Uchaguzi 2020 Rais Magufuli anakosea kwa kuamini kuwa anaweza wachagulia wabunge kwenye majimbo yao

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Tafsiri ya neno demokrasia ni kiongozi aliyechaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki kwa ajili ya kuwatumikia watu

Tumemsikia wenyewe Rais Magufuli katika ziara yake akiwa huko Kimamba-Kilosa, mkoani Morogoro akiwaambia wakazi wa huko kuwa eti walikosea kumchagua mbunge wao, kwa kuwa walimchagua kwa jazba, bila ya kutafakari na ndiyo sababu inayowapata wakazi wa huko wakose maendeleo!

Ni jambo lililonistua sana niliposikia kauli hiyo kwa kuwa ninajua kuwa mbunge wa Kilosa ni mwanaccm mwenzao, kwa kuwa nilizizoea kauli hizo za Mheshimiwa Rais akizitoa kwenye majimbo waliochagua wabunge wa upinzani

Nika-realize kuwa kumbe kauli aliyowahi itoa Mwalimu Nyerere ni ya kweli tupu kuwa mtu aliyeanza kula nyama ya mtu hataweza acha kuila kamwe!

Ubaguzi aliouanza Jiwe wa kuwabagua wapinzani sasa umeingia kwenye CCM yake!

Nikakumbuka kauli aliyowahi itoa siku chache za nyuma, kuwa matokeo ya kura za maoni za majimbo za CCM si lolote wala chochote safari hii, kwa kuwa itategemea yeye kama Mwenyekiti ameamkaje siku hiyo, kwa kuwa upo uwezekano, hata kama umeshinda kwenye kura za maoni kwenye jimbo lako, lakini Kamati Kuu isilirudishe jina lako kwa kuwa litakuwa limekatwa na bila kutolewa sababu zozote zile

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi kuna haja gani ya kuitisha kura za maoni za CCM, iwapo kumbe inaeleweka, kura hizo si lolote wala chochote, kwani safari hii, Mwenyekiti wa CCM ndiyo "atakayeamua" nani awe mgombea wa ubunge wa jimbo husika?

Dalili zimeshaanza kujitokeza kutokana na hizo ziara za Rais majimboni na "kuwachagulia" wabunge huko majimboni mwao.

Ili tufahamu kuwa Mwenyekiti wetu tayari ana majina yake mfukoni, hebu nijaribu kuwakumbusha namna huyo Mwenyekiti wetu alivyoweza "wachagulia" wabunge kwenye majimbo yao.

Tulimsikia wenyewe Rais wetu akiwaambia wakazi hao wa Kimamba-Kilosa, kuwa "amemu-import" toka Dodoma, Mbunge atakayewafaa, Profesa Palamagamba Kabudi, ili awe Mbunge wao

Akaendeleza hizo "tamaa" zake Rais alipofanya ziara ya mikoa ya Kusini akiwaambia wakazi wa huko, wamchague msanii anayevaa "milegezo" Harmonize awe mbunge wao kwa jimbo la Tandahimba!

Hakuishia hapo, bali alipotembelea jimbo la Kongwa, aliwaomba wakazi wa huko wasikose kumchagua mbunge wao Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, ingawa kwa "body language" yao wananchi wa huko walionyesha kumkatalia pendekezo lake hilo

Aliendelea "kuwachagulia" wananchi Mbunge wao pale alipotembelea jimbo la Mbeya mjini, akawaomba wakazi wa huko wamchague kuwa mbunge wao, Naibu wa Spika, wa Bunge letu la Jamhuri, Tulia Ackson, kwani yeye anaamini huyo mwanamama, ndiyo "the right choice' kwa wana Mbeya!

Ndipo hapo ninapojiuliza hivi wanaccm wa majimboni mna haja gani ya kupiga kura za maoni yenu huko majimboni kwenu, kwa kuwachagua wabunge wenu, wakati mnajua kuwa Mwenyekiti wenu tayari ana majina yake "mfukoni" ya wabunge wake anaotaka yeye wawe wabunge wa Bunge lijalo la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Sijawahi shuhudia hapo kabla tokea mfumo huu urejee nchini kwetu mwaka 1992, kwa Rais wa Jamhuri kuamua "kuwachagulia" wabunge kwenye majimbo yao

Huyu Jiwe ndiye wa kwanza kufanya hivyo!
 
Dalili zimeshaanza kujitokeza kutokana na hizo ziara za Rais majimboni na "kuwachagulia" wabunge huko majimboni mwao.
anasoma majitu anayo deal nayo, takataka kabisa, he can twist them the way he likes! Kama"Professor" anajiita wa jalalani, unategemea yeye apate picha gani,... kuwa haya kumbe ni makondoo ya kuswaga.. .....Lenini aliwaelezea watu kama hao kuwa are like sacs of potatoes, you can treat them the way you like!
... since (it is said) the Marxists saw the peasants as nothing more than a sack of potatoes, had only contempt for the mental capacities of the peasants, saw them ...
 
Muda wake utafika naye atatoka madarakani lakini tutakuwa tumeteseka sana ndani ya huu utawala wake pia tutakuwa tumejifunza kuwapa uongozi watu wa namna hii.
Ni jambo la ajabu vile vile kwa kuona wao CCM wakianza kampeni katika "full swing" wakati wapinzani wakiendelea kupigwa marufuku kuendesha kampeni za aina yoyote ile.....................

Refer tukio la majuzi la kiongozi wa ACT Wazalendo, alipokamatwa na Polisi wetu kule Mtwara, kwa kufanya mkusanyiko waliouita wenyewe kuwa ni haramu!
 
1. Hao anao wapigia debe Kwanza Ni wepesi, hawana mvuto wa kisiasa na Ni watu dhaifu kwa mamlaka yake...

2. Wananchi hawadanganyiki na sio sahihi kuwachagulia wawakilishi wa kisiasa...
 
Sijawahi shuhudia hapo kabla tokea mfumo huu urejewe nchini kwetu mwaka 1992, kwa Rais wa Jamhuri kuamua "kuwachagulia" wabunge kwenye majimbo yao

Huyu Jiwe ndiye wa kwanza kufanya hivyo!
Ajabu ni kuwa anataka kuwachagulia watu kiongozi wao wakati yeye mwenyewe hatakiwi.
Magufuli ajue nguvu yake inaishia kwenye uteuzi ndani ya chama, atawawekea mgombea amtakaye na hii imetokana na UFALA wao wa kumpa madaraka ya umungu mtu na kushindwa kumuwekea mshindani.
CCM acha wapelekeshwe maana wamezidi uboza, yaani chama kikongwe kinaendeshwa kibabe na MTU mmoja tena wa kuja?
 
Hata Yule Mzee aliyetoa maelezo kuwa Kabudi ni mzaliwa wa pale alipangwa,hivi haya maigizo igizo hadi lini?
Profesa Palamagamba Kabudi anajukikana kuwa ni mgogo na ni mzaliwa wa Dodoma na wala si mzaliwa wa Kimamba-Kilosa, kama alivyotaka kutuaminisha Mheshimiwa Rais
 
Back
Top Bottom