Uchaguzi 2020 Rais Magufuli anakosea kwa kuamini kuwa anaweza wachagulia wabunge kwenye majimbo yao

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
4,920
2,000
Katika kitu ambacho hakinipi stress ni siasa kabisaaa. Hata kama Wasukuma wawe maraisi wote, bado nitakula kwa jasho langu pekee
 

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,780
2,000
100% naunga mkono! Yani pamoja na kujimwamba kuwa yeye ndiye alfa na omega, yeye ndiye mwisho wa reli. Bado ameanza kuwafanyia kampeni baadhi ya wakataliwa kwenye majimbo yao. Kwanini asiwaache wakataliwe na wananchi then yeye awarudishe!!
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
8,830
2,000
Tafsiri ya neno demokrasia ni kiongozi aliyechaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki kwa ajili ya kuwatumikia watu

Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli katika ziara yake akiwa huko Kimamba-Kilosa, mkoani Morogoro akiwaambia wakazi wa huko kuwa eti walikosea kumchagua mbunge wao, kwa kuwa walimchagua kwa jazba, bila ya kutafakari na ndiyo sababu inayowapata wakazi wa huko wakose maendeleo!

Ni jambo lililonistua sana niliposikia kauli hiyo kwa kuwa ninajua kuwa mbunge wa Kilosa ni mwanaccm mwenzao, kwa kuwa nilizizoea kauli hizo za Mheshimiwa Rais akizitoa kwenye majimbo waliochagua wabunge wa upinzani

Nika-realize kuwa kumbe kauli aliyowahi itoa Mwalimu Nyerere ni ya kweli tupu kuwa mtu aliyeanza kula nyama ya mtu hataweza acha kuila kamwe!

Ubaguzi aliouanza Jiwe wa kuwabagua wapinzani sasa umeingia kwenye CCM yake!

Nikakumbuka kauli aliyowahi itoa siku chache za nyuma, kuwa matokeo ya kura za maoni za majimbo za CCM si lolote wala chochote safari hii, kwa kuwa itategemea yeye kama Mwenyekiti ameamkaje siku hiyo, kwa kuwa upo uwezekano, hata kama umeshinda kwenye kura za maoni kwenye jimbo lako, lakini Kamati Kuu isilirudishe jina lako kwa kuwa litakuwa limekatwa na bila kutolewa sababu zozote zile

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi kuna haja gani ya kuitisha kura za maoni za CCM, iwapo kumbe inaeleweka, kura hizo si lolote wala chochote, kwani safari hii, Mwenyekiti wa CCM ndiyo "atakayeamua" nani awe mgombea wa ubunge wa jimbo husika?

Dalili zimeshaanza kujitokeza kutokana na hizo ziara za Rais majimboni na "kuwachagulia" wabunge huko majimboni mwao.

Ili tufahamu kuwa Mwenyekiti wetu tayari ana majina yake mfukoni, hebu nijaribu kuwakumbusha namna huyo Mwenyekiti wetu alivyoweza "wachagulia" wabunge kwenye majimbo yao.

Tulimsikia wenyewe Rais wetu akiwaambia wakazi hao wa Kimamba-Kilosa, kuwa "amemu-import" toka Dodoma, Mbunge atakayewafaa, Profesa Palamagamba Kabudi, ili awe Mbunge wao

Akaendeleza hizo "tamaa" zake Rais alipofanya ziara ya mikoa ya Kusini akiwaambia wakazi wa huko, wamchague msanii anayevaa "milegezo" Harmonize awe mbunge wao kwa jimbo la Tandahimba!

Hakuishia hapo, bali alipotembelea jimbo la Kongwa, aliwaomba wakazi wa huko wasikose kumchagua mbunge wao Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, ingawa kwa "body language" yao wananchi wa huko walionyesha kumkatalia pendekezo lake hilo

Aliendelea "kuwachagulia" wananchi Mbunge wao pale alipotembelea jimbo la Mbeya mjini, akawaomba wakazi wa huko wamchague kuwa mbunge wao, Naibu wa Spika, wa Bunge letu la Jamhuri, Tulia Ackson, kwani yeye anaamini huyo mwanamama, ndiyo "the right choice' kwa wana Mbeya!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi wanaccm wa majimboni mna haja gani ya kupiga kura za maoni yenu huko majimboni kwenu, kwa kuwachagua wabunge wenu, wakati mnajua kuwa Mwenyekiti wenu tayari ana majina yake "mfukoni" ya wabunge wake anaotaka yeye wawe wabunge wa Bunge lijalo la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mawe anafeli maana hili alilitabiri Nyerere,usichagulie watu wagombea!

Yeye anaenda kinyume,anachagulia watu wagombea...

Anapigwa kilio kisichokua na msiba!
 

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
442
500
Hao waarabu wako, usidhani walikuwa wakipita kwa haki! Ni rushwa! Ndio maana nashangaa leo kujua huyo ndo mbunge wao, maana haongeagi chochote bungeni
Inabidi vijana wachangamkie tenda.
Kipindi cha jpm nichawanyonge! Naatakumbukwa nchi hii.
 

konyola

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
1,887
2,000
CCM watapata taabu sana kwa huyu buana afadhari upinzani wao angalau walishazoea manyanyaso, lakini hawa ambao wamo ktk chama ambacho wamekiuza bei poa kwa watu wa kolomije na Burigi jamaa kawageuza kama magunia ya magimbi.

Katika zama hizi pamoja na kwamba ccm ndo walifanya figisu hadi katiba ya Warioba kupigwa chini kivumbi walichotimuliwa msimu ulopita na tope watakalomwagiwa msimu ujao hakika wao ndo watakuwa wa kwanza kuomba katiba mpya maana watakuwa wamenyooka.
Mbunge aliemaliza muda wake ktk jimbo niliko kila wakati alikuwa hakosi kupita kwa wapiga kura wake sasa hivi kalowana kawa mpole kama kafunikwa na barafu na hii ni baada ya kupenyezewa kuwa jina lake halitarudi.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba hatohamia upinzani ila kuna vikao vianfanyika usiku na mchana kuhakikisha uasi ili huyo atakaeletwa ashindwe octoba 2020.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
13,511
2,000
CCM watapata taabu sana kwa huyu buana afadhari upinzani wao angalau walishazoea manyanyaso, lakini hawa ambao wamo ktk chama ambacho wamekiuza bei poa kwa watu wa kolomije na Burigi jamaa kawageuza kama magunia ya magimbi.

Katika zama hizi pamoja na kwamba ccm ndo walifanya figisu hadi katiba ya Warioba kupigwa chini kivumbi walichotimuliwa msimu ulopita na tope watakalomwagiwa msimu ujao hakika wao ndo watakuwa wa kwanza kuomba katiba mpya maana watakuwa wamenyooka.
Mbunge aliemaliza muda wake ktk jimbo niliko kila wakati alikuwa hakosi kupita kwa wapiga kura wake sasa hivi kalowana kawa mpole kama kafunikwa na barafu na hii ni baada ya kupenyezewa kuwa jina lake halitarudi.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba hatohamia upinzani ila kuna vikao vianfanyika usiku na mchana kuhakikisha uasi ili huyo atakaeletwa ashindwe octoba 2020.
Walidhani namba tutaisoma wapinzani pekee?

Sasa wanaisoma na wao wanaccm wenyewe!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom