Rais Magufuli amtumbua Naibu Waziri Suzan Kolimba, Dkt. Ndumbaro aula

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Dkt Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma anachukua nafasi ya Dkt. Susan Alphonce Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushitikiano wa Afrika Mashariki.

Dkt. Mnyepe anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Prof. Mkenda amechukua nafasi ya Mej. Jen. Mstaafu Gaudence Miami ambaye amestaafu.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 26 Septemba, 2018 na tarehe ya kuapishwa kwao itatangazwa baadaye.

Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,

IKULU Dar es Salaam

26 Septemba, 2018
d5669fcd-8772-4870-919c-a2e9577d235e.jpg
 
Back
Top Bottom