Rais Magufuli amualika Rais wa Zambia kwa ziara ya siku 3

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Rais John Pombe Magufuli amemwalika Rais wa Jamhuri ya Zambia, Edgar Lungu kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Novemba 27 hadi 29, 2016.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga amesema katika ziara ya rais Lungu atatembelea vitengo na sehemu muhimu zinazounganisha nchi ya Tanzania na Zambia kiuchumi.

“Rais Edgar Lungu amealikwa na Dk. Magufuli kutembelea nchini kuanzia Jumapili ya Novemba 27 hadi 29, 2016. Katika ziara yake atatembelea vitengo na sehemu mumihu vinavyounganisha nchi na Zambia kiuchumi ikiwa ni pamoja reli ya Tazara,” amesema.

Ametaja sehemu nyingine atakazotembelea Rais Lungu kuwa ni Bandari ya Dar es Salaam, na kituo cha mizigo kinachohifadhi mizigo inayokwenda Zambia kabla ya kwenda bandarini.

“Siku ya mwisho ya ziara yake, atembelea bandari ya DSM kabla ya kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi nchini kwake,” amesema.

Aidha, Mahiga amesema Rais Lungu na Magafuli watasaini baadhi ya mikataba ikiwemo ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara ) ili kulifufua shirika hilo.

Chanzo:
Dewj Blog
 
Hata awaite hawarudi tena kutumia bandari ya Dar es Salaam bandari wanayotumia sasa ya Beira hainaga mikodi ya ajabu..Kamuomba Kagame warudi ziiii kamwita Kabila ziiii Kaenda kwa Museveni ziiiiiiii sasa kwa Wazambia.. Kitu ambacho hakijui bwana yule ni kwamba wanasiasa sio wanaowaamulia wafanya biashara wapitishe mizigo yao wapi..wafanyabishara wanakwenda wanapovuna faida
 
Kaamua kuwa afisa masoko wa bandari.

Tatizo la nchi ni mifumo,systems.

Bandari ijiendeshe kibiashara,iwe na watu wa.masoko wanaojua kazi yao.

ikishindikana aje huku bariadi achukue ndagu
 
Hata awaite hawarudi tena kutumia bandari ya Dar es Salaam bandari wanayotumia sasa ya Beira hainaga mikodi ya ajabu..Kamuomba Kagame warudi ziiii kamwita Kabila ziiii Kaenda kwa Museveni ziiiiiiii sasa kwa Wazambia.. Kitu ambacho hakijui bwana yule ni kwamba wanasiasa sio wanaowaamulia wafanya biashara wapitishe mizigo yao wapi..wafanyabishara wanakwenda wanapovuna faida
Mwache afanye kazi yake ..watarudi ama kutokurudi wanajua wao
 
Kikwete hakusubiri waje ndio auze. Aliwafuata wateja huko. Kuna haja ya kuangalia utitiri wa kodi na kejeli kwa wafanyabiashara. Pale Tunduma watu hutumia siku nyingi kuvuka mpaka.
 
Tazara iko hoi,kila siku wafanyakazi wanagoma,hawajalipwa mishahara,halafu eti wafanyabiashara wa zambia waje huku!

Bora angekikutanisha chama cha wafanyabiashara wa zambia na mamlaka za Tanzania kama TRA,Bandari,uhamiaji,Tazara ili wajue shida iko wapi.

Kukutana na wanasiasa haisaidii
 
..Zambia wanatumia bandari na reli za Angola.

..Angola wamejenga upya reli yao toka bandari ya Lobito mpaka kwenye mpaka na Zambia.

..kama tunataka kushindana na Angola ktk biashara ya kusafirisha mizigo ya Zambia basi tunapaswa tujizatiti kwelikweli.
 
Kikwete hakusubiri waje ndio auze. Aliwafuata wateja huko. Kuna haja ya kuangalia utitiri wa kodi na kejeli kwa wafanyabiashara. Pale Tunduma watu hutumia siku nyingi kuvuka mpaka.
kweli kabisa mkuu,kejeli na kutukanwa.

Bandari imekuwa kama eneo lililotangazwa hali ya hatari na magaidi wanasakwa,harrassment,hakuna business language,ubabe tu,kodi zinabambikwa.
 
Bado kuna bandari imara kama Beira,msumbiji wamekaba gepu,

South Afrika nao wana bandari,imekaba gepu

kule kuna mombasa haina longolongo

hahahaa
 
Kweli
Hapa tunaangalia wale wenye faida nasi .
Rais ana jenga urafiki wakibiashara zaidi
Pongezi kwako
 
Ni wakati muafaka kwa Mh Rais kutafakari kauli zake. Sisi Watanzania hatuna pa kusemea maana ndio nchi. Tumeambiwa tuishi kama mashetani. Wale hawawezi kukubali hali hii.
Kumuita Rais na kumuonyesha Bandari haitoshi. Waende watu kule wakafanye marketing. Wakutane na wadau wa Bandari. Serikali iwe tayari kukubali kutoa incentives.
Kauli za kibabe zifike ukomo.
 
Bado kuna bandari imara kama Beira,msumbiji wamekaba gepu,

South Afrika nao wana bandari,imekaba gepu

kule kuna mombasa haina longolongo

hahahaa
Jidanganyeni kwenye mitandao. Njoo hapa Tunduma uangalie Malori yanayovuka kwa siku pamoja na utitiri wa yad za malori zilivyojaaa
 
Hata awaite hawarudi tena kutumia bandari ya Dar es Salaam bandari wanayotumia sasa ya Beira hainaga mikodi ya ajabu..Kamuomba Kagame warudi ziiii kamwita Kabila ziiii Kaenda kwa Museveni ziiiiiiii sasa kwa Wazambia.. Kitu ambacho hakijui bwana yule ni kwamba wanasiasa sio wanaowaamulia wafanya biashara wapitishe mizigo yao wapi..wafanyabishara wanakwenda wanapovuna faida
Tatizo fikra zako umewaachia wanasiasa wazitumia kama wanavyopenda na kwa sasa unapiga kelele tu kama ndege angani.

Hufahamu kama ziara za Rais huwa zinaambatana na wafanyabiashara wakubwa wa nchi.

Hufahamu kama ziara za Rais huwa ni fursa ya wafanyabiashara kukutana na kubadilisha mawazo ya kibiashara.

Hufahamu kama kwa siku tatu kuna wamiliki wa hotel watakuwa na furaha kwa mapato yatokanayo na ziara ya Rais.

Umefanya utafiti gani ugagundua kama ziara za marais wa Rwanda, DRC zimekuwa ziii?

Siku hizi ujinga hapa Jamiiforums umekuwa ujanga, hekima na busara!
 
kwanza katafute wenye maarifa afu uwaulize ziara ya kualikwa gharama analipa nani?ukipata jibu ndio urudi tena tuanze kujadiliana.. kuhusu wafanyabiashara wa DRC na Rwanda kuikacha bandari hadi sasa hilo kaulize kamati ya bunge iliyotembelea pale na taarifa yao kwa vyombo vya habari.. Kama Bakharesa mwenyeji anashusha mizigo yake Beira ni mfanyabishara gani kichaa kutoka nje atapitisha mzigo pale?
Usilete siasa kwenye uchumi.. tunajua usiyoyajua
 
Ungekuwa na maarifa ungefahamu vizuri hoja yangu lakini ninachokisoma kwa sasa ni pumba tupu.

Kwa hiyo Bakharesa unashusha mizigo Beira na kuipeleka wapi? Au unadhani anaingiza nchini bure?

Eti nisilete siasa kwenye uchumi. Nani alikudanganya siasa sio msingi wa uchumi. Hufahamu kuwa sheria za kiuchumi zinatungwa na wanasiasa. Ndio maana nimekuambia akili zako kama timamu umewaachia wanasiasa na unachoandika hapa ni pumba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom