Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Unapuyanga,Magu alisema Mazao chini ya tani 1 hakuna kodi au ushuru sasa baba kajaribu kusafirisha gunia moja tuu utapata majibu kama ni kweli au sio kweli .Nyie si mnaishi kwa jasho letu ndio maana unatetea ushuziUelewa wa watu wengi wa Transformation ni mdogo ikiwemo mleta mada na wanao muunga mkono
1. Hakuna kodi isiyoeleweka zaidi ya kauli au dhana ya mleta mada, kwani ameshindwa kueleza ni kodi ipi isiyo eleweka ili aweze kueleweshwa.
2. Account kuwa frozen sio jambo geni na ndio maana Maneno hayo yapo hayakuanza wakati wa Nyerere au wakati wa Awamu hii ya Tano.
Na kama kuna Nchi ina freeze account ni USA ambayo imezui fedha nyingi sana Iran na za Venezuela, just to a mentioned a few e.g.
Na kuna sheria za kimataifa ktk usafirishaji wa pesa toka nchi moja kwenda nyingine, na hata ubadilishaji wa pesa wakati mwingine hufanyika ili kudhibiti mambo kama haya ya ukwepaji kodi na uhifadhi wa fedha zilizopatikana kwa njia zisizo faa kama matendo, madawa ya kuleta n.k.
3. Hakuna kodi ya kuku wawili wanaofugwa nyumbani for matumizi ya nyumbani, lakini kuna kodi zimewekwa kwa kufanya biashara mfano unauza kuku sokoni kuna kodi zake au uhuru wa soko n.k.
Na madhumuni yake ni watu wengi kadri inavyo wezekana wachangie maendeleo na utoaji wa huduma kwa watu wote waliopo Tanzania . Na sio kodi itoke kwa baadhi tu ya wananchi au tuseme wafanyakazi na wafanya biashara
4. Hakuna mara kile mara hiki , bali ni kuimarisha mifumo yetu ambayo ilikuwa dini kwa kutokuwa na wafanyakazi wa kutosha wenye weledi na matumizi mazuri ya technology yenye kuwezesha kupata taarifa sahihi za mtu/watu / vitu/ biashara n.k .
Vitu hivyo visipo fanyika ni huyu huyu mleta mada atalalamika kukosekana kwa waalimu, vyoo, thamani za shule vitu, ma desk n.k
Hivyo uwe na mchango endelevu ili Maisha ya watoto iwe bora zaidi. Fikiria future
Kuna kitu ambacho hukijui kuwa mfumo wa Maisha na kiuchumi aliyoweka Nyerere alijaribu kuweka system za UK,
Mfano vijiji vya ujamaa ilikuwa ni kama watu UK wanavyo ishi kwenye estate ambako kunawekwa social amenities hapo hapo ili kuleta tija ya matumizi ya huduma za kijamii, sasa wewe kwa uelewa wako mdogo hujui hilo, kingine ni uwazishwaji wa Board of Internal trade na kuwa na etc, bhesco,hosco ni sawa sawa na UK kuwa na hizo supermarket za chakula-RTC, vifaa vya ujenzi wickens, vyombo vya nyumbani Homebase n.k n.k .
Sasa wewe kwa kuwa uelewa wako mdogo huelewi, jingine ilikuwa ni kutoa ajira kwa watanzania kama wewe ili kupitia mashirika hayo upate exposure na uelewa wako use mkubwa na baadae ukienda kijijini kwenu unapeleka ulicho kiona kwenye nyumba za wafanyakazi au ma flat ya mashirika ya umma kijijini kwenu.
Sasa kutokana na uelewa wako mdogo wewe ulishindwa kuelewa hilo na Nyerere asingeweza kuwa kila sehemu.
Kuna kingine kwa sababu ya uelewa wako mdogo na no reserve kwa Sasa , mpaka uelewe nilicho kieleza hapo juu.
Hilo la account kuwa frozen, lipo kisheria na kama wewe unaona umeonewa unaweza kwenda mahakamani kudai account ifunguliwe na kudai fidia