Rais Magufuli anaposita kupelekewa list ya majina ya waliohukumiwa kifo kwa mujibu wa sheria ina maanisha nini?

"Naomba orodha ya watu waliohukumiwa kunyongwa msiniletee kwa sababu najua ugumu wake."

hii statement ya muheshimiwa kwa jaji mkuu imekaa vipi?
Yeye hahusiki na tabia za mauaji.na jamii ielewe hivyo.na dunia ielewe hivyo! Sasa hili la lissu limekaaje sasa....serikali haitoi uhai wa watu hata kama wamebainika bila mashaka kuwa ni wahalifu !
 
We neither rob robbers nor rape rapists. Why should we murder murderers?

Let us stop this savage practice.
 
"Naomba orodha ya watu waliohukumiwa kunyongwa msiniletee kwa sababu najua ugumu wake."

"..kwa sababu najua ugumu wake..."
Nadharia/uchanganuzi wangu juu ya hii kauli.
1:Ameshapata yzoefu na sasa anajutia?(Aidha alishaidhinisha na sasa anaona si sahihi). Au aliona kwa aliyewahi kufanya hivyo na akaona masaibu yake? Au alisimuliwa akajua?

2:Defensive mechanism hasa kipindi hiki baadhi ya wananchi wanamuona kama ni katili anayeweza kufanya vitu hivi amabavyo havikuwepo kabla ya utawala wake. Rejea kauli zake za kunyang'anya silaha na athari zake kwa watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi. Matukio ya kupotea na kutekwa kwa wapingaji wa mipango na utekelezaji wa sera za utawala wake.

Just my opinion.

Nil
 
kwa kweli siijui sheria lakini maoni yangu yupo sawa kutokana na imani yake labda au dhamiri au lengo!
imani- kama mkristo mkatoliki anajua wazi imani inafundisha usiue kwa hapa nadhani anataka kuepuka kuhusika na dhambi ya kuua, na hii kwa mtu wa kiroho ni mbaya sana damu ya mtu ikimwagika hua inakugarimu wewe na vizazi vyako 4
dhamiri- huenda amedhamiria katika uongozi wake mkono wake usihsike kuutoa uhai wa mtu, kwa hio akifanya hivyo dhamiri itamuuma sana katika maisha yake.
lengo- huenda analengo la kuupoteza uma mwelekeo kutokana na yanayokea.
Mara nyingi watu wanaohukumiwa kunyongwa ni wale ambao wameshiriki kufanya mauaji ya watu wengine kwa makusudi. Hivyo wanapohukumiwa kifo damu yao inabaki kuwa juu ya vichwa vyao wenyewe na siyo kwa jaji au yoyote anayeidhinisha wanyongwe. Mfano, kuna watu wamekutwa na hatia ya mauaji ya albino, unaona sawa waachwe tu waendelee kula bata kuogopa kumwaga damu yao wakati wao hawakuthamini damu ya watu wengine!?
 
Mimi nilichokiambulia hapo ni kauli ya kuonesha kuwa yeye hawezi kuhusika na tukio lolote la kuondoa uhai iwe kwa mujibu wa sheria au kwa namna nyingine.Nadhani ni kutaka serikali yake hisitajwetajwe katika tukio la watu wasiojulikana la kutaka kuondoa uhai wa Mh Lissu.

Sent using Jamii Forums mobile app
You have a point or the man has a good spin doctor.
 
unachosema ni kweli mkuu,na ndio maana nikasema sijui kwa upande wa sheria. lakini hakuna maumivu makali kama ya dhamiri, damu ya mtu hua haipiti bure haijalishi amefanya kosa gani, itakugarimu kwa namna moja ama nyingine kulingana na uhusika wako
Mara nyingi watu wanaohukumiwa kunyongwa ni wale ambao wameshiriki kufanya mauaji ya watu wengine kwa makusudi. Hivyo wanapohukumiwa kifo damu yao inabaki kuwa juu ya vichwa vyao wenyewe na siyo kwa jaji au yoyote anayeidhinisha wanyongwe. Mfano, kuna watu wamekutwa na hatia ya mauaji ya albino, unaona sawa waachwe tu waendelee kula bata kuogopa kumwaga damu yao wakati wao hawakuthamini damu ya watu wengine!?
 
hivi kwq anayejua atueleze kwq faida ya wote, akisaini hukumu ya kunyongwa ni lazima itangazwe kuwa Rais amesaini hati ya kunyongwa mtu fulani au huwa ni kimya kimya?
 
Kuuw awatu ni kitu kigumu sana hasa ukiwa unazijua amri kumi za Mungu.
Kitu pekee alicho barikiwa JPM ni kusema ukweli..Wengine wamechengachenga wee hadi umefika wakati wake ndo kasema ukweli wake toka moyoni.
Ikipendeza tubadili katiba na hao wafungwa wafungwe maisha waanze uzarishaji hukohuko gerezani.
 
Kauli hii ya rais ni agizo kwa Kabudi kuwa wakati umefika wa kufutwa Kwa Sheria hiyo.

Bunge limeonyesha kuunga mkono kila kitu cha serikali hivyo muswada ukienda utapita na kesho yake rais atasaini kuwa Sheria.
Kabisa na inawezekana kuwa hivyo.
 
Adhabu ya kunyonga mpaka kufa imepitwa na wakati hata kipindi cha Kikwete alikuwa anakwepa kutia saini ili watu wapate kunyongwa cha msingi waziri wa sheria apeleke mswaada bungeni sheria ibadilishwe tuachane na sheria hii ya kipuuzi na kizamani kifungo cha maisha kinatosha kuliko kumnyonga mtu.
Ndiyo maana amesema Mahakama inatoa Hukumu ya kifo na Wanasiasa wanaogopa kutia saini utekelezaji wake.

Hata yeye hapendi kupelekwewa listi ya watu waliohukumiwa kifo.
 
Kuuw awatu ni kitu kigumu sana hasa ukiwa unazijua amri kumi za Mungu.
Kitu pekee alicho barikiwa JPM ni kusema ukweli..Wengine wamechengachenga wee hadi umefika wakati wake ndo kasema ukweli wake toka moyoni.
Ikipendeza tubadili katiba na hao wafungwa wafungwe maisha waanze uzarishaji hukohuko gerezani.
Kabisa mkuu.
 
Back
Top Bottom