Rais Magufuli anapenda sana kuvaa kijeshi. Asalimiana na Viongozi wa kikosi cha Wanajeshi 238

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,211
113,520
Naona Rais Magufuli anapenda sana kuvaa kijeshi.

Sijui huwa anatamani angekuwa mwanajeshi au vipi..?

Nyie mnaonaje....ni sawa Rais akitupia hayo manguo ya kijeshi au si sawa?

Binafsi hainisumbui kuona rais kavaa hayo manguo.

===

IKULU, DAR: Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania, John Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kikosi cha Wanajeshi 238 wanaoendelea na zoezi la usafi wa fukwe jijini Dar

Usafi huo ambao ni sehemu ya kuimarisha usafi wa jiji kuelekea Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC unasimamiwa na Viongozi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

Rais Magufuli amesalimiana na Wanajeshi hao akiwa nje ya majengo ya Ikulu ya Dar es Salaam

 
Haina shida mradi tuu awe anajua kupokea ile heshima ya kijeshi. Manake nasikia ukitinga hivyo viwalo salimiana inakuwa tofauti kidogo
 
Rais ana kofia nyingi!
1. Ni mwenyekiti wa chama (Ukimkuta na pamba za CCM usihoji)
2. Ni mkuu wa mhimili (Kama mhimili wa admin ungekuwa na uniform kama walivyo majaji nazo angezivaa- hapa mara nyingi anavaa suti)
3. Ni kiongozi wa nchi (Hapa mara nyingi napo vazi ni lile lile hasa la suti)
4. Ni amirjeshi mkuu (Hapa anaweza kuvaa pamba za kijeshi)
 
Back
Top Bottom