KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,600
Katika zama hizi za utandawazi, imekuwa ni ngumu sana kwa nchi za kiafrika kuendana na mabadiliko hayo ya utandawazi na hivyo kupelekea kujenga uchumi kuwa ni ngumu. Utandawazi unatumiwa na mabeberu kama njia mojawapo ya kuitawala tena Afrika kupitia teknolojia kutokana na kwamba nchi za Afrika zimekuwa zikishindwa kuendana na mabadiliko. Hali hii ya kushindwa kuendana na mabadiliko ya utandawazi inapelekea changamoto za mabadiliko katika nchi za kiafrika.
Tanzania kama moja ya nchi katika Afrika, kwa namna moja au nyingine tumeathirika sana na utandawazi. Kwa kipindi kirefu nchi za Afrika zimegeuzwa ‘dampo au gulio’ la bidhaa za kigeni kutokana na kukosa teknolojia ya kuzalisha hizo hizo bidhaa sisi wenyewe. Nchi za Afrika zimekuwa ni soko tu la wazalishaji na tumekuwa watumiaji. Utandawazi umeathiri sana uchumi wa Afrika.
Rais Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa ni sehemu ya wazalishaji na si kubaki kama soko la bidhaa za kigeni, akaja na wazo la TANZANIA YA VIWANDA. Hii ni moja ya silaha muhimu sana katika kuondokana na utandawazi na athari za kiuchumi katika nchi yetu zinzaotokana na utandawazi.
Utandawazi ulikuwa unafanya nchi yetu unakosa mapato makubwa ya madini kwa kuuza kwa bei ndogo madini ambayo hayajachakatwa lakini Rais Magufuli kaweza kukabiliana na hali hii kwa kuyachakata madini hayo hapahapa nchini ili kuyaongezea thamani. Hii ni jambo la kupongeza sana
Pia, utandawazi umetuathiri kiuchumi kwa sababu nchi ina rasilimali nyingi ila ziligeuka ‘ rasilimali bubu’ ila Rais Magufuli ameweza kuzibadili ili ziweze kuchangia maendeleo hii na katika kuondoa umasikini wa watu. Haya yote ni athari ambazo si tu Tanzania bali Afrika kwa ujumla inazipata kutokana na utandawazi.
Utandawazi umefanya uchumi wa nchi za afrika kumilikiwa na wawekezaji wa kigeni wenye viwanda vya kuzalisha bidhaa na watu wengine binafsi na hivyo kufanya uwiano katika ya masikini na matajiri kuwa mdogo na masikini kuongeza sana. Sehemu kubwa ya utajiri wa nchi unamilikiwa na wageni na hii ni mbaya kwa sababu wapo kwa ajili ya pesa tu bila kujali uzalendo kwa nchi.
Afrika imegeuzwa jalala la kila takataka ya kigeni kisa utandawazi. Vijana wanakesha kwenye mitandao ya kijamii wakifuatilia habari zisizowasaidia, tamaduni za ushoga na usagaji zimeingia afrika kisa utandawazi, nidhamu kupungua, uzalendo kushuka na mavazi yasiyofaa kwa watoto wa kike na wa kiume yote yakiwa ni matokeo hasi ya utandawazi. Utandawazi lazima uwe na kikomo ili kulinda utu, uchumi, siasa, mshikamano na Amani.