Rais Magufuli amteua tena Lyatonga Mrema kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Parole

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
Rais Magufuli ateua wenyeviti 5 wa bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa.

Mara kwanza Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli kuongoza bodi ya Parole Julai16, 2016, na muda wake kuisha Julai 16, 2019 baada ya kutimiza kipindi cha miaka mitatu cha kuongoza bodi hiyo. Na leo 20 January 2020 amemteua tena. Hongera kwa Mrema. Mrema ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani cha TLP.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Jumatatu Januari 20, 2020 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema wenyeviti hao wameongezewa muda baada ya vipindi vyao vya awali kumalizika;

Pili, Rais Magufuli amemteua Dk Harun Ramadhani Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Uteuzi wa Mrema na Dk Kondo umeanza Januari 20, 2020.

Tatu,
Rais Magufuli amemteua Profesa Mayunga Habibu Hemed Nkunya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).

Nne, Rais Magufuli amemteua Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa Mipango na Matumizi ya Ardhi.

Tano, Rais Magufuli amemteua Peter Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Uteuzi wa Profesa Nkunya, Mutakyamilwa na Maduki umeanza Januari 17, 2020.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dk Noel Logwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa. Uteuzi wa Dk Logwa umeanza Januari 17, 2020 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Akiolojia na Mafunzo ya Urithi (Archeology and Heritage Studies) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Logwa amechukua nafasi ya Profesa Audax Mabula ambaye amestaafu.

Pia soma:
1). Augustine Mrema aitaka Serikali kumlipa Tsh. Bilioni 2 kwa kusingiziwa kesi katika Serikali ya awamu ya tatu
2). Video: Halmashauri kuu ya TLP yampitisha Dr. John Magufuli kuwa Mgombea Urais 2020
3). Lyatonga Mrema: CCM wamenichezea rafu Uchaguzi Serikali za Mitaa, aonya

mrema.jpg
 
Hongera zake mzee wa Kiraracha lkn naona ni baada ya kuitaka sirikale imlipe fidia ya 2b
Rais Magufuli ateua wenyeviti 5 wa bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa.

Mara kwanza Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli kuongoza bodi ya Parole Julai16, 2016, na muda wake kuisha Julai 16, 2019 baada ya kutimiza kipindi cha miaka mitatu cha kuongoza bodi hiyo. Na leo 20 January 2020 amemteua tena. Hongera kwa Mrema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani yaweza kuwa fair well .Akipata fursa kutoa shukrani mzee Mrema aweza kuahidi kutoa gawio. ... Nitamshauri raisii tuwe na wafungwa wa nje ujasiliamali tulipe gawio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha Mrema ndani tena! Huyu Mzee ana akili kuliko tunavyofikiri ! Hongera Mrema
 
Rais Magufuli ateua wenyeviti 5 wa bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa.

Mara kwanza Mrema aliyeteuliwa na Rais John Magufuli kuongoza bodi ya Parole Julai16, 2016, na muda wake kuisha Julai 16, 2019 baada ya kutimiza kipindi cha miaka mitatu cha kuongoza bodi hiyo. Na leo 20 January 2020 amemteua tena. Hongera kwa Mrema. Mrema ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani cha TLP.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo Jumatatu Januari 20, 2020 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema wenyeviti hao wameongezewa muda baada ya vipindi vyao vya awali kumalizika;

Pili, Rais Magufuli amemteua Dk Harun Ramadhani Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Uteuzi wa Mrema na Dk Kondo umeanza Januari 20, 2020.

Tatu,
Rais Magufuli amemteua Profesa Mayunga Habibu Hemed Nkunya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC).

Nne, Rais Magufuli amemteua Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa Mipango na Matumizi ya Ardhi.

Tano, Rais Magufuli amemteua Peter Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Uteuzi wa Profesa Nkunya, Mutakyamilwa na Maduki umeanza Januari 17, 2020.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dk Noel Logwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa. Uteuzi wa Dk Logwa umeanza Januari 17, 2020 na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Akiolojia na Mafunzo ya Urithi (Archeology and Heritage Studies) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dk Logwa amechukua nafasi ya Profesa Audax Mabula ambaye amestaafu.

Pia soma:
1). Augustine Mrema aitaka Serikali kumlipa Tsh. Bilioni 2 kwa kusingiziwa kesi katika Serikali ya awamu ya tatu
2). Video: Halmashauri kuu ya TLP yampitisha Dr. John Magufuli kuwa Mgombea Urais 2020
3). Lyatonga Mrema: CCM wamenichezea rafu Uchaguzi Serikali za Mitaa, aonya

View attachment 1328719
Lyatonga ameula
 
Mrema huyu huyu aliyesema ataidai serikali fidia ya sh bilioni 3?
Nadhani umejigundua kuwa kujifanya Mtoto Wa chato unaonekana john mpiga chabo tu hata mrema anateuliwa toka kiraracha chabo boy umebong'oa tu rudi kwenu iringa katubu kwa msigwa
 
Back
Top Bottom