Rais Magufuli anasalitiwa, Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Maisha halisi ya Wanatabora

Mkuu nadhani hii nyumba ni ya kawaida sana kwa cheo cha DC. Ni kweli kuna matatizo lakini pia tukumbuke uongozi una hadhi na uwajibikaji
 
Heshima kwenu wakuu,

Najaribu kuwaza watanzania tunaanza na nini kama kipaumbele chetu? Nahisi kama Viongozi wanatusaliti na kutupaka mafuta kwa Mgongo wa Chupa. Kwenye TV naona wakiongea kwa hasira huku wamekunja sura lakini ukiangalia matendo yao tofauti.

Kwa matatizo ya Tabora au hata tuseme Ulambo amabayo hamna Vymba vya Madarasa, Zahanati, Maji, Barabara hazipitiki, Madawa, Madawati Nk, ndo watu wa kumjengea Mkuu wa Wilaya Nyumba kama hii? Kwa hali hii sitegemei mtu aishi kama mashetani wakati Wakubwa hawaoneshi Mfano.

Walipoapishwa nlisikia Wanaenda kuwatumikia Wananchi tena kuna kauli walisema eti Ukiona umekaa kwenye A/C halafu Shule zako watoto wanakaa chini Jitumbue kabla sijakutumbua.

Nikasikia Hakutakuwa na Matumizi ya Magari ya Garama, hapa ni kazi tu kuwatumikia wananchi...Haahaaaa...!!
View attachment 416106
Muonekano wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora, ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi.

Wakati huo huo ndani ya tabora hiyo hiyo, Kuna wazee wameitumikia Tabora Kila kukicha hawajui kesho watakula nini. Mimi kwa mawazo yangu nlikuwa najua kwamba Walala hoi au Masikini wa nchi hii ni hawa Wazee.
View attachment 416134 View attachment 416135
Sehemu ya Nyumba kwa ajili ya Makazi ya Wazee ambazo hazitumiki kutokana na kuwa katika hali mbaya katika Makazi ya kulea Wazee ya Kolandoto Mkoani Shinyanga.
 
Chadema wangeenda kuwasaidia hao wananchi ili tuone mfano .
Hii tabia ya kulialia kwenye mitandao wakati huko rombo madiwani wa Chadema wanajigawia mashamba ya wananchi siyo sahihi na haitasaidia chochote.
 
1. Hiyo ni nyumba stahiki kwa hadhi ya Mkuu wa Wilaya. Wakati ule Ikulu inajengwa, ikulu ndilo likikokuwa jengo zuri kuliko jengo jingine lolote. Hivyo nyumba ya rais wa Urambo pia inastahili kuwa ndio nyumba nzuri kuliko nyumba zote Urambo nzima.

2. Sii kazi ya serikali kuwajengea nyumba raia wake. Kazi ya serikali ni kujenga miundombinu ya umma na kuweka mazingira wezeshi wananchi kujiletea maendeleo ikiwemo kujenga nyumba bora.

3.Wazee wasijiweza wana makao yao hivyo hao wazee kama hawajiwezi na hawana jamii hifadhi ya maisha yao, wakikabidhi ustawi wa jamii, watahifadhiwa, kula bure, na kulala bure.

Pasco
Hivyo vituo vya wazee ni janga lingine.
Wtu wnapiga cha juu wazee wanataabika
 
Karume alijenga nyumba nyingi lakini yeye alikuwa anaishi kwenye hii nyumba;
Zanzibar_State_House.jpg
Na sasa huyu wenzie wanasukumana na nyoka yeye jumba lote hilo...hivi si walisema wote tunatakiwa tuwe levo za mashetani?!?!?
Huwa wakipigiwa makofi wakitoka wapo wanatuzomea
 
Mleta hoja kwa hiyo ulitaka DC Ajengewe nyumba ya tembe ili afanane na wazee na mazingira yanayomzunguka au nini kusudio lako,kwenye kutatua kero za maeneo husika hakumaanishi kiongozi wa eneo husika asiishi kwenye mazingira bora mkuu.
 
Sisi huwa tunawajali masikini kwa maneno tu lakini hatuwapendi na hatuna mpango nao kabisa.
 
Huko Urambo ndio anatoka yule Spika wa awamu iliyopita mzee wa Standard and Speed?

Acha waisome namba ,CCM ni ile ile.
 
Inakuuma Sana Urambo kupata jengo zuri!!
Likitokea kwingineko hamsemi
Huu ni wivu,
Pongezi kwenu wana urambo

Mmejitahidi walau mbadilishe mandhari ya mji wenu
Broq q, Na majengo ya kaliua
 
Miradi ya JK, wacha imaliziwe. Si vibaya mkuu wa wilaya kuishi pazuri. Ipo siku na wewe utakuwa dc
 
Back
Top Bottom