Rais Magufuli anatamani Tanzania ya neema kama libya ya hayati Gadafi

..viongozi wetu should know better.

..Gaddafi alimuunga mkono Iddi Amin Dada aliyevamia nchi yetu, kuua raia, na kuharibu mali.

..askari wetu walipoteza maisha wakipambana na majeshi ya Iddi Amini na swahiba wake Muamar Gaddafi.

..nakumbuka wako mateka askari wa Gaddafi ambao waliletwa Tanzania toka uwanja wa mapambano.

..Watanzania tulimsamehe Gaddafi na kuamua kuwarudisha Libya askari wake waliotekwa.

..Kinachonishangaza mimi ni viongozi wetu kusahau au kujisahaulisha uovu aliotufanyia Muamar Gaddafi ktk vita vya Uganda.

..Mtanzania anayemtukuza, na kumlilia Gaddafi, kwa maoni yangu, anadhihaki mchango wa mashujaa wetu waliopigana vita vya Kagera na Uganda.

cc The Boss, Nguruvi3
 
Mwenzake wa libya,neema ya libya ilikuwa ni matibabu bure kwa raia,elimu bure kwa raia,umeme bure kwa raia,lakini mtamani neema ya Tanzania amefikia hatua ya kuwatoza VAT raia hadi voucha wanazotumia kwenye simu.
 
Dah! Mkuu nimeuliza maswali wala sikutoa mawazo yangu. Sasa sijui umejuaje uwezo wangu ni mdogo wakati nataka kujua tu! Au yeyote aulizae swali anauwezo mdogo wa kufikiri? Ukitoa sentesi yako ya kwanza mengine nimekuelewa na asante kwa hilo
 
Dua ya leo inaendelea kuwa mahala pabaya pa kuishi mwanaadamu kutokana na wingi wa watu wenye mawazo kama yako, mawazo ambayo ni static, yanaangalia upande mmoja, yeyote anaewaza kinyume nawe ana uwezo mdogo wa kufikiri. One man leadership with full of free social services and well advanced living standards ni sawa na utawala wa kubadilishana kila kukicha huku raia wakifa kwa njaa, kodi za ajabu ajabu.......think twice, acha chuki binafsi.
Unajua kile ulichoambiwa tu, husumbui kichwa chako kutafuta yaliyojificha. Zile nyumba za makuti na madebe kule Benghazi wale sio Walibya wale?

Waambiwaji msiosumbua vichwa, mmeambiwa kuwa Gaddafi aliwasomesha bure wananchi wake hadi Univesity, na bado wananchi hao hao ambao pia wanapewa benefits kibao bado ni wajinga kiasi cha kudanganywa na KAFIRI wamuondoe mtukufu Gaddafi kwa namna ile?

Amsha kichwa chako wewe!
 
Back
Top Bottom