AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Ukiacha miradi mkubwa ya kimkakati inayotekelezwa sasa hivi hapa nchini kwa kasi Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mh. Dr. John Pombe Magufuli amefanikiwa kujenga vituo vya afya 360 na Hospitali mpya za Wilaya katika Halmashauri 67 nchi nzima.Hii ni hatua kubwa sana ya maendeleo yanayogusa maisha ya watanzania makabwela wanyonge lakini pia ni kete muhimu kuelekea katika uchumi wa kati kwa sababu hatuwezi kufika huko kama afya za Watanzania ambao ndio wazalishaji zitakua kwenye hati hati.
Sasa mwaka 2020 ukiwa ni mwaka wa uchaguzi mkuu amabapo bila shaka, panapo neema za MUNGU Chama Cha Mapinduzi kama ilivyo ilivyo mila na desturi zake kitamchagua tena Mh. Dr. John Pombe kama mgombea wake kwa muhula wa pili mfululizo. Sote ni mashuhuda wa jinsi nchi ya uongozi wake alivyoweza kuiboresha na kuifanyia mabadiliko makubwa sekta ya afya kwa kujenga vituo vua afya,na Hospitali za Wilaya 67 nchi nzima ukiachilia mbali dawa na vifaa tiba .
Maendeleo hayo kwenye sekta ya afya yamewagusa moja kwa moja Watanzania zaidi ya million 50 ambao sasa wanafaidika na uongozi bora wa Rais Magufuli.Katika watanzania hao wapo waliofikisha umri wa kupiga kura mwakani ni wazi kwamba kutokana ukweli huo kura zao hawatakua na sehemu nyingine ya kuzipeleka zaidi ya kupiga alama ya tiki kwenye picha ya Mh Magufuli akiwa kama mgombea wa CCM ambae amekua ni mkombozi wa afya zao.
Rais Magufuli anazo sababu nyingi za kuchaguliwa kwa awamu nyingine, afya ikiwa ni sababu mojawapo, hakuna Mtanzania ambae tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani hajafaidika na huduma za afya zilizoboreshwa.Watakaojitekeza kuchuana nae watambue kwamba hawataweza kufurukuta hata kidogo kwa sababu Rais Magufuli anajiuza mwenyewe kwa maendeleo makubwa aliyofanya kwenye sekta ya Afya.
Rais Magufuli anatosha sana, watu wanashangaa amewezaje kufanya mambo makubwa ya kutukuka ndani ya muda mfupi, hiki ni kipaji kikubwa cha uongozi kilichomo ndani yake alichobarikiwa na Mwenyezi MUNGU.Anaacha alama na somo kubwa la uongozi kwa namna alivyojitoa sadaka kwa ajili ya Tanzania iliyokua inachezewa kwenye matumizi ya fedha za umma badala ya kwenda miradi kama hii yenye tija ilikwenda kwenye mifuko ya watu fulani fulani.
Wanaotaka kuchuana nae 2020 ni vema wakayapima maji haya marefu kwa miguu kabla ya kuamua kujitosa. Rais Magufuli ana mamilioni ya Watanzania nyuma yake wenye vyama na wasio na vyama wanaomuunga mkono. Rais huyu Watanzania wamepewa kama zawadi na bado wanamuhitaji kwa ajili ya kushughulika na kero zao.Uhakika wa kupata ushindi wa kishindo kwake uko palepale kwa sababu maendeleo aliyoyaleta yanaoeneka wazi.
Augustino Chiwinga
0659438889 / 0756810804