domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,545
- 1,719
Rais Magufuli amepiga marufuku majeshi kuuza maeneo yao au kuingia ubia na watu binafsi kufanya biashara. Rais Magufuli amechelewa kutoa amri hiyo kwani eneo la jeshi maeneo ya maji chumvi limeuzwa kwa muwekezaji na ujenzi wa kituo cha mafuta (Filling Station) Unaendelea kwa kasi.
Licha ya eneo hilo kuwa mali ya jeshi, lakini kituo hicho cha mafuta kimejengwa katikati ya kilima teremko mkali wenye kona kali mita kumi kutoka daraja la maji chumvi, daraja liunganishalo Wilaya ya Ilala kwa maana ya Tabata na wilaya ya Ubungo kwa maana ya Ubungo jeshini.
Hiki ni kipimo kingine cha usimamiaji wa maamuzi ya rais wetu. Je, ataweza kubatilisha biashara iliyofanyika kinyume na amri yake aliyoitoa leo? Ataacha biashara ile iendelee kwa vile amri yake imekuja baada ya biashara kufanyika?