Rais Magufuli ana maoni makubwa na nchi hii, tatizo ni kauli zake na ukosefu wa mbinu za kiuongozi

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,019
3,877
Wanajamvi habari za wakati huu,

Kabla ya kuendele niseme tu huu ni mtazamo wangu binafsi.

Nimefuatilia kwa muda sasa hatua zinazochukuliwa na mtukufu Rais wetu na nimeona niseme tu hatua anazochukua zinaonesha,uzalendo wa kweli,nia ya dhati na hamasa ya kipekee katika utendaji kazi wake.

Rais Magufuli ana nia ya dhati ya kujenga taifa imara hilo halina mjadala ila tatizo ni hili;

1. Lack fo leadership skills (Ukosefu wa mbinu za kiuongozi)

Kwa wale wataalum wa uongozi mtakubaliana nami kwamba 'a leader is as strong as his team'kipimo cha kwanza cha kiongozi ni namna anavyopanga timu yake na katika hilo rais wetu ameshindwa kabisa.Ninaposema kashindwa simaanishi kuwa viongozi anaowateua ni wabovu!hapana!namaanisha hajawapanga vizuri.

Nitoe mfano wa sakata la Mwakyembe, Nape na hili la Muhongo hawa ni sehemu ya viongozi wenzake ukiangalia hatua alizozichukua na mazingira yaliyopelekea kuchukua hatua hizo unachoona ni Kiongozi ambaye anahitaji kuwekwa katika maombi kwani badala ya kujenga timu yake ya kila siku anabomoa tu. Kama kiongozi mkuu wa nchi huwezi kuwa unafukuza wateule wako kila mara kwa maswala ambayo zaidi mngetakiwa kuchukua collective responsibility na kuyasemea kama serikali badala ya kutoana kafara.

2. Tabia ya kauli za rais kugeuzwa sheria bila kupitishwa bungeni.

Kauli za rais zinapogeuzwa kuwa sheria bila kufanyiwa scrutiny huwa zinaleta shida sana kwenye utekelezaji na kwa kanchi ketu haka ambako viongozi wengi ni waoga ni rahisi sana watu kufanya maamuzi ya kijinga ambayo hayajengi kwa sababu Rais kasema bila kutafakari kwa kina.

Nimwombe tu rais wetu akae na viongozi wake awambie anataka wafanyeje kazi asiseme hapa kazi tu bila kuwapa mwongozo kama anaona hilo gumu basi nimuombe kazi ya kuwa biographer wake nizunguke naye kisha nimetengenezee manifesto ambayo watu wakisoma wataweza kujua anataka nini. Hakuna haja ya Mkuu wa nchi kuongoza nchi bila kuwa na personal manifesto tena ukichangia kuwa kanchi kitu ni kachanga sana na kanihitaji kiongozi kuwa na maono ya muda mrefu.

Ni hayo tu kwa leo tujadili.

Wasalaam.
 
Hii awamu mambo mengine inabidi yakae pembeni, ameamua kusafisha. Ma pale anaona mty hafai ni aende tu, haya ya kukaa na hao hao eti unajenga timu huku wana madudu yao na anayagundua sifikiri kama ni vyema...bora aondoe majipu wakae pembeni na wengine wanaopenda kazi na mstari ulionyooka wafanye nae kazi.

Tabu ni mazoea, ila itazoeleka tu.

Hapa kazi tu
 
Naheshimu maoni yako.

Lakini kama Taifa tunahitaji Katiba Mpya. Katiba nzuri itatupa kiongozi/viongozi wazuri. Tunahitaji mjadala na makubaliano kama Taifa kuhusu mambo yote muhimu mfano:-

1) Maono (vision) yetu kuhusu uchumi, elimu, afya, kilimo nk nk

2) Falsafa yetu kama nchi ni ipi? Ujamaa ulishindwa na kupitwa na wakati, lakini sisi pia sio mabepari je sisi ni akina nani hasa?

3) Muundo wa Serikali ya JMT unahitaji mabadiliko makubwa. Sambamba na mabadiliko chanya kwenye taasisi zote za Serikali na mimihimili mfano Polisi, Mahakama, Bunge nk

Nia ni sehemu tu ya hitaji la msingi kama Taifa.
 
Nchi aiwezi kungozwa kwa maono bali kwa mipango iliyo jadiliwa kwa uwazi na kuhusisha wadau.

Pili kiongozi yeyote wa CCM hawezi kuwa na nia njema kama huko nyuma aliyaona maovu na akakaa kimya. Mtu wa namna hiyo ni mtu anaye ngojea zamu yake ya kuchuma
 
Pili kiongozi yeyote wa CCM hawezi kuwa na nia njema kama huko nyuma aliyaona maovu na akakaa kimya. Mtu wa namna hiyo ni mtu anaye ngojea zamu yake ya kuchuma[/QUOT

Umesema vyema
 
Tatizo ni Elimu yake na PHD hewa

Swissme​
R.I.P Mzee ndesa....... labda ndo utafurahi manake hakunaga mawazo huwa ya na kufanya japo kidogo uwe mzalendo.kila kitu kila siku ni kuwa against na serikali as if hakuna jambo hata moja la maana linalofanywa...what an idiot
 
Naheshimu maoni yako.

Lakini kama Taifa tunahitaji Katiba Mpya. Katiba nzuri itatupa kiongozi/viongozi wazuri. Tunahitaji mjadala na makubaliano kama Taifa kuhusu mambo yote muhimu mfano:-

1) Maono (vision) yetu kuhusu uchumi, elimu, afya, kilimo nk nk

2) Falsafa yetu kama nchi ni ipi? Ujamaa ulishindwa na kupitwa na wakati, lakini sisi pia sio mabepari je sisi ni akina nani hasa?

3) Muundo wa Serikali ya JMT unahitaji mabadiliko makubwa. Sambamba na mabadiliko chanya kwenye taasisi zote za Serikali na mimihimili mfano Polisi, Mahakama, Bunge nk

Nia ni sehemu tu ya hitaji la msingi kama Taifa.
Tunataka katiba lakini na maendeleo pia tunataka pia.Hatutaki abdakadabra za kutumbua majibu na kutuachia vidonda
 
Wanajamvi habari za wakati huu,

Kabla ya kuendele niseme tu huu ni mtazamo wangu binafsi.

Nimefuatilia kwa muda sasa hatua zinazochukuliwa na mtukufu Rais wetu na nimeona niseme tu hatua anazochukua zinaonesha,uzalendo wa kweli,nia ya dhati na hamasa ya kipekee katika utendaji kazi wake.

Rais Magufuli ana nia ya dhati ya kujenga taifa imara hilo halina mjadala ila tatizo ni hili;

1. Lack fo leadership skills (Ukosefu wa mbinu za kiuongozi)

Kwa wale wataalum wa uongozi mtakubaliana nami kwamba 'a leader is as strong as his team'kipimo cha kwanza cha kiongozi ni namna anavyopanga timu yake na katika hilo rais wetu ameshindwa kabisa.Ninaposema kashindwa simaanishi kuwa viongozi anaowateua ni wabovu!hapana!namaanisha hajawapanga vizuri.

Nitoe mfano wa sakata la Mwakyembe, Nape na hili la Muhongo hawa ni sehemu ya viongozi wenzake ukiangalia hatua alizozichukua na mazingira yaliyopelekea kuchukua hatua hizo unachoona ni Kiongozi ambaye anahitaji kuwekwa katika maombi kwani badala ya kujenga timu yake ya kila siku anabomoa tu. Kama kiongozi mkuu wa nchi huwezi kuwa unafukuza wateule wako kila mara kwa maswala ambayo zaidi mngetakiwa kuchukua collective responsibility na kuyasemea kama serikali badala ya kutoana kafara.

2. Tabia ya kauli za rais kugeuzwa sheria bila kupitishwa bungeni.

Kauli za rais zinapogeuzwa kuwa sheria bila kufanyiwa scrutiny huwa zinaleta shida sana kwenye utekelezaji na kwa kanchi ketu haka ambako viongozi wengi ni waoga ni rahisi sana watu kufanya maamuzi ya kijinga ambayo hayajengi kwa sababu Rais kasema bila kutafakari kwa kina.

Nimwombe tu rais wetu akae na viongozi wake awambie anataka wafanyeje kazi asiseme hapa kazi tu bila kuwapa mwongozo kama anaona hilo gumu basi nimuombe kazi ya kuwa biographer wake nizunguke naye kisha nimetengenezee manifesto ambayo watu wakisoma wataweza kujua anataka nini. Hakuna haja ya Mkuu wa nchi kuongoza nchi bila kuwa na personal manifesto tena ukichangia kuwa kanchi kitu ni kachanga sana na kanihitaji kiongozi kuwa na maono ya muda mrefu.

Ni hayo tu kwa leo tujadili.

Wasalaam.
Nimekuelewa mkuu Walio wengi ni wagumu wa kuelewa wana akili za kuvukia barabara ndiyo maana wanatoka mapovu Wamezoe kufungwa na kufunguliwa midomo
 
R.I.P Mzee ndesa....... labda ndo utafurahi manake hakunaga mawazo huwa ya na kufanya japo kidogo uwe mzalendo.kila kitu kila siku ni kuwa against na serikali as if hakuna jambo hata moja la maana linalofanywa...what an idiot
Punguza povu,hilo la PHD watajua waliompa.Kwetu sisi yeye ni Rais PHD or no PHD tunataka tuone mambo yanaenda vyema
 
Nimekuelewa mkuu Walio wengi ni wagumu wa kuelewa wana akili za kuvukia barabara ndiyo maana wanatoka mapovu Wamezoe kufungwa na kufunguliwa midomo
Tuko Pamoja sisi ni wajenzi wa nyumba moja hakuna haja ya kugombea fito tukosoane na kuambiana ukweli ili nchi isonge mbele
 
Nchi aiwezi kungozwa kwa maono bali kwa mipango iliyo jadiliwa kwa uwazi na kuhusisha wadau.

Pili kiongozi yeyote wa CCM hawezi kuwa na nia njema kama huko nyuma aliyaona maovu na akakaa kimya. Mtu wa namna hiyo ni mtu anaye ngojea zamu yake ya kuchuma
Ndugu yangu uko sawa tatizo povu.Sote tulikuwepo na hatukuchukua hatua na hata sasa tupo na hatuchukui hatua kwa hiyo sio swala la CCM au nani ni swala la Taifa kwa ujumla kama tunataka uwazi basi tudai uwazi nasio kukejeli jitihada.Mimi bianafsi nafikiri yapasa zaidi kuhoji kwa hoja.Maona na Mipango huenda pamoja na siwa na mimba inahitaji mume na mke ili ikamilike.Maono anayo mipango pia anayo tatizo ni leadership qualities
 
Sio povu bali ni kusema ukweli. Kuhusu kuchukua hatua watu wengi kasoro CCM walichukua hatua. Watu wameongelea sana kuhusu kuweka mikataba wazi na kuwa na mijadala ya kutosha ila CCM wakalazimisha kwa kuzima mijadala na kutumia hati za zarura kupitisha na kuhalalisha wizi. Sasa huyo mwenye maono hakuwa na maono kipindi hicho cha hati za zarura?. Nazani hatasheria zinatambua mtu aliekaa kimya akiona uhalifu unafanyika na yeye pia ni mualifu.
 
Hii awamu mambo mengine inabidi yakae pembeni, ameamua kusafisha. Ma pale anaona mty hafai ni aende tu, haya ya kukaa na hao hao eti unajenga timu huku wana madudu yao na anayagundua sifikiri kama ni vyema...bora aondoe majipu wakae pembeni na wengine wanaopenda kazi na mstari ulionyooka wafanye nae kazi.

Tabu ni mazoea, ila itazoeleka tu.

Hapa kazi tu
Sasa akitumbua si bila mpango si atatuachia vidonda vyenye usaha.Nafikiri tatizo ni namna ambavyo wanawekwa pembeni.Inaonekana zaidi ni swala la mkuu kutotaka kuwasikiliza viongozi hawa
 
Sio povu bali ni kusema ukweli. Kuhusu kuchukua hatua watu wengi kasoro CCM walichukua hatua. Watu wameongelea sana kuhusu kuweka mikataba wazi na kuwa na mijadala ya kutosha ila CCM wakalazimisha kwa kuzima mijadala na kutumia hati za zarura kupitisha na kuhalalisha wizi. Sasa huyo mwenye maono hakuwa na maono kipindi hicho cha hati za zarura?. Nazani hatasheria zinatambua mtu aliekaa kimya akiona uhalifu unafanyika na yeye pia ni mualifu.
Hapo sawa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom