Rais Magufuli amteua tena Lyatonga Mrema kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Parole

Nadhani umejigundua kuwa kujifanya Mtoto Wa chato unaonekana john mpiga chabo tu hata mrema anateuliwa toka kiraracha chabo boy umebong'oa tu rudi kwenu iringa katubu kwa msigwa
Hahahaaaa....... Msigwa anarudi kwai Uwanji pale Iringa wanamtaka mwarabu Salim Asas " Misasa"
 
Kuna mwanasheria alipata kudai kuwa kulingana na sheria mwenyekiti wa Bodi ya Parole anatakiwa kuwa Jaji aliyestaafu au aliyeko kazini. Kama mwanasheria huyo yuko sahihi maana yake ni kuwa sheria imevunjwa mara ya pili!
 
wakabiliwa na mashtaka 280

Monday January 6 2020

Mhasibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania, Luis Lyimo (54) na Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Christian Social Services Commission, Peter Maduki (61) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 280.


[https://www-mwananchi-co-tz] TaAlly, Mwananchi tally@mwananchi. co.tz

IN SUMMARY

Watu wawili wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 280 ambapo 150 ya kughushi, 128 kuwasilisha nyaraka za uongo, moja la wizi na moja la kutakatisha fedha.


Dar es Salaam. Mhasibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania, Luis Lyimo (54) na Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Christian Social Services Commission, Peter Maduki (61) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 280.

Mawakili wa Serikali ya Tanzania, Zakaria Ndaskoi na Genes Tesha wamewasomea mashtaka washtakiwa hao leo Jumatatu Januari 6, 2020 huku wakipokezana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 150 ya kughushi, 128 kuwasilisha nyaraka za uongo, moja la wizi na moja la kutakatisha fedha.

Wakili Ndaskoi amedai washtakiwa hao walitenda makosa hayo kati ya mwaka 2017 na mwaka 2019 ndani ya Jiji la Dar es Salaam, Tanzania.

Amedai washtakiwa hao kwa nafasi zao wakiwa na nia ovu walighushi hundi mbalimbali zenye thamani ya mamilioni ya fedha na kusaini kwa jina la Upendo Mwingira bila ridhaa yake huku wakijaribu kuonyesha mshtakiwa, Luis Lymo alikuwa akilipwa na taasisi ya Christian Social Services Commission Fedha hizo kama kamisheni wakati si kweli.

atika mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo washtakiwa hao wanadaiwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali walizozighushi katika benki ya Standard Chartered.

Pia, washtakiwa hao kwa nyakati tofauti wanadaiwa kuandaa taarifa ya fedha ya uongo wakionyesha akaunti yenye namba 01080002404200 iliyopo katika benki ya Standard Charterd NIC Life House ilikuwa na zaidi ya Sh1.7 bilioni wakati wakijua ni uongo.



Katika shtaka la wizi kati ya Machi 30 mwaka 2017 na Oktoba 2018 katika benki hiyo washtakiwa hao waliiba zaidi ya Sh1 bilioni mali ya taasisi ya Christian Social Services Commission.

Kwa upande wa shtaka la utakatishaji fedha, washtakiwa hao wanadaiwa kutakatisha kiasi hicho cha Fedha cha zaidi ya Sh1 bilioni wakati wakijua fedha hizo zilitokana na kosa la kughushi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hao hawakuruhusiwa kuongeza chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikilizwa kesi ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika.

Kwa mujibu wa sheria shtaka la utakatishaji wa fedha pia halina dhamana hivyo washtakiwa walipelekwa rumande na kesi imeahirishwa mpaka Januari20 2020 kwa ajili ya kutajwa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom