Rais Magufuli anangoja nini kumtumbua RC Makonda?

Hilo swali tunatakiwa kuliweka la kwanza ktk maswali ya kumuulliza mheshimiwa Sugu. Swali la pili liwe la kumtaka mheshiwa Sugu afafanue kuhusu yale marinda yaliyoharibiwa vabaya.
 
Kwa vipindi tofauti anko Magu amekuwa akitumia majukwaa tofauti kuzungumzia mambo mbalimbali yanayofanywa au kusemwa na wateule wake. Amekuwa na kawaida ya kuchomekea baadhi yake ili kutoa ufafanuzi au msimamo wake juu ya jambo fulani. Mfano alitoa maimamo ktk vita vya mihadharati, alimjibu Nape na mambo yake ya Brand na alielezea hisia zake dhidi ya raia kudharau polisi (kwaya kuimba kituoni au masela wa Yanga kusafishia gari la Manji kituoni).

Sasa naona hoja dhidi ya Makonda inazidi kushika kasi lakini simsikii akiitolea msimamo wake. Nimeanzä kjiuliza "Je! Kimya kingi kina mshindo mkuu?"

Hata hivyo naendelea kuusubiri ufafanuzi wa Anko Magu kuhusu cheti cha kidato cha nne cha mteule wake. Nitasubiri tu hata kama ni mwaka 2020.

Bazazi
 
Aende necta ghafla au TCU ndio akaongelee suala la vyeti bandia aazige uchunguzi ufanyike kw watumishi wote maana ndio zake anakwepa suala hot ataleta siasa!! Makonda hawezi kumtoa hata akifanya kosa kubwa kiasi gani!! Kwa kosa la kushirikiana na Akbar kuhusu ardhi wakati inajulikana jamaa ni mchafu ana scandal nssf lile tu astahili kuaminiwa tena kuwa RC! GSM amewakumbatia wakati JP anawadai pesa mingi sana za kodi waliifilisi wakafunga kampuni......hayo tu makosa......hastahili kuwepo
 
Kesi ya nyani kumpa ngedere,sahau hilo.

Napata mashaka sana kuona tuhuma hizi nzito zinakosa kuzungumziwa.
Nimjuavyo Makonda haya yasemwayo yangekuwa sio kweli angeshaitisha press conference na kutolea ufafanuzi.
 
Kwako Rais wa JMT, Mhe. John Joseph Pombe Magufuli,
Kwa heshima na taadhima naomba utafakari kwa kina kama Rais, Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa Chama Tawala ili kumng'oa RC Daudi Albert Bashite a.k.a Paulo Makonda.

Kitendo cha kuendelea kumlea RC Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Dar, kinazidi kuidhalilisha Serikali yako, Ikulu na Chama chako cha CCM. Tunajua Makonda ni Msukuma kabila moja na wewe, isiwe ni kigezo cha kuendelea kumlea. Kumbuka ulimtumbua Charles Kitwanga Mawematatu Msukuma tena akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kosa la kujibu swali Bungeni akiwa amelewa.

Je, nani mwenye kosa kubwa la kutumbuliwa au kusamehewa kati ya RC Makonda na Waziri Kitwanga? Paulo Makonda ameivuruga Serikali yako(paralized)kisiasa, kiuchumi na kiulinzi. Waswahili wanasema ai afadhali ya mchawi kuliko MWONGO. Makonda amelidanganya Taifa na Serikali yako kwa kusingizia watu maneno ya uongo kuwa ni wauza unga na wanaruhusu SHISHA.
Kitendo cha Makonda kumtuhumu PM Majaliwa kuwa aliruhusu Shisha ilikuwa ni kosa la kumfukuza kazi! Kwnye ajira kuna kitu tunaita INSURBODINATION yaani kudharau mamlaka iliyo juu na ndicho alichofanya Makonda.

Lakini kama hayo hayatoshi lililo baya kabisa kuliko yote kwa sasa ni hili la RC Makonda kutuhumiwa kuwa anatumia VYETI FAKE kwenye ajira aliyo nayo. Kelele zimetapakaa nchi nzima kila mtu analalamika kuhusu Makonda kuwa na vyeti vya kughushi. Watanzania hawaelewi kwani i Rais na Mkuu wa nchi hujachukua hatua. Nini hatima ya Makonda katika wingu hili jeusi linaloning'inia juu yake???
 
screenshot_2017-02-28-07-20-20-png.475263
 
RC Makonda alikoleza vita ya Mihadarati kwa kutangaza majina ya watuhumiwa wa Dawa za kulevya hadharani bila ya ushahidi na hatimaye wengine kuachiwa huru baada ya kuthibitika kuwa walionewa kama ilivyotokea kwa Askofu Gwajima!!

Juzi mama Wema Sepetu na bintiye wamekihama Chama cha CCM baada ya kushudha tuhuma nzito! Nina hakika Rais Magufuli ameiona Video clip iliyonaswa ikionyesha mazumgumzo ys simu kati ya Steve Nyererena Mama Wema Sepetu kuhsu kukamatwa kwa Wema Sepetu kwamba ilikuwa ni visasi kati ya Makonda na Wema! Kwamba Makonda alikuwa akimtongoza Wema lakini akamkatolea nje. Hii ni kwa mjibu wa maneno ya mama Wema Sepetu!!

Tuhuma hizi ni nzito kumhsu RC Makonda na kwa kweli ilitakiwa uchunguzi wa haraka na wa kina ufanyike huku Makonda akiwa nje ya ofisi na ikibainika basi atumbuliwa haraka!

Hatuwezi kuwa na kiongozi anayeingiza mambo binafsi kuwakomoa Watanzania! Hili halikubaliki hata kidogo! Baba wa Taifa angelikuwepo leo asingevumilia ujinga huu tayari angelikuwa kesha mkoromea siku nyingi!!!!!
Samahani mkuu nikusahihishe kidogo; Mkuu wa Mkoa wa Dsm anaitwa Daud Albert Bashite na sio Paul Makonda!
 
Back
Top Bottom