Rais Magufuli anapoacha kusafiri nje ya nchi huokoa milioni 100, lakini anakosa fursa ya kuvutia uwekezaji wa matrilioni

Upeo wako mdogo
Sawa wewe mwenye upeo mkubwa, Dunia ya kwanza watu wanatumia social media na njia mbalimbali za mawasiliano kusoma mambo mbalimbali ya maana kwa ustawi wao na kujua fursa za uchumi kwenye mataifa mengine nk, Sisi waafrika ni tofauti kabisaaaaaa, tunatumia kutukana wengine, kukashifu wengine, kupotosha wengine ...Yaani sijui tuna laana gani sisi. Tubadilike jitahidi kuwaambia na wenzako tubadilike...Tutasonga mbele kiustawi
 
Kwa kweli nampongeza JPM kwa maamuzi take ta kutosafiri nje ya nchi

Kwa makadirio,anapoacha kusafiri nje ya nchi,huwa anaokoa milioni karibu 100,

Kiongozi anaposafiri nje ya nchi huandaliwa mikutano na matajiri wakubwa wa dunia ambao wana maelfu ya matrilioni katika akaunti zao,wanahitaji fursa tu ziko wapi,wanakuja na malori yaliyojaa hela ambazo hazijawahi kuonekana

Kukutana na midude hii iliyotengeneza hela karne na karne zilizopita ni jambo muhimu kwa mtu yeyote anayelia kuhusu viwanda,ajira na kukuza uchumi

Ni jambo la ajabu kiongozi anakuja kijijini kwetu KAKONKO,Kigoma,anatuambia Tanzania yake ni ya viwanda,nadhani anakuwa hajui kuwa anaoongea nao hata Jana wamelala njaa na hawana hela ya Kununua hata nati ya baskeli,sembuse kiwanda!?

Nchi yetu ina tatizo la mitaji,lakini kuna watu tayari wana mitaji huko duniani,tuwaalike waje wawekeze mitaji yao na tusiwatukane hovyo majukwaani,

Ukituimbia Tanzania ya viwanda huku Itigi,huo mtaji wa viwanda tuutolee wapi ?

Hivi wakati ulaya inaingia katika mapinduzi ya viwanda ,je viwanda hivyo vilitokana na hotuba za majukwaani?au ulikuwa ni mchakato mrefu wa kisayansi ulioleta mapinduzi ya viwanda?

Nadhani mkuu akatafute mitaji huko duniani,ailete hapa,viwanda vishamiri,kutuimbia viwanda hapa KAKONKO na itigi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa

Unaokoa milioni 100,unakosa fursa ya maelfu ya matrilioni,laiti angekuwa anasafiri,hakika angejua neno "tajiri" lina watu wanastahili kuitwa,na angeacha kuhangaika na akina manji
Kwani Jk amesafiri nchi zote duniani tena saba mara sabini kwani ameleta wawekezaji wangapi wa matrilioni? Au wale wa Sulivan wamekuja? pamoja na gharama kubwa tulizolipa luwahudumia poleni TZ
 
Tuangalie tulikotoka na namna tulivyofaidika na safari za kina dalali Vasco da Gama
 
Sawa wewe mwenye upeo mkubwa, Dunia ya kwanza watu wanatumia social media na njia mbalimbali za mawasiliano kusoma mambo mbalimbali ya maana kwa ustawi wao na kujua fursa za uchumi kwenye mataifa mengine nk, Sisi waafrika ni tofauti kabisaaaaaa, tunatumia kutukana wengine, kukashifu wengine, kupotosha wengine ...Yaani sijui tuna laana gani sisi. Tubadilike jitahidi kuwaambia na wenzako tubadilike...Tutasonga mbele kiustawi
BADILIKA kwanza,itakusaidia
 
Back
Top Bottom