figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Rais Magufuli ateua wenyeviti 5 wa bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa.
Mara kwanza Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli kuongoza bodi ya Parole Julai16, 2016, na muda wake kuisha Julai 16, 2019 baada ya kutimiza kipindi cha miaka mitatu cha kuongoza bodi hiyo. Na leo 20 January 2020 amemteua tena. Hongera kwa Mrema. Mrema ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani cha TLP.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Jumatatu Januari 20, 2020 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema wenyeviti hao wameongezewa muda baada ya vipindi vyao vya awali kumalizika;
Pili, Rais Magufuli amemteua Dk Harun Ramadhani Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).
Uteuzi wa Mrema na Dk Kondo umeanza Januari 20, 2020.
Tatu, Rais Magufuli amemteua Profesa Mayunga Habibu Hemed Nkunya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).
Nne, Rais Magufuli amemteua Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa Mipango na Matumizi ya Ardhi.
Tano, Rais Magufuli amemteua Peter Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Uteuzi wa Profesa Nkunya, Mutakyamilwa na Maduki umeanza Januari 17, 2020.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dk Noel Logwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa. Uteuzi wa Dk Logwa umeanza Januari 17, 2020 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Akiolojia na Mafunzo ya Urithi (Archeology and Heritage Studies) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Dk Logwa amechukua nafasi ya Profesa Audax Mabula ambaye amestaafu.
Pia soma:
1). Augustine Mrema aitaka Serikali kumlipa Tsh. Bilioni 2 kwa kusingiziwa kesi katika Serikali ya awamu ya tatu
2). Video: Halmashauri kuu ya TLP yampitisha Dr. John Magufuli kuwa Mgombea Urais 2020
3). Lyatonga Mrema: CCM wamenichezea rafu Uchaguzi Serikali za Mitaa, aonya