Rais Magufuli anashtuka wakati kiwanja cha jeshi 'maji chumvi' kimeshauzwa!

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,545
1,719
Rais Magufuli amepiga marufuku majeshi kuuza maeneo yao au kuingia ubia na watu binafsi kufanya biashara. Rais Magufuli amechelewa kutoa amri hiyo kwani eneo la jeshi maeneo ya maji chumvi limeuzwa kwa muwekezaji na ujenzi wa kituo cha mafuta (Filling Station) Unaendelea kwa kasi.

Licha ya eneo hilo kuwa mali ya jeshi, lakini kituo hicho cha mafuta kimejengwa katikati ya kilima teremko mkali wenye kona kali mita kumi kutoka daraja la maji chumvi, daraja liunganishalo Wilaya ya Ilala kwa maana ya Tabata na wilaya ya Ubungo kwa maana ya Ubungo jeshini.

Hiki ni kipimo kingine cha usimamiaji wa maamuzi ya rais wetu. Je, ataweza kubatilisha biashara iliyofanyika kinyume na amri yake aliyoitoa leo? Ataacha biashara ile iendelee kwa vile amri yake imekuja baada ya biashara kufanyika?
 
Kwani kiliuzwa lini? Labda ndio maana aliamuwa kuyasema hayo kutokana na mauzo hayo, (nafikiri tuu sina uhakika).
 
HAYA NI MAJUNGU! Mbona hukusema mapema kabla Rais hajatoa maelezo yake.
 
Twende Vema Wewe Umesema Mpakani
Tueleze Jeshi Gani Lipo Hapo?

Anayesema Mgulani Naye Ataje Rais Akija Aone Na Ukweli Ujulikane Bayana
 
Maeneo mengi ya JWTZ yamekuwa yakimegwa na wananchi hata Ramani ya Lugalo ikichunguzwa kwa umakini inaweza kutokea bomoabomoa ambayo haijawahi kutokea Tanzania hii kwa sababu asilimia 40% ya maeneo ya jeshi yalivamiwa na wananchi.
 
Kila tasisi Nchi wana madhambi yao akisema atembelee kila jeshi atakutana na vioja vya kila Aina.
 
Twende Vema Wewe Umesema Mpakani
Tueleze Jeshi Gani Lipo Hapo?

Anayesema Mgulani Naye Ataje Rais Akija Aone Na Ukweli Ujulikane Bayana
Maeneo mengi ya wazi na viwanja vingi vya serikali vilichukuliwa kinyemela na Wajanja wachache kitambo.
 
Pale gongo la mboto njia panda ya kuelekea Kampala university nina wasiwasi na ile petrol station inayojengwa
 
Sasa ni wakati wa majeshi 'kung'atuka' mjini na kwenda kujichimbia msituni... Hayo maeneo wanayo 'yaatamia' mjini hasa lile eneo la kambi ya Lugalo yagawiwe kwa wawekezaji waendeleze jiji... Siku hizi vita vinapiganwa kiteknolojia. Huhitaji kuwa na makambi mengi ili kushinda vita...
 
Kambi zinawekwa kistatejia mkuu na kwenye makambi ya jeshi kuna mikondo miwili ambayo saporting na technical. ambaxo zinakua inasaidiwa na backup system kwa kik
La mkondo ambapo lazima izungukwe na mikondo mbadala.
Vita ni teknojia ila ufahamu vita ni zaidi ya teknolojia vita ni timing na takitiki
 
Kambi za jeshi zipo mahali hisika sio by chance but stratergically...
 
Maeneo mengi ya JWTZ yamekuwa yakimegwa na wananchi hata Ramani ya Lugalo ikichunguzwa kwa umakini inaweza kutokea bomoabomoa ambayo haijawahi kutokea Tanzania hii kwa sababu asilimia 40% ya maeneo ya jeshi yalivamiwa na wananchi.
Mengi yanavamiwa na wastaafu!!
 
Twende Vema Wewe Umesema Mpakani
Tueleze Jeshi Gani Lipo Hapo?

Anayesema Mgulani Naye Ataje Rais Akija Aone Na Ukweli Ujulikane Bayana
Mkuu hapo maji chumvi napafahamu ni kweli kuna filling station inajengwa kwa kasi ya unyoya!! Ni maeneo ya Ubungo Kibangu mpakani na mabibo
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Pale gongo la mboto njia panda ya kuelekea Kampala university nina wasiwasi na ile petrol station inayojengwa
Huku ndipo eneo la jeshi limekwatwa vipande vingi sana hakuna kambi ya JWTZ iliyopo Dsm ambayo eneo lake halijakegwa kwa njia haramu.
 
Ukiangalia historia basi utakutana na maafande/wakubwa wa jeshini ndio wavamizi au ndio waliokula njama kuuza ardhi ya jeshi, kama Juma anaweza mwombeni afukue makaburi hayo
 
Kambi zinawekwa kistatejia mkuu na kwenye makambi ya jeshi kuna mikondo miwili ambayo saporting na technical. ambaxo zinakua inasaidiwa na backup system kwa kik
La mkondo ambapo lazima izungukwe na mikondo mbadala.
Vita ni teknojia ila ufahamu vita ni zaidi ya teknolojia vita ni timing na takitiki
Kaka ingependeza kama ungetumia Kiswahili fasaha na uihakiki habari yako kabla ya kuituma,
 
Back
Top Bottom