Rais Magufuli anafukua Makaburi ya akili za watanzania, wengi mtaelewa hili 2025

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Wengi walijua ni mchanga angalau sasa wanajua ni makinikia ambayo baada ya muwekezaji kubanwa alisema ukweli yanamuingizia 50% ya kipato chake chote, Baada ya kubanwa zaidi alisema tangu yazuiwe makontena Kila siku anapoteza Bil 2 za kitanzania. Kabla ya hapo waliaminishwa ni michanga isiyo na cha maana.

Wengine wakisikika kupinga kuwa michanga huwa haisafirishwi wakati miaka yote inapita hapohapo dodoma kuelekea ughaibuni ....

Angalau sasa tunaelekea kufunguliwa bongo nini ni nini katika madini kutoka kwa Serikali, wakosoaji wake,muwekezaji,wachambuzi etc zamani ilikuwa ni malalamiko yasiyoelekea kwenye hitimisho.

Asante JPM kwa kufukua makaburi ya akili zetu

Nguli wa madawa ya kulevya aliyetikisa dunia Pablo Escobar aliwahi kuchoma mahakama, kukodi waasi kufanya mauaji, kufanya Kila unyama ili sheria ya yeye au wauza madawa wenzake wasipelekwe marekani maana kulikuwa na uwezekano 0% kutoroka au kuhonga.

Leo moja ya watuhumiwa wakubwa alihamishwa kutokea gereza la tanzania hadi marekani kitu ambacho huwa ni pigo kubwa kwa mtuhumiwa wa drugs popote ulimwenguni. Pablo Escobar alifananisha na kuwekwa kwenye kaburi la CHUMA(Iron TOMB) yenye uwezekano sufuri wa kutoroka. Yale yaliyokuwa tunadhani hayawezekani sasa yanawezekana.

Asante JPM kwa kufukua Makaburi ya Akili zetu

Ni aibu kupita sehemu kukuta kijiji kinalia njaa huku nyasi zimesitawi mashambani bila kuwepo na zao lolote. Angalau basi pawe na mazao kidogo yaliyokauka kama ushahidi kuwa kuna juhudi zilifanyika lakini mabadiliko ya hali ya hewa yalikuwa kikwazo.

Hapa alionekana katili lkn ukweli ni huo uko dhahiri. Anafungua bongo zetu kuwa kila mtu ajitume kwa kadili ya uwezo wake na akibaki kulalamika basi atakula matunda ya malalamiko yake. Leo ni kawaida kusikia dada mrembo young graduate akiulizia bei ya mbegu za tikiti wakati zamani angekaa sebuleni anaangalia TV hadi muujiza wa ajira utakapomdondokea.

Asante JPM kwa kufukua makaburi ya akili zetu.

Kuna watu walizoea kujenga majumba, kununua magari,kufanya kila aina ya anasa kwa pesa kwa misingi ya rushwa, ujanjaujanja, udaladalali, madilimadili, kukandamiza wasio nacho, dhuruma na uonevu. Angalau sasa kila mmoja anaanza kufikiri upya baada ya mianya hii kuhafifishwa kabisa.

Watu wengi wenye uwezo waliweka akili zao na uwezo wao kando na kujielekeza kwenye njia za mikato zisizohalali ili wanufaike. Leo angalau ni kinyume.

Kila maamuzi yana madhara yake, na wenda matatizo yanayoonekana sasa ktk biashara baada ya muda yatapita tunaamini mambo yatakuwa sawa.

Asante JPM kwa Kufukua Makaburi ya Akili zetu
 
Hiyo kuhusu kulima, hata mimi amenifumbua sana macho.
Mwaka mzima unaisha, mtu anaishi pembezoni mwa mto hajapanda hata mpapai halafu anataka msaada wa serikali wa vitu ambavyo angevipata kwenye matunda...
Hata kama ningekuwa mimi, bakora tu ili akili zirudi kwenye defaultmode...
 
Kabla ya kuondoa privileges za marais hajafukua makaburi bado.

Labda kafagia juu juu tu.
 
Kabla ya kuondoa privileges za marais hajafukua makaburi bado.

Labda kafagia juu juu tu.
ndio maana nimekuwa specific kwa aina ya makaburi.
Watanzania wote wakiwa conscious na kinachoendelea nchini na duniani kwa ujumla makaburi hayo yatajifukua automatically. hata wanasiasa itabidi wajiadjust kwenye facts maana watakoswa wafuasi wakufuata mikumbo na kununulika kwa chumvi na wali maarage. Hata ulaya walianza na Enlightenment ndio mambo mengine tunayowasifia yakafuata.
mkuu anatufungua akili tuwaze kitofauti.
 
ndio maana nimekuwa specific kwa aina ya makaburi.
Watanzania wote wakiwa conscious na kinachoendelea nchini na duniani kwa ujumla makaburi hayo yatajifukua automatically. Hata ulaya walianza na Enlightenment ndio mambo mengine tunayowasifia yakafuata.
mkuu anatufungua akili tuwaze kitofauti.
Enlightenment hairuhusu double standards.
 
Enlightenment hairuhusu double standards.
Inaanza enlignment kwa watu wote ndio doublestandard(Kama ipo) itaondoka kwa kudumu. Double standard(KAma ipo) ikiondolewa kabla ya citizen's enlightenment itakuwa ni temporary.
Kufunguka kiakili kwa kila mtanzania na kujua uhalisia wa kinachoendelea ndio msingi wa yote hayo kutokuwepo kwa kudumu.
 
Inaanza enlignment kwa watu wote ndio doublestandard(Kama ipo) itaondoka kwa kudumu. Double standard(KAma ipo) ikiondolewa kabla ya citizen's enlightenment itakuwa ni temporary.
Kufunguka kiakili kwa kila mtanzania na kujua uhalisia wa kinachoendelea ndio msingi wa yote hayo kutokuwepo kwa kudumu.
Kila Mtanzania?

For real?

Si kila siku tutasubiri Watanzania wapya wanaozaliwa waelimike ili tuweze kufanya chochote?
 
Hayo unayoyaita makaburi ni nani aliyachimba na kufukia akili zako huko?
 
Hizi ni ngonjera tu kama zingine ambazo tumekuwa tunalishwa. Vita yeyote lazima iwe na mikakati na mbinu. Nia njema kutokaka moyoni haiwezi kusaidia chochote katika mapambano. Tujipe muda kidogo turudi kwenye historia ya mapambano, tuanganie waasisi walitupa wosia gani na tusome classics ili tujue wanzuoni walisema nini kuhusu mambo mbalimbali kabla hatujakurupuka. It is not possible to invent the wheel.
 
Back
Top Bottom