Uchaguzi 2020 Rais Magufuli anakosea kwa kuamini kuwa anaweza wachagulia wabunge kwenye majimbo yao

Tafsiri ya neno demokrasia ni kiongozi aliyechaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki kwa ajili ya kuwatumikia watu

Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli katika ziara yake akiwa huko Kimamba-Kilosa, mkoani Morogoro akiwaambia wakazi wa huko kuwa eti walikosea kumchagua mbunge wao, kwa kuwa walimchagua kwa jazba, bila ya kutafakari na ndiyo sababu inayowapata wakazi wa huko wakose maendeleo!

Ni jambo lililonistua sana niliposikia kauli hiyo kwa kuwa ninajua kuwa mbunge wa Kilosa ni mwanaccm mwenzao, kwa kuwa nilizizoea kauli hizo za Mheshimiwa Rais akizitoa kwenye majimbo waliochagua wabunge wa upinzani

Nika-realize kuwa kumbe kauli aliyowahi itoa Mwalimu Nyerere ni ya kweli tupu kuwa mtu aliyeanza kula nyama ya mtu hataweza acha kuila kamwe!

Ubaguzi aliouanza Jiwe wa kuwabagua wapinzani sasa umeingia kwenye CCM yake!

Nikakumbuka kauli aliyowahi itoa siku chache za nyuma, kuwa matokeo ya kura za maoni za majimbo za CCM si lolote wala chochote safari hii, kwa kuwa itategemea yeye kama Mwenyekiti ameamkaje siku hiyo, kwa kuwa upo uwezekano, hata kama umeshinda kwenye kura za maoni kwenye jimbo lako, lakini Kamati Kuu isilirudishe jina lako kwa kuwa litakuwa limekatwa na bila kutolewa sababu zozote zile

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi kuna haja gani ya kuitisha kura za maoni za CCM, iwapo kumbe inaeleweka, kura hizo si lolote wala chochote, kwani safari hii, Mwenyekiti wa CCM ndiyo "atakayeamua" nani awe mgombea wa ubunge wa jimbo husika?

Dalili zimeshaanza kujitokeza kutokana na hizo ziara za Rais majimboni na "kuwachagulia" wabunge huko majimboni mwao.

Ili tufahamu kuwa Mwenyekiti wetu tayari ana majina yake mfukoni, hebu nijaribu kuwakumbusha namna huyo Mwenyekiti wetu alivyoweza "wachagulia" wabunge kwenye majimbo yao.

Tulimsikia wenyewe Rais wetu akiwaambia wakazi hao wa Kimamba-Kilosa, kuwa "amemu-import" toka Dodoma, Mbunge atakayewafaa, Profesa Palamagamba Kabudi, ili awe Mbunge wao

Akaendeleza hizo "tamaa" zake Rais alipofanya ziara ya mikoa ya Kusini akiwaambia wakazi wa huko, wamchague msanii anayevaa "milegezo" Harmonize awe mbunge wao kwa jimbo la Tandahimba!

Hakuishia hapo, bali alipotembelea jimbo la Kongwa, aliwaomba wakazi wa huko wasikose kumchagua mbunge wao Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, ingawa kwa "body language" yao wananchi wa huko walionyesha kumkatalia pendekezo lake hilo

Aliendelea "kuwachagulia" wananchi Mbunge wao pale alipotembelea jimbo la Mbeya mjini, akawaomba wakazi wa huko wamchague kuwa mbunge wao, Naibu wa Spika, wa Bunge letu la Jamhuri, Tulia Ackson, kwani yeye anaamini huyo mwanamama, ndiyo "the right choice' kwa wana Mbeya!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi wanaccm wa majimboni mna haja gani ya kupiga kura za maoni yenu huko majimboni kwenu, kwa kuwachagua wabunge wenu, wakati mnajua kuwa Mwenyekiti wenu tayari ana majina yake "mfukoni" ya wabunge wake anaotaka yeye wawe wabunge wa Bunge lijalo la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kama ilivyokuwa uchaguzi sm na huu wajipitishe wenyewe ili vioja vinavyoendelea mitaani viwape wananchi maamuzi, maana upinzani ni uadui na fisiemu ndio wazalendo na watanzania kuliko watanzania wengine!!!
Binafsi sioni tija katika uchaguzi huu zaidi ya kujichosha na kuharibu rasilimali za nchi pasi sababu ikiwa dalili ndizo hizi...
Tumuombe Muumba atuvushe salama...
 
Inabidi kama Taifa tuondoe woga huo unaosema...........

Kwa kuwa haiwezekani kwa Rais wa nchi ndiyo atuchagulie wabunge wote wa majimbo nchini!
Ndio keshaanza kuwachagua hivyo...
Upinzani ni uadui...
Nina shaka tutaona makuu kuliko chaguzi zote zilizopita... ninahofia ya kina Mawazo na wengineo R.I.P kuzidi.
Muda ni mwamuzi mzuri sana..
 
watanzania hii dharau tumeijenga wenyewe na magu ineshamkolea. amejifanyia mengi ikiwa ni pamoja na kuvunja katiba,ndio kwanza bunge likaweka azimio la kumpongeza. hapo unategemea nini
 
Muda wake utafika naye atatoka madarakani lakini tutakuwa tumeteseka sana ndani ya huu utawala wake pia tutakuwa tumejifunza kuwapa uongozi watu wa namna hii.
Ni rahisi kusema hivyo lakini matendo yanasema vingine? Tuambiane ukweli, ni wangapi wanajifanya hawaoni natural arrogance ya Lissu huku wakitaka awe Rais?
Arrogant man + absolute power = ?
You do the math.
 
Tafsiri ya neno demokrasia ni kiongozi aliyechaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki kwa ajili ya kuwatumikia watu

Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli katika ziara yake akiwa huko Kimamba-Kilosa, mkoani Morogoro akiwaambia wakazi wa huko kuwa eti walikosea kumchagua mbunge wao, kwa kuwa walimchagua kwa jazba, bila ya kutafakari na ndiyo sababu inayowapata wakazi wa huko wakose maendeleo!

Ni jambo lililonistua sana niliposikia kauli hiyo kwa kuwa ninajua kuwa mbunge wa Kilosa ni mwanaccm mwenzao, kwa kuwa nilizizoea kauli hizo za Mheshimiwa Rais akizitoa kwenye majimbo waliochagua wabunge wa upinzani

Nika-realize kuwa kumbe kauli aliyowahi itoa Mwalimu Nyerere ni ya kweli tupu kuwa mtu aliyeanza kula nyama ya mtu hataweza acha kuila kamwe!

Ubaguzi aliouanza Jiwe wa kuwabagua wapinzani sasa umeingia kwenye CCM yake!

Nikakumbuka kauli aliyowahi itoa siku chache za nyuma, kuwa matokeo ya kura za maoni za majimbo za CCM si lolote wala chochote safari hii, kwa kuwa itategemea yeye kama Mwenyekiti ameamkaje siku hiyo, kwa kuwa upo uwezekano, hata kama umeshinda kwenye kura za maoni kwenye jimbo lako, lakini Kamati Kuu isilirudishe jina lako kwa kuwa litakuwa limekatwa na bila kutolewa sababu zozote zile

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi kuna haja gani ya kuitisha kura za maoni za CCM, iwapo kumbe inaeleweka, kura hizo si lolote wala chochote, kwani safari hii, Mwenyekiti wa CCM ndiyo "atakayeamua" nani awe mgombea wa ubunge wa jimbo husika?

Dalili zimeshaanza kujitokeza kutokana na hizo ziara za Rais majimboni na "kuwachagulia" wabunge huko majimboni mwao.

Ili tufahamu kuwa Mwenyekiti wetu tayari ana majina yake mfukoni, hebu nijaribu kuwakumbusha namna huyo Mwenyekiti wetu alivyoweza "wachagulia" wabunge kwenye majimbo yao.

Tulimsikia wenyewe Rais wetu akiwaambia wakazi hao wa Kimamba-Kilosa, kuwa "amemu-import" toka Dodoma, Mbunge atakayewafaa, Profesa Palamagamba Kabudi, ili awe Mbunge wao

Akaendeleza hizo "tamaa" zake Rais alipofanya ziara ya mikoa ya Kusini akiwaambia wakazi wa huko, wamchague msanii anayevaa "milegezo" Harmonize awe mbunge wao kwa jimbo la Tandahimba!

Hakuishia hapo, bali alipotembelea jimbo la Kongwa, aliwaomba wakazi wa huko wasikose kumchagua mbunge wao Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, ingawa kwa "body language" yao wananchi wa huko walionyesha kumkatalia pendekezo lake hilo

Aliendelea "kuwachagulia" wananchi Mbunge wao pale alipotembelea jimbo la Mbeya mjini, akawaomba wakazi wa huko wamchague kuwa mbunge wao, Naibu wa Spika, wa Bunge letu la Jamhuri, Tulia Ackson, kwani yeye anaamini huyo mwanamama, ndiyo "the right choice' kwa wana Mbeya!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi wanaccm wa majimboni mna haja gani ya kupiga kura za maoni yenu huko majimboni kwenu, kwa kuwachagua wabunge wenu, wakati mnajua kuwa Mwenyekiti wenu tayari ana majina yake "mfukoni" ya wabunge wake anaotaka yeye wawe wabunge wa Bunge lijalo la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Ccm waliingia choo cha kike kumpa huyu mzee uenyekiti wa taifa wakati hakuwahi kuwa hata mwenyekiti wa wilaya. Kazi wanayo
 
Ni rahisi kusema hivyo lakini matendo yanasema vingine? Tuambiane ukweli, ni wangapi wanajifanya hawaoni natural arrogance ya Lissu huku wakitaka awe Rais?
Arrogant man + absolute power = ?
You do the math.
ww unazani kulikuwa na humuhimu gani jana kuwaka kile kikao? wakati tunajuafika kabisa hakuna mtu mwengine alieyechukua form dhidi yake hela walizotumia jana situngezisave tufanye mambo mengine?
 
Tarajia bunge dhaifu kuliko hili lilopita... Yaan bunge dhaifu litashindwA kuihoji serikali...

Na hapo mwisho wa CCM ndio utakuwa umeshawadia...
CCM haifi kwa utaratibu wa sasa kuelekea chama kimmoja.Lakini mashindano yatahamia huko huko CCM kuwania nyadhifa hizo hizo.
 
Tarajia bunge dhaifu kuliko hili lilopita... Yaan bunge dhaifu litashindwA kuihoji serikali...

Na hapo mwisho wa CCM ndio utakuwa umeshawadia...
Huenda ni mkakati Maalum ili Ajaenda ya kumfanya awe Lifetime President isipate vikwazo pindi ikiwasilishwa Bungeni...
 
Back
Top Bottom