Rais Magufuli anatakiwa kutengua uteuzi wa Waziri Mpango na Waziri Kabudi kwa kuwateua kabla Waziri Mkuu hajapatikana

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Rais Magufuli anatakiwa kutengua uteuzi wa Waziri Mpango na Waziri Kabudi kwa kuwateua kabla Waziri Mkuu hajapatikana, nakuteua wengine ili asifunguliwe kesi baada ya kustaafu.

Don Nalimison: Kutengua Uteuzi huo kutamjengea heshima Rais kwa kuiheshimu Katiba ya Nchi. Maana Katiba inamtaka Rais ashauriane na Waziri Mkuu juu ya Uteuzi wa mawaziri lakini Waziri Mkuu alikuwa bado hajapatikana pindi wanateuliwa na hivyo Rais ameikosea Nchi na Wananchi kwa kuvunja Katiba ya Nchi iliyotungwa na Wananchi. Ni heri uvunje Sheria maana zinatungwa na kundi dogo la wabunge lakini Katiba ni kundi kubwa la Wananchi.

RAIS akitengua Uteuzi huo na kuteua wengine kwa kushauriana na Waziri Mkuu kwa Sasa atakuwa ameheshimisha Katiba na Nchi.Na baada ya Miezi sita ANAWEZA kuwarudisha Tena kwa mjibu wa Sheria au atengue Uteuzi huo na kuwaapisha upya kwa kushauriana na Waziri Mkuu. Na hivyo ndivyo Sheria inavyotaka. Katiba lazima iheshimiwe Kama Rais atakaidi italazimu kufungua mashitaka na atakapo staafu akamatwe Mara moja.

DON NALIMISON
Kahama-Shinyanga.
 
ICC sio ‘dampo’ la kila kitu wala hawawezi kupokea kesi ya kipuuzi kama hii

Yaani upuuzi unaofanywa na Mwafrika haiwezekani kuwategemea mabeberu kuutatua. Hii ‘kesi’ inapaswa kufunguliwa ndani ya nchi
 
Wewe mwalimu wa huko Misungwi usikurupuke ovyo,

Hilo wazo na ushauri wako ulitakiwa uelekeze kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali sio Mh Rais maana yeye anauliza na anashauriwa na yeye ndio maana alikuwa mtu wa kwanza kuteuliwa.

Hilo suala la kumkamata baada ya muda wake kuisha kwa madai uliyotoa na kushitakiwa kwa kuvunja katiba, hebu soma vizuri mabadiliko ya Sheria. Mamlaka ya Waziri mkuu kwa sasa ni kiduchu na yana nakisi ndogo sana kwa Rais. Waziri mkuu ambaye alikuwa na utisho wa kiuongozi, kiutawala na kisiasa alikuwa Edward Moringe Sokoine pekee wengine wote wanatenda kwa utashi wa Rais kulingana na sera zinazohitajika kutekelezwa.

Waziri mkuu ni Mbunge jimbo lake la Uchaguzi ni Ruangwa kwa sasa na Mh Rais ni kiongozi wa nchi jimbo lake la Uchaguzi ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bara & Zanzibar). Kwa mantiki hiyo Waziri Mkuu ushauri wake ulikasimishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kulingana na dharura.

Wewe ni mwalimu unatakiwa kujiongeza kama msomi badala la kutoa tafsiri za kisiasa zilizoathiriwa kisaikolojia kutokana na matendo uliyotenda na hatua ulizochukuliwa ndipo unaonesha hasira zako kwenye jukwa la utambulisho mficho.
 
Nilitamani ungekuwa mgombea mwenza wa Lissu maana wote dishi zenu zimeyumba
 
Bahati nzuri Rais Dk. John Pombe Magufuli ninayemjua Mimi huwa hana muda 'Mchafu' wa Kusikiliza 'Ushauri' wa 'Kipuuzi' kutoka kwa 'Mpuuzi' pia.
Kwa nini usipokubali hoja ya mtu lazima umtukane, kashifu au kumfanya punguwani? Nauliza tu. Hebu thubutu kujibu. Moja ya matatizo makubwa ya internet ni kwamba imempa kila mtu uwezo wa kujiona ana akili kupindukia ! Ni wale tu ambao kweli wanazo ndiyo wanaozitumia kwa staha!
 
Jf ..where people dare to talk...hata kama unaongea pumba unaachwa tu uonyeshe ujinga wako.
 
ICC sio ‘dampo’ la kila kitu wala hawawezi kupokea kesi ya kipuuzi kama hii

Yaani upuuzi unaofanywa na Mwafrika haiwezekani kuwategemea mabeberu kuutatua. Hii ‘kesi’ inapaswa kufunguliwa ndani ya nchi
Mbona wamethihurisha kuipokea kesi juu ya mamlaka ya Tanzania!
 
ICC sio ‘dampo’ la kila kitu wala hawawezi kupokea kesi ya kipuuzi kama hii

Yaani upuuzi unaofanywa na Mwafrika haiwezekani kuwategemea mabeberu kuutatua. Hii ‘kesi’ inapaswa kufunguliwa ndani ya nchi
Kwani Don kasema Rais atashitakiwa ICC kwa kukiuka Katiba? au aliandika akafuta?
 
Watanzania tunataka maendeleo sio porojo, Watanzania tunataka njia sahihi za kututoa tulipo kama Taifa na sio mijadala mfu ya mlioshindwa na kupigwa chini na Wananchi.
Watanzania wanataka Elimu, Miundombinu, Madawa, Umeme, na Maji kupatikana katika makazi yetu.
 
Ngoja tushughulike na haya mauaji yaliyotokea Zanzibar kipindi cha Uchaguzi, pia na huku bara uminywaji wa democracy na violation of human rights..

Hayo mengine watajijua wao na 'Mahakama' uchwara zao!
 
Wamala?
Nenda kasome Katiba ibara ya 51 (3)( d)
55.
(1) All Ministers who are members of Cabinet by virtue of Article 54 of Ministers shall be appointed by the President after consultation with the Prime Minister and and Deputy they shall be responsible for such offices as the President may, from time to time,

(2) In addition to the Ministers referred to in subarticle (1) the President may, after consultation with the Prime Minister, appoint Deputy Ministers. All Deputy Ministers shall not be members of Cabinet.

(3) The President may appoint any number of Deputy Ministers who shall assist Ministers in the discharge of their duties and functions.
(4) All Ministers and Deputy Ministers shall be appointed from among Members of Parliament.

(5) Notwithstanding the provision of subarticle (4), in the event that the President is obliged to appoint a Minister or a Deputy Minister after dissolution of Parliament then he may appoint any person who was a Member of Parliament before Parliament was dissolved.
 
Wewe mwalimu wa huko Misungwi usikurupuke ovyo,

Hilo wazo na ushauri wako uliktakiwa uelekeze kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali sio Mh Rais maana yeye anauliza na anshauriwa na yeye ndio maana alikuwa mtu wa kwanza kuteuliwa.

Hilo suala la kumkamata baada ya muda wake kuisha kwa madai uliyotoa na kushitakiwa kwa kuvunja katiba, hebu soma vizuri mabadiliko ya sheria. Mamlaka ya Waziri mkuu kwa sasa ni kiduchu na yana nakisi ndogo sana kwa Rais. Waziri mkuu ambaye alikuwa na utisho wa kiuongozi, kiutawala na kisiasa alikuwa Edward Moringe Sokoine pekee wengine wote wanatenda kwa utashi wa Rais kulingana na sera zinazohitajika kutekelezwa.

Waziri mkuu ni mbunge jimbo lake la uchaguzi ni Ruangwa kwa sasa na Mh Rais ni kiongozi wa nchi jimbo lake la uchaguzi ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bara & Zanziba). Kwa mantiki hiyo waziri mkuu ushauri wake ulikasimishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kulingana na dharura.

Wewe ni mwalimu unatakiwa kujiongeza kama msomi badala la kutoa tafsiri za kisiasa zilizoathiriwa kisaikolojia kutokana na matendo uliyotenda na hatua ulizochukuliwa ndipo unaonesha hasira zako kwenye jukwa la utambulisho mficho.
Umeongea mengi lakini hujajibu hoja za mtoa thread. Umeongea kishabiki wakati yeye kaongea kisheria
 
Back
Top Bottom