Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Tumeshuhudia tokea serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, juhudi kubwa ikifanyika kwa ajili ya kuua upinzani ili nchi ibaki kuwa na mfumo wa chama kimoja
Tumeshuhudia pia wabunge na madiwani wakinunuliwa na kuahidiwa nafasi za "ulaji" iwapo tu wataafiki kujiunga na chama cha CCM kwa kile wenyewe walichokibatiza jina la kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuleta maendeleo hapa nchini
Kutokana na tabia hiyo ya hao wanasiasa "wasaliti" wanaojiunga na CCM tumekuwa tunalazimika kurudia uchaguzi ambao unaligharimu Taifa letu mabilioni ya pesa ambazo zingeweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo. Mathalani ujenzi wa madarasa ya shule na hospitali
Lakini kwa bahati mbaya sana priority no 1 ya serikali hii imekuwa siyo tena kujenga madarasa wala hospitali zetu ambazo ziko katika hali mbaya, badala yake ni kuua upinzani nchini!
Kipindi wanachopitia viongozi wa upinzani nchini, hususani wa chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema ni kipindi kigumu sana ambacho hawajawahi kukipitia tokea mfumo wa vyama vingi nchini urejeshwe nchini kikatiba mwaka 1992
Viongozi kadhaa wa upinzani wamefungwa jela kwa sababu za kisiasa na viongozi wengine wameathirika kutokana na vizuizi wanavyowekewa vya kutofanya siasa na karibu viongozi wote wa chama kikuu cha upinzani cha Chadema wanakabiliwa na kesi mbalimbali za kile kinachoitwa uchochezi kwenye Mahakama zetu
Ninachojaribu kujiuliza ni iweje serikali hii ya awamu ya tano iwachukulie wapinzani maadui wakubwa badala ya kuwachukulia kuwa ni wadau muhimu sana wa maendeleo nchini mwetu??
Na kama kweli kama wapinzani wangekuwa maadui wa maendeleo wangezuiwa kwenye mataifa yaliyostawi sana kimaendekeo mathalani Taifa lenye uchumi namba moja duniani la Marekani, ambalo kwenye Taifa hilo Rais wake Donald Trump anatukanwa waziwazi na wapinzani wa nchi hiyo lakini hawafanywi chochote kwa kuwa Taifa hilo linachukulia kama sehemu ya demokrasia ya kueleza hisia za wananchi kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Taifa hilo
Vile vile humu barani Afrika nchi ya Afrika Kusini ambayo ndiyo inayoongoza barani humu kiuchumi, wameimarisha sana demokrasia nchini mwao
Nitoe tu ushauri kwa watawala wetu waiache demokrasia ishamiri nchini kwa kuwa hawana uwezo wa kuua upinzani wa nchi ambao umeota mizizi ndani ya mioyo ya mamilioni ya watanzania
Mungu ibariki Tanzania