Rais Magufuli anafaa kuwa rais wa Africa

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Kwa kuwa rais wa dunia ni Trump wa Marekani ni wakati muafaka sasa Afrika nayo iwe na kiongozi wake ili kuwa na sauti ya pamoja katika masuala yenye maslahi mapana na bara hilo ndani na nje ya mipaka yake. Nkwame Nkrumah angekuwepo au Nyerere au mzee Madiba angechukua mikoba ila kazi ya Mungu haina makosa.

Naomba kutoa hoja ndugu zangu, kwa kuzingatia kazi aliyoifanya kwa mwaka huu mmoja tangu awe rais wa Tanzania, imetosha kabisa kumpima kuujua moyo wake, utendaji wake, msimamo wake na uwezo wake mkubwa wa kiuongozi na kiutendaji. Ona alivyotumbua majipu, ona alivyoikomesha rushwa, ona alivyowanyoosha watumishi wa umma waliokuwa miungu watu maofisini.

Natoa hoja tena. Rais Magufuli achaguliwe kuwa rais wa Afrika tuondoke kuwa bara la giza.

Nawasilisha.
 
AFRIKA..!! kwa misingi ipi..? na siasa ipi ya chama chake au..?
waafrika tulivyo bora tubaki na utawala wa kinchi tu huko bado bara lote litachafuka hasa na mtu uliempendekeza kuwa na kauli za kibabe
 
Kwa wengi watakaochangia hapa naamini hawataunga mkono hoja kwa kuwa ni sehemu ya waathirika wa maamuzi magumu yanayofanywa na Le Prof: John Pombe Magufuli. Hivyo basi kwa sisi tunaojitambua kuhusu Africa tunakubaliana na mtoa mada kuwa Africa inamuhitaji rais sampuli ya Magufuli na siyo vibaraka kama akina nanihiii na akina waleee...

Magufuli is a true man of Africa.
 
KAMA ILIVYO MAREKANI NI KIRANJA WA DUNIA, TANZANIA NAYO NI KIRANJA WA AFRIKA SO NI LAZIMA MAGUFULI ADIKTETI TERMS, CONDITION AND REFFERENCE ZA BARA HILI
 
Nawaomba nyie makada wa ccm mumshauri ili ajipime kuwa kama kweli anakubalka kwa watanzania aweke tume huru ya uchaguzi ili tulijuze bara LA Africa kuwa ata akishindanishwa na zito kabwe kuwa asubuhi tu bara la Africa litajua Uyo jamaa anakubalika kwa asilimia chini ya 20 ya watanzania wote.

Mjiongeze sababu za ccm na uyo naye pia kuiogopa tume huru ya uchaguzi..... ni kuogopa kushindwa vibaya kwa aibu
 
Kwa kuwa rais wa dunia ni Trump wa Marekani ni wakati muafaka sasa Afrika nayo iwe na kiongozi wake ili kuwa na sauti ya pamoja katika masuala yenye maslahi mapana na bara hilo ndani na nje ya mipaka yake. Nkwame Nkrumah angekuwepo au Nyerere au mzee Madiba angechukua mikoba ila kazi ya Mungu haina makosa.

Naomba kutoa hoja ndugu zangu, kwa kuzingatia kazi aliyoifanya kwa mwaka huu mmoja tangu awe rais wa Tanzania, imetosha kabisa kumpima kuujua moyo wake, utendaji wake, msimamo wake na uwezo wake mkubwa wa kiuongozi na kiutendaji. Ona alivyotumbua majipu, ona alivyoikomesha rushwa, ona alivyowanyoosha watumishi wa umma waliokuwa miungu watu maofisini.

Natoa hoja tena. Rais Magufuli achaguliwe kuwa rais wa Afrika tuondoke kuwa bara la giza.

Nawasilisha.
Nchi kuwa na watu wenye mawazo km yako ni MKOSI MKUU, Tanzania tuna mkosi sana
 
Mwambie labda Africa ya chato n kolomije mtu ana PHD ya magumashi hata kuongea kimombo dk 5 jasho linajaa upara wote
 
Angalia jinsi anavyo ongoza familia yake.... alafu angalia kama ataweza kuongoza africa?
 
Back
Top Bottom