ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,138
- 4,153
Wanajamvi habari za wakati huu,
Kabla ya kuendele niseme tu huu ni mtazamo wangu binafsi.
Nimefuatilia kwa muda sasa hatua zinazochukuliwa na mtukufu Rais wetu na nimeona niseme tu hatua anazochukua zinaonesha,uzalendo wa kweli,nia ya dhati na hamasa ya kipekee katika utendaji kazi wake.
Rais Magufuli ana nia ya dhati ya kujenga taifa imara hilo halina mjadala ila tatizo ni hili;
1. Lack fo leadership skills (Ukosefu wa mbinu za kiuongozi)
Kwa wale wataalum wa uongozi mtakubaliana nami kwamba 'a leader is as strong as his team'kipimo cha kwanza cha kiongozi ni namna anavyopanga timu yake na katika hilo rais wetu ameshindwa kabisa.Ninaposema kashindwa simaanishi kuwa viongozi anaowateua ni wabovu!hapana!namaanisha hajawapanga vizuri.
Nitoe mfano wa sakata la Mwakyembe, Nape na hili la Muhongo hawa ni sehemu ya viongozi wenzake ukiangalia hatua alizozichukua na mazingira yaliyopelekea kuchukua hatua hizo unachoona ni Kiongozi ambaye anahitaji kuwekwa katika maombi kwani badala ya kujenga timu yake ya kila siku anabomoa tu. Kama kiongozi mkuu wa nchi huwezi kuwa unafukuza wateule wako kila mara kwa maswala ambayo zaidi mngetakiwa kuchukua collective responsibility na kuyasemea kama serikali badala ya kutoana kafara.
2. Tabia ya kauli za rais kugeuzwa sheria bila kupitishwa bungeni.
Kauli za rais zinapogeuzwa kuwa sheria bila kufanyiwa scrutiny huwa zinaleta shida sana kwenye utekelezaji na kwa kanchi ketu haka ambako viongozi wengi ni waoga ni rahisi sana watu kufanya maamuzi ya kijinga ambayo hayajengi kwa sababu Rais kasema bila kutafakari kwa kina.
Nimwombe tu rais wetu akae na viongozi wake awambie anataka wafanyeje kazi asiseme hapa kazi tu bila kuwapa mwongozo kama anaona hilo gumu basi nimuombe kazi ya kuwa biographer wake nizunguke naye kisha nimetengenezee manifesto ambayo watu wakisoma wataweza kujua anataka nini. Hakuna haja ya Mkuu wa nchi kuongoza nchi bila kuwa na personal manifesto tena ukichangia kuwa kanchi kitu ni kachanga sana na kanihitaji kiongozi kuwa na maono ya muda mrefu.
Ni hayo tu kwa leo tujadili.
Wasalaam.