papaa musofe
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 842
- 1,475
Kwa Mara ya kwanza nimemsikia Rais John Pombe Magufuli akikiri kwamba tangu aingie madarakani takribani miaka miwili iliyopita,ameshindwa kuhakikisha Sera zake zinazaa matunda (uzalishaji)na maendeleo kwa taifa
Hali hii ya kupungua kwa ukuaji wa uchumi(uzalishaji)umemfanya ashindwe hata kulipa stahiki za wafanyakazi ikiwemo kuongeza mishahara na au increment
Kabla ya kipindi chake,JK alikuwa akiongeza mishahara na kuilipa pia bila kubabaika,hii ilimaanisha kwamba awamu ya nne ilikuwa na Sera zilizofanya uchumi ukue na kuzalisha mali iliyofanya taifa lijikimu
Je Magufuli anakwama wapi kulielekeza taifa katika Sera zitakazofanya uzalishaji uongezeke? Ni kwa nini uzalishaji umepungua?
Tunapanga bajeti zetu sawasawa kwa kuangalia sekta zinazozalisha na hivyo kuziongezea nguvu na raslimali fedha na utaalamu? JK na Mkapa walielekeza raslimali katika sekta zipi ambazo ziliwafanya waendeshe nchi kwa kurelax,wakulima wakipata pembejeo,wafanyakazi wakilipwa mishahara na kupata nyongeza,barabara zikajengwa,Taasisi imara zikaundwa kama Sumatra,Tanroad,Ewura,miradi ya maji ikafanyika,misingi ya biashara ikawa imara na taifa likaaminika
Kwa nini JPM anakwama? Anajifunza nini kutoka kwa watangulizi wake kuhusu uendeshaji wa uchumi ambao ulisimama imara kwa takribani miaka 20?
Hii falsafa ya hapa kazi tu ilichambuliwa kisayansi,maana tangu mkoloni hajaja tulikuwa tunafanya kazi,pamoja na kufanya kazi bado taifa hili ni masikini,anamaanisha kufanya kazi kwa maguvu tu kama wabeba zege?
Hapa kazi tu kwa mkulima inamaanisha alime tu?lakini si miaka yote tunalima?! Hapa kazi tu kwa dereva wa mabasi,si miaka yote anaendesha magari!? Hapa kazi tu kwa muhasibu,si miaka yote anatunza hesabu!? Hapa kazi tu kwa injinia,si miaka yote anafanya uinjinia wake!? Hapa kazi tu kwa mwandishi wa habari,si miaka yote anafanya uandishi wa habari!?
Je hii falsafa ya hapa kazi tu ni ngeni?ina maana hapo zamani tulikuwa hatufanyi kazi?nchi hii angeikuta ilivyo kama tulikuwa hatufanyi kazi? Na kwa nini tangu aanze kuimba hapa kazi tu ndio uzalishaji umeshuka