Rais Magufuli ana kazi ya kumtafuta Lissu wa kipindi cha Uchaguzi ili kuyaelewa haya

Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
386
517
Niwazi kampeni zimeisha na Rais Dr. JPM amechukua ofisi kwa awamu ya pili, sasa kinachofuata ni utekelezaji wa Illani ya CCM.

Pamoja na ukweli kwamba ilani inayotekelezwa ni ya CCM lkn tumejifunza kuwa kuna mambo ambayo hayakuibuliwa ndani ya ilani ya CCM na yameibuliwa ndani ya ilani ya CHADEMA na mara nyingi yale ya msingi tulipata impact moja kwa moja kwa JPM naye kujaribu kuyajibu au kuyanakili(copy) kwa sababu kweli yanagusa maisha marefu ya taifa lolote.

Hivyo, jampo kampeni zimeisha Lissu bado hajaisha na anahehitaji kumtafuta zaidi nakumwelewa ni mimi na ww zaidi sana JPM, embu tuyatazame yafuatayo katika kumtafuta Lissu wa wakati wa Kampeni:

Kwanza; Aliahidi kufumua mfumo wa Elimu na kusuka upya
Hapa tunahitaji kupata mawazo yake alimaanisha nn katika elimu yetu na kunadosari zipi katika mfumo wa utoaji elimu. Naamini JF kuna wabobezi wengi wa masuala mbalimbali naombeni tulijadili kwa kwa maslahi ya nchi.

Pili, Bima ya Afya kwa wote
Lissu alimaanisha nini? Na angewezaje kulitekeleza hili? Na kama kweli hii ndiyo mifumo inayotumika hasa huku katika nchi za wenzetu na imeonesha mafanikio basi itakuwa vyema na sisi tukajifunza toka kwao kwa kuzingatia mazingira yetu,katika hili Lissu wa wakati wakampeni bado hajaisha.

Tatu: Mfumo wa Kodi
katika mifumo ya kodi aliainisha kodi ambazo hazina ustawi kwa wakulima wadogo na wafanya biashara akaahidi atazifuta.

JPM ana lakujifunza kwamba hivi huyu Lissu alimaanisha nn, au aliona nn. Na bila kodi hauwezi endesha nchi, Je huyu Lissu alikuwa na maana gani? Yaani tupate mawazo yake “idea” zake. Najua wataalam wa kodi na maswala ya biasha hapa JF wapo kama mlimwelewa Lissu tujadili hoja yake hii.

Ningependa kwa leo tumtafute Lissu wa kampeni katika hayo mambo matatu hapo juu maana ni msingi wa maendeleo ya nchi yeyote.

Elimu, Afya na Kazi
 
Kumbuka pale Lissu hakukulenga wewe mwenye uwezo wa kuchambua hivi hoja.

Alilenga wanainchi wa mkalama, Nkoye, Mpigamiti, Nkudumba na Chanjanachui.

Wanasiasa wote huwa wanaamini wanaowasikiliza ni zero brain.
 
Lissu hakuwa na jipya kila alilolopoka CCM inalifahamu sana na lipo kwenye mipango yake.
 
Hoja yako mleta mada ni nzuri sana ila ngoja yaje yale matakataka ya CCM uone uharo wao. Kama tungekua na TISS nzuri yenye akili wangeifanyia kazi. Ila kwa hii iliyopo wana shida kunyang’anyana malaya na barmaids pale Four ways na Breakpoint. Tulia tu.
 
Lissu hakuwa na jipya kila alilolopoka CCM inalifahamu sana na lipo kwenye mipango yake
Kila binadamu ana jambo lakufikirisha katika maongezi yake, JF imejengwa katika msingi wakuzama kwenye fikra nakujenga hoja.
 
Hoja yako mleta mada ni nzuri sana ila ngoja yaje yale matakataka ya CCM uone uharo wao. Kama tungekua na TISS nzuri yenye akili wangeifanyia kazi. Ila kwa hii iliyopo wana shida kunyang’anyana malaya na barmaids pale Four ways na Breakpoint. Tulia tu.

Mkuu umeua asee!
 
Lisu hana utalaam wowote kuhusiana na hizo zingine ulizo zingumzia hapo zaidi ya vifungu vya sheria na haki za binadamu. Naomba hii kauli ieleweke.
 
Back
Top Bottom