Rais Magufuli anapokomaa kujenga uchumi wa kati, Taasisi ya bima ya afya (NHIF) kuna haja wakamulikwa kwa namna wanavyotoa huduma kwa wateja wao

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,459
2,829
Naomba kutoa hoja yangu kukosoa na kutoa ushauri kuwe na ulazima wa marekebisho kwa mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa kwa namna inavyotoa huduma kwa wateja wake wapya na wanao renew bima zao za afya.

Aidha nianze na nukuu za muhimu kutoka tovuti ya NHIF;

Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa Nov 14, 2019; "Mwishoni mwa mwezi wa 11 tunatarajia kuanza huduma za bima zitakaomwezesha kila Mtanzania kujiunga na bima ili Watanzania wote waweze kujiunga na Bima ya Afya"

Mhe. Anne Makinda Mkiti wa Bodi ya NHIF
"NIHF imeanzisha vifurushi hivi ili kujibu hitaji la wananchi kuwezeshwa kuwa kwenye mfumo wa bima ya afya, lakini kubwa zaidi ni kuwahakikishia wananchi huduma za matibabu wakati wowote"

Baaada nukuu hizo, naomba kutoa tafsiri ya msingi wa uwepo wa bima ya afya kwa dhana ya jumla.

Bima ya Afya ni zao la bima inayokinga gharama za kitabibu au upasuaji kwa mtu alie na bima ya afya. Bima inafidia gharama anazotakiwa kulipia mhusika kutokana na ugonjwa, majeraha au kumlipa mtoa huduma kwa alie na kinga ya bima moja kwa moja.

(Health insurance is an insurance product which covers medical and surgical expenses of an insured individual. It reimburses the expenses incurred due to illness or injury or pays the care provider of the insured individual directly.)

Bima ya afya ni mfumo wa kulipia gharama za matibabu kwa mfumo wa michango inayolipwa kwenye mfuko wa pamoja. Kinga hii ya bima ni kwa huduma zote au zilizoainishwa tu kwenye sera au sharia.

Msingi wa mpango wa bima ya afya ni malipo ya mchango (premium) kwenye mfuko mkuu wa pamoja na kufaidika kwa mchangiaji kuanza kutolewa kama janga litatokea. Katika msingi wa bima ya afya, janga ni ungonjwa (sickness, illness) au majeraha (injuries).

National Health Insurance fund ilianza na wafanyakazi wa serikali na baadae wakaja na mifumo ya ku-accommodate watu wengine ikiwa ni vikundi vya wakulima, wafanyabiashara, wajasiliamali na watoto. Michango ya bima kwa watoto iliwekewa malipo (premium) y ash. 50,400 kwa mwaka.

Mpaka naandika Makala hii, nimeshwangazwa na taarifa rasmi kutoka mmoja wa jamaa zangu wa karibu ambae alikuwa amelipia watoto bima ya afya premium ya sh.50,400; mhusika alipochelewa kulipia malipo yam waka unaofuatia, amekutana na “new policy” (sera mpya) kuwa baada ya kupokea malipo huduma zitapatikana kwa mfaidika wa bima (insured) baada ya siku 90.

Je, kwa wafanyakazi wapya ambao wanakatwa 3% ya mshahara nao wanasubiri 90 days; kama sivyo kwanini kuwe na double standard?

Ni sawa na malipo ya nauli ya mshirika ya ndege, malipo ya watoto huwa ni chini ukilinganisha na watu wazima. Isipokuwa baada ya ticket kutoka, mtoto ana-enjoy huduma za kuwa kwenye usafiri sawia na watu wazima kwa muda uleule ndege inapo-anza safari. Huwezi kumuacha mtoto nyuma kwa kuwa tu, malipo yake yalikuwa nusu.

Jitihada zilifanyika kwa kuwasiliana na makao makuu ya NHIF nao pia wakathibitisha kuwa mhusika anapochelewa ku-renew malipo, anaanza upya.

Nina maswali ya msingi, kwanini siku 90 na sio siku 10, wala 30 wala 60. Sina hakika kama Tanzania tuna sharia mahsusi ya kudhibiti/kuratibu (regulation). Moja ya sababu iliyotolewa ni kutengeneza smart card kwa kuwa mchakato wake “unachukua muda mrefu”.

Nitoke nje ya mada kujenga hoja, ukifikia kujiandikisha kwenye mifumo ya NEC (tume ya kupiga kura) taarifa baada ya kuingizwa kwenye mifumo ya NEC, mpiga kura anaondoka na kadi yake siku hiyohiyo.

Kuna benki moja imeingia hapa nchini kutoka Kenya, ukifika kufungua account kwa ile benki, mara baada ya kuchukua taarifa za mteja na kufungua account, mteja huwa anaondoka na smart card siku hiyo hiyo.

Dhana ya siku 90 inatokea wapi wa NHIF na tupo kwenye karne ya 21 ambapo technological tools zipo? Unless kama kuna msingi wa kusubiri ambako hakuko wazi.

Tutazame mfumo wa general insurance (bima ya ujumla) hususani kinga ya ajali kwa magari ikiwa ni third party au comprehensive.

Baada ya mteja (insured) kulipia malipo, na kupewa stika ya bima, Iterim Cover-note na policy; ikitokea ajali ndani ya muda aliokata bima na malipo yake kuchukuliwa, hata kama ni malipo ya 100,000 kwa Third party cover, shirika la bima au kampuni ya bima itahusika na kutoa fidia kwa uharibifu wa mali, kusabisha majeraha au kifo kwa watu wengine au kwa mali za watu wengine.

Kama haya yanawezekana kwenye general insurance, kwanini health insurance masuala haya yasiwezekane kwa wakati.

Nitoe rai kwa TIRA (Tanzania Insurance Regulatory Authority) iwapo mfuko wa bima ya Afya ya Taifa iko chini ya mamlaka yenu ya udhibiti, huu ni wakati wa kuweka mambo sawa na wafaidika wa bima (insureds) waweze kupata vitambulisho ili kupata huduma kwa wakati kama itatokea wanahitaji kutembelea kwa watoa huduma ya afya.

Pengine niweke swali fikirishi, kwa sasa kuna kampuni nyingi binafsi kama Jubilee, AAR, Strategis, Britam; hawa nao wakija na mfumo kama wa NHIF wa kuanza kuwapa huduma kwa insured ndani ya siku 90, je TIRA watawa-treat private insurance firms sawia na NHIF ambayo ni taasisi ya umma kwenye utoaji sawa wa huduma.

Wangekuwa ni watoto wa kuzaa wa John Pombe Magufuli wakaambiwa wasubiri siku 90, bodi ya Bima afya ya Taifa chini ya mwenyekiti mama Makinda, je wangewajuza njooni baada ya siku 90 wakiwa washachukua malipo kwa wateja (insured)?

Kwa uelewa wangu, JPM ni raia namba moja na anakuwa baba wa kila Mtanzania, sidhani hoja hii ya siku 90 ikimfikia mezani kwake kama atakubiliana na mfumo huu wa NHIF.

Kukuza uchumi wa kati inajumuisha watoa huduma wakiwemo NHIF kuwa more innovative kwenye namna ya kutoa huduma kwa wakati.

Otherwise, tunalazimika kufikiri kwa kina kwanini huko nyuma Watanzania baada ya kulipia walipewa provisional identification ya kuanza kupata huduma huku wakisubiri smart card, cha ajabu pamoja na ubora wa technology, NHIF wao wanafanya vitu kana kwamba tupo karne ya 21.

Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom