Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ukiiga mfano Wa mijengo ya Chato kuna tatizo?Hiyo ni nyumba ya kuishi ama ofisi?
Kwani tetemeko limeletwa na Serikali?Huyo unayesema anasalitiwa angalia maisha wanayoishi wanawake na watoto Kule Kagera baada ya tetemeko wakati huu mvua zikiwa zimeanza na kauli zake kisha jitafakari.
Ni walewale tuu
Heshima kwenu wakuu,
Najaribu kuwaza watanzania tunaanza na nini kama kipaumbele chetu? Nahisi kama Viongozi wanatusaliti na kutupaka mafuta kwa Mgongo wa Chupa. Kwenye TV naona wakiongea kwa hasira huku wamekunja sura lakini ukiangalia matendo yao tofauti.
Kwa matatizo ya Tabora au hata tuseme Ulambo amabayo hamna Vymba vya Madarasa, Zahanati, Maji, Barabara hazipitiki, Madawa, Madawati Nk, ndo watu wa kumjengea Mkuu wa Wilaya Nyumba kama hii? Kwa hali hii sitegemei mtu aishi kama mashetani wakati Wakubwa hawaoneshi Mfano.
Walipoapishwa nlisikia Wanaenda kuwatumikia Wananchi tena kuna kauli walisema eti Ukiona umekaa kwenye A/C halafu Shule zako watoto wanakaa chini Jitumbue kabla sijakutumbua.
Nikasikia Hakutakuwa na Matumizi ya Magari ya Garama, hapa ni kazi tu kuwatumikia wananchi...Haahaaaa...!!
View attachment 416106
Muonekano wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora, ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi.
Wakati huo huo ndani ya tabora hiyo hiyo, Kuna wazee wameitumikia Tabora Kila kukicha hawajui kesho watakula nini. Mimi kwa mawazo yangu nlikuwa najua kwamba Walala hoi au Masikini wa nchi hii ni hawa Wazee.
View attachment 416134
Sehemu ya Nyumba kwa ajili ya Makazi ya Wazee ambazo hazitumiki kutokana na kuwa katika hali mbaya katika Makazi ya kulea Wazee ya Kolandoto
View attachment 416135
Hapa ndipo wanapoishi hawa wazee
Mkuu Pasco, kumbe unaweza. Umeandika kishwahili bila kuchanganya hata neno moja la kiingereza! Nimeipenda sana.1. Hiyo ni nyumba stahiki kwa hadhi ya Mkuu wa Wilaya. Wakati ule Ikulu inajengwa, ikulu ndilo likikokuwa jengo zuri kuliko jengo jingine lolote. Hivyo nyumba ya rais wa Urambo pia inastahili kuwa ndio nyumba nzuri kuliko nyumba zote Urambo nzima.
2. Sii kazi ya serikali kuwajengea nyumba raia wake. Kazi ya serikali ni kujenga miundombinu ya umma na kuweka mazingira wezeshi wananchi kujiletea maendeleo ikiwemo kujenga nyumba bora.
3.Wazee wasijiweza wana makao yao hivyo hao wazee kama hawajiwezi na hawana jamii hifadhi ya maisha yao, wakikabidhi ustawi wa jamii, watahifadhiwa, kula bure, na kulala bure.
Pasco
Aliyekuletea hiyo picha muombe ukupigie picha ofisi ya Mbunge wa Urambo. Pia Akupigie picha ya nyumba ya Mkurugenzi wa Urambo.
Akupigie picha na nyumba ya Samweli Sitta hapo Urambo, nasisitiza kama hali ya uchumi wa Urambo inaruhusu, jengo mijengo ya hadhi ya viongozi wa Kitaifa wa Urambo na mahali pengine popote.
Pasco
Mkuu Zinj, nimesema na narudia tena kusema kuwa hiyo nyumba ni ya kawaida sana. Mkuu wa Wilaya ndio rais wa wilaya husika, nyumbani kwake kunatakiwa kuwe ndio ikulu ya mahali hapo.Mkuu:
Tuende kwenye uhalisia na sio nadharia ya kusadikika, (Kama hali ya uchumi wa Urambo inaruhusu) Lakini ofisi ya Mh. Mbunge ni ya kawaida kabisa kwa watu wanao fahamu maana ya ujenzi wa nyumba, aidha sina hakika na kuifahamu nyumba ya mzee Sitta.
nyumba mliziuza sasa hiv munatetea huu utoto wa kujenga nyumba zingine.....nafkir kwa sababu zile mlizotupa hata chumba kimoja hastahili kujengewa cz bdae mtakuja kuuziana kwa bei chee1. Hiyo ni nyumba stahiki kwa hadhi ya Mkuu wa Wilaya. Wakati ule Ikulu inajengwa, ikulu ndilo likikokuwa jengo zuri kuliko jengo jingine lolote. Hivyo nyumba ya rais wa Urambo pia inastahili kuwa ndio nyumba nzuri kuliko nyumba zote Urambo nzima.
2. Sii kazi ya serikali kuwajengea nyumba raia wake. Kazi ya serikali ni kujenga miundombinu ya umma na kuweka mazingira wezeshi wananchi kujiletea maendeleo ikiwemo kujenga nyumba bora.
3.Wazee wasijiweza wana makao yao hivyo hao wazee kama hawajiwezi na hawana jamii hifadhi ya maisha yao, wakikabidhi ustawi wa jamii, watahifadhiwa, kula bure, na kulala bure.
Pasco
watupe sababu kwann waliuza nyumba za serikali na leo wajenge tenaKujengewa nyumba nzuri, hakika sio tatizo sana, kwa maana ni nyumba ya umma, sio ya mtu binafsi na umma unatakiwa kujenga vitu vizuri. Na wala hakuna sababu ya kujenga nyumba mbovu eti kwa kuwatetea masikini. Ila tunachotakiwa kusema, na kupiga kelele kweli kweli ni pale mkuu wa wilaya atakapokuwa kwenye nyumba nzuri na akafanya mambo ya hovyo, akaiba, akakandamiza watu watu kwa sababu sio wa chama chake, akapokea rushwa kutokea humo. Hapo ndipo lilipo tatizo, kwani nyumba ya mkuu wa wilaya ya Urambo ina tofauti gani na nyumba za wakuu wengine wa wilaya?