Rais Magufuli anakosea kudhani kuwa mataifa ya kigeni hayapaswi kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Taarifa ambayo imestua watu wengi ni hii taarifa ya pamoja iliyotolewa na ubalozi wa Marekani na uingereza nchini, wakilaani vikali vitendo vya ukiukwaji wa haki za msingi wa kibinadamu nchini

Wapo watu wengi sana waliounga mkono tamko hilo na wakieleza kuwa nchi hizo za Magharibi zimechelewa mno kutoa tamko hill na wapo wale watu wanaoitwa "praise and worship team for Magufuli" ambao wanasema mambo ya ndani ya nchi yetu hayapaswi kuingiliwa na mataifa ya kigeni

Siyo siri kuwa kuna ukiukwaji wa hali ya juu wa haki za msingi wa binadamu nchini na wananchi wamepiga kelele sana, lakini ni dhahiri kuwa watawala wetu wameamua kuweka pamba masikioni mwao na kutosikiliza kilio hicho!

Hata hivyo kwa wale wenzetu wanaotetea vitendo hivi vya ukiukwaji wa hali ya juu wa haki za binadamu, ningependa tu kuwauliza kitu kimoja, nyinyi mnaendelea kutetea kwa nguvu zote Rais wetu, lakini je mshajiuliza kuwa Tanzania siyo kisiwa cha kujifanyia mambo yake itakavyo na kuna mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo inakiukwa waziwazi na utawala huu wa awamu ya tano??

Tuchukulie hili suala la mwandishi Kabendera lilivyoshughullkiwa, hivi ndivyo inavyopaswa kushughulikiwa hata kwa sheria zetu za ndani??

Yule mwandishi Kabendera amebebwa usiku wa manane nyumbani kwake na "watu wasiojulikana,"/ambao hawwkutaka hata kujitambulisha, hivi ndiivyo sheria zetu zinavyosema kweli??

Kibaya zaidi ni pale Kamanda Mambosasa alipokiri mwenyewe kuwa Jeshi hilo ndilo linalomshililia mwandishi huyo kituoni kwao na huku likiwa linamhoji kuhusu kile alichokiita kuwa ni uraia wake wenye utata bila kumpa nafasi mtuhumiwa huyo aweze kuleta mwanasheria wake wakati wa mahojiano hayo, je hivi ndivyo sheria zetu za nchi zinavyosema??

Jambo la kushangaza zaidi ni pale walipomburuza mahakamani mwandishi huyo na kumsomea mashitaka ya kubambikiwa kuwa eti amashitakiwa kwa makosa matatu ambayo ni kujiunga na genge la kihalifu, utakatishaji pesa na ukwepaji kodi, makosa yote hayo siyo yale ambayo Kamanda Mambosasa alitueleza watanzania kuwa ndiyo waliyomhoji Kabendera kituoni kwao.

Hivi kwa vitendo kama hivyo vya ukiukwaji wa hali ya juu wa misingi ya kibanadamu, kama dunia haitapaza sauti zao, watakuwa wanaenda kinyume cha ubinadamu

Nimalizie tu post yangu kwa kisema kuwa kitendo cha serikali ya Tanzania kulalamikia kitendo cha ubalozi wa Marekani na Uingereza, kutoa tamko la pamoja kulaani vitendo vya serikali yetu kuminya sheria tulizojiwekea sisi wenyeee, ni sawasawa na majirani wanapoona baba wa mwenye nyumba jirani hao, akifanya vitendo vya "kishenzi" vya kuwacharaza bakora wanawe mara kwa mara na kuvifumbia macho na kusema kuwa havimuhusu kwa kuwa ni vya nyumba jirami

Hakika katika nchi hii kwa hivi sasa hakuna mtu aliye salama hata kidogo, kwa hiyo ni wajibu wa kila mtanzania kupaza sauti yake kwa hali ya juu kabisa ili kuvikomesha vitendo hivyo vya kinyama na vinavyokiuka misingi ya kibinadamu

Tukificha ficha maradhi, mwisho kilio kitatuumbua. OVA
 
Yani watu wapaze sauti kuzuia vitendo hivyo? Sauti huwa inazuia uovu? Labda ungesema tufanye jitihada za kuwamaliza wasiojulikana kwa kila mmoja kuwa na kitendea kazi cha kumlinda we unasema sauti Tena?
Mkuu,

Wewe hufai kuwa na hizo zana,utawamaliza hata wasio husika.
 
Uzi wako unamapengo mengi sana, unandika kama ulipata kuchungulia jalada zima la mashtaka na ushahidi. Ni raisi kulaumu ukiwa umeshikilia hoja ya upande mmoja bila kujua upande mwingine una nini cha kujitetea. Muwe wakweli, mnamtetea mtu ambaye mnaimani kwamba yeye ni wa upande wenu na anashika agenda zenu kisa tu, aliwahi kuikosoa serikali siku za nyuma. Lakini wengi wenu hamkumjua hata alikuwa ni nani wiki chache zilizopita.
 
Uzi wako unamapengo mengi sana, unandika kama ulipata kuchungulia jalada zima la mashata na ushahidi. Ni raisi kulaumu ukiwa umeshikilia hoja ya upande mmoja bila kujua upande mwingine una nini cha kujitetea. Muwe wakweli, mnamtetea mtu ambaye mnaimani kwamba yeye ni wa upande wenu na anashika agenda zenu kisa tu, aliwahi kuikosoa serikali siku za nyuma. Lakini wengi wenu hamkujua hata alikuwa ni nani wiki chache zilizopita.
Yaani hiki ndio kinachokwaza na ushabiki huu wa siasa.Macho ya uchunguz huru yanafungwa,unachagua kinachosupport agenda yako tu ukipuuza nadharia zingine zote za msingi kwenye analysis yako.Siasa ni upuuz mkubwa zaidi Kuwahi kutokea duniani!
 
View attachment 1176375
View attachment 1176373



View attachment 1176390

Ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania wametoa tamko la pamoja kuhusu kile walichokiita "wasiwasi wa kuzorota kwa kwa haki za kisheria nchini Tanzania."

Katika tamko hilo, ofisi hizo mbili za ubalozi zinadai kuwa imedhihirika kwa zaidi ya mara moja watu kutiwa kizuizini kwa muda nchini Tanzania bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashitaka na mamlaka zake za kisheria.

"Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni -- jinsi ambavyo halikushughulikiwa kwa haki la kukamatwa, kuwekwa kizuizini na tuhuma za mashtaka ya mwandishi wa habari za uchunguzi Bw Erick Kabendera, ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na mwanasheria kwenye hatua za awali na kutiwa kizuizini kwake, ambapo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai," inasema sehemu ya tamko hilo.

"Tunaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake, kama ilivyotambua kwamba ni haki ya msingi na kuridhia kwenye mikataba mbali mbali ya haki za kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa, miongoni mwao ikiwemo azimio la kimataifa la haki za kirai na kisiasa."

Erick Kabendera alipandishwa kizimbani Jumatatu ya wiki hii ikiwa ni wiki moja toka alipokamatwa na vyombo vya usalama nchini Tanzania.

Mkuu Informer, asante kwa taarifa hii, naitafakari kwa makini na kuiangalia kama sio kuingilia mambo yetu ya ndani.
P
 
Hoja yangu ni moja tu, ingekuwa nchi za wenzetu asubuhi hii tungekuwa barabarani kupongeza tamko hili, ila sasa....
 
Rais alipotembelea magereza na kusamehe viwete wazee na wajawazito walikaa kimya utafikiri wanavuka mto rufiji, hawa washenzi waambieni ni wakati wetu kuendelea sasa,
Kuota ni haki yako mkuu. Kaisome historia ya Maendeleo ya Europe, America na Asia halafu uone kama haya yanayoendelea kwetu ni maendeleo!
 
Mkuu Informer, asante kwa taarifa hii, naitafakari kwa makini na kuiangalia kama sio kuingilia mambo yetu ya ndani.
P
Hawa kweli wameingilia mambo yetu.
Kwanini wasituache tuuane tu?
Kwani tunaua watu wao?
Kwani tunafunga watu wao?
Kwani hawa watu wanaookotwa kwenye viroba ni watu wao?
Watuache tuendelee kuua na tutaua mpaka tutakapowamaliza wale wote wasio upande wetu.
Haya ni mawazo ya wale misukule wa Lumumba street akiwemo Pascal mwenyewe.
 
Ingawa tume kuwa taifa huru tangu 1960-61 lakini uhuru wetu tuliupata kutoka kwa Uingereza chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Uingereza ana wajibu wa kumuonya mtoto wake wa kuasili anapo potoka.

Marekani inatoa mchango mkubwa katika Baraza la aUmoja wa Mataifa ambayo Tanzania ni mwana chama. Hivyo kama nchi ina haki ya kusaidia matatizo ya ndani. Hivi anaekununulia nyama ule na wanao akikwambia hapendi jinsi unavyomchapa mtoto wako utashangaa?

Pia sisi wa na chama wa Jumuaia ya Madola ambayo Uingereza ni mama wa Jumuia. Mlipitia Katiba ya Jumuia nakuangalia majukumu ya Uingereza kwa nchi wana chama?
 
Hakika katika nchi hii kwa hivi sasa hakuna mtu aliye salama hata kidogo, kwa hiyo ni wajibu wa kila mtanzania kupaza sauti yake kwa hali ya juu kabisa ili kuvikomesha vitendo hivyo vya kinyama na vinavyokiuka misingi ya kibinadamu

Hahahahaa mshana umenukuu au umekopi na kupesti?
 
Uzi wako unamapengo mengi sana, unandika kama ulipata kuchungulia jalada zima la mashata na ushahidi. Ni raisi kulaumu ukiwa umeshikilia hoja ya upande mmoja bila kujua upande mwingine una nini cha kujitetea. Muwe wakweli, mnamtetea mtu ambaye mnaimani kwamba yeye ni wa upande wenu na anashika agenda zenu kisa tu, aliwahi kuikosoa serikali siku za nyuma. Lakini wengi wenu hamkujua hata alikuwa ni nani wiki chache zilizopita.
Mkuu sawa tu tulia uandike ueleweke kwani una kigugumizi au kithembe?
 
Back
Top Bottom