezaji wa BY LAW waliojiwekea ila si tamko la Tanzania nzima.

Ila tukilazimishwa kujifungia tutakuja kuhoji na kukosoa maana wanadamu hatuna jema
 
Ok sawa

Labda ni utekelezaji wa BY LAW waliojiwekea ila si tamko la Tanzania nzima.

Ila tukilazimishwa kujifungia tutakuja kuhoji na kukosoa maana wanadamu hatuna jema

By Law ambayo inawanyima watu kufanya kazi? Kwa hiyo kama ni by Law ina nguvu kuliko maagizo ya rais?
 
By Law ambayo inawanyima watu kufanya kazi? Kwa hiyo kama ni by Law ina nguvu kuliko maagizo ya rais?
Wanakazia by Law, sio kila sehemu ya nchi kuna uwepo wa rais au unavyojua rais ni kama GHOST mkuu?

Kama umeona toa reports sehemu uhusika mkuu.
 
Wanakazia by Law, sio kila sehemu ya nchi kuna uwepo wa rais au unavyojua rais ni kama GHOST mkuu?

Kama umeona toa reports sehemu uhusika mkuu.

Sehemu husika ni polisi, na polisi ndio wameendesha hilo zoezi la kuwapiga hao wananchi. Kibaya zaidi sasa hivi hakuna uhuru wa habari, hivyo hakuna muandishi wa habari anaweza kuripoti huo unyama kwa kuhofia usalama wake.

Ndio yale yale tuliyokua tunasema, kuondolewa kwa uhuru wa habari, lengo lake kubwa lilikuwa ni kutia watu na woga, na kutoa mwanya wa watu kufanyiwa ukatili na vyombo vya kimamlaka wakishirikiana na watawala.
 
Sehemu husika ni polisi, na polisi ndio wameendesha hilo zoezi la kuwapiga hao wananchi. Kibaya zaidi sasa hivi hakuna uhuru wa habari, hivyo hakuna muandishi wa habari anaweza kuripoti huo unyama kwa kuhofia usalama wake. Ndio yale yale tuliyokua tunasema, kuondolewa kwa uhuru wa habari, lengo lake kubwa lilikuwa ni kutia watu na woga, na kutoa mwanya wa watu kufanyiwa ukatili na vyombo vya kimamlaka wakishirikiana na watawala.
Hahahahahaha

Eti sasa hivi hamna uhuru wa habari? Tupu humu tunaongea tunavyotaka na wengine wanadiriki kutukana viongozi au uhuru wa habari gani?
 
Hahahahahaha

Eti sasa hivi hamna uhuru wa habari? Tupu humu tunaongea tunavyotaka na wengine wanadiriki kutukana viongozi au uhuru wa habari gani?

Huku ni uchochoroni ndio maana 95% huku ndani wanatumia fake ID. Huenda hujui maana ya vyombo vya habari. Nazungumzia vyombo rasmi vya habari pls.
 
Back
Top Bottom