Rais Magufuli amteua Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), achukua nafasi ya Dr. Modestus Kipilimba

Status
Not open for further replies.
Rais Magufuli amemteua Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa(TISS). Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS, Dr. Modestus Kipilimba atapangiwa kazi nyingine.


Tokea 2015, Kamishna Diwani Msuya ameshika nyadhifa mbalimbali kwa kasi sana

2015:
Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai

Mei 2015: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Novemba 2016: Katibu Tawala Kagera

Septemba 2018: Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU

Septemba 2019: Mkurugenzi Mkuu TISS

----------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua na kumuapisha Karnishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Kamishna Diwani Athuman Msuya umeanza leo tarehe 12 Septemba, 2019 na ameapishwa leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani Athumani Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Akizunguniza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amerntaka Kamishna Diwani Athuman Msuya kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa kuweka nibele masilahi va Taifa.

Kamishna Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi va Dkt. Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine

View attachment 1205370

View attachment 1205386

View attachment 1205394
Mkurugenzi Mkuu TISS, Diwani Athuman akiapishwa

DIWANI ATHUMAN MSUYA NI NANI?

Diwani Athuman Msuya katika utumishi wake kwenye Jeshi la Polisi ameshika vyeo na nyadhifa mbalimbali, ikiwemo kuwa msaidizi binafsi (Aide-De-Camp) wa IGP Omary Mahita. (Aide-de-camp ama kwa kifupi ADC au 'bodyguarg' kama wengi mlivyozoea kuwaita).

Mwaka 2008 alipandishwa cheo kutoka Mrakibu wa Polisi (SP) kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) na baadae kuteuliwa kuwa Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya (RCO).

April 28 Mwaka 2010 alipandishwa cheo kutoka Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kubaki na majukumu yake yaleyale ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya.

Novemba mwaka 2010 IGP Said Mwema alimpangia majukumu mapya ya kuwa Kamanda wa polisi (RPC) mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya ACP Daudi Siasi.

Mei 2012 alihamishwa kutoka Shinyanga kurudi Mbeya kuendelea na majukumu yake kama Kamanda wa polisi (RPC) wa mkoa wa Mbeya.

Novemba 21 mwaka 2013 Rais Jakaya Kikwete alimpandisha cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP).

Alidumu katika cheo hicho kwa wiki mbili tu, na Disemba 06 mwaka huohuo (2013) Rais Kikwete alimpandisha tena kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na kumteua kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (Deputy DCI).

Mwaka 2014 alibadilishiwa majukumu kutoka Deputy DCI, kuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai.

Tarehe 20 Machi 2015, Rais Kikwete aliwapandisha vyeo maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka Naibu Kamishina (DCP) kuwa Makamishina kamili (CP). Maafisa hao ni Kenneth Kasseke, Elice Mapunda na Diwani Athuman.

Mei 12 mwaka 2015 Rais Kikwete alimteua Kamishna Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuchukua nafasi ya Isaya Mungulu ambaye alistaafu.

Novemba 18 mwaka 2016 Rais Magufuli alitengua uteuzi wake katika nafasi ya DCI na kumteua kuwa Katibu Tawala (RAS) mkoa wa Kagera.

Miaka miwili baadae yani mwaka 2018, Rais Magufuli alimtoa kuwa RAS Kagera na kumteua kuwa Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU kuchukua nafasi ya Valentino Mlowola ambaye aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Septemba 12 mwaka 2018 Diwani Athumani Msuya aliapishwa kuwa Mkurugenzi mkuu TAKUKURU. Na Septemba 12 mwaka 2019 ameapishwa tena kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), kuchukua nafasi ya Mchungaji Dkt. Modestus Kipilimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Diwani ana shahada ya uzamili ya Sheria (LLM).

View attachment 1206133

Nadhani hiki Cheo cha Kamishna kinatumika vibaya katika kumtambulisha huyu Diwani Athuman....Haijazoeleka hii kusemma amemteua Kamishna so and so..tumezoea amemteua Kanali or Jeneral so and so...Kamishna imekaa kama jina la mtu...Nadhani wangekuwa wanasema amemmteua Kamishna wa polisi so and so...tehtehtehtehteh ni mawazo yangu tu lakini
 
Sijaandika uongo.

Ila kama hali ndivyo hivyo ilivyo ya kuchanganya hizi kazi basi Tanzania haina idara imara ya Usalama na maofisa wenye sifa stahiki.

Ndo maana raisi wa sasa anapata shida hata kumpata mtu sahihi kuongeza idara hii.

Ndo maana Nyara za serikali zilikuwa zikitoroshwa mchana kweupe.

Tukashindwa kubaini kwamba kuna mtu anataka kuizuia ndge ya ATCL isirudi Tanzania kisa tunadaiwa na mkulima huyo.

TISS imeruhusu watu wasio na maadili kuiingilia na kuivuruga kiasi cha kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Litakuwa jambo la busara kwa mkurugenzi mkuu atakaekuja baadae atoke ndani ya TISS.

Hapa namaanisha kwamba yule ofisa ambae ameanzia na ufuatiliaji yaani surveillance, afisa habari yaani reports officer, mchambuzi yaani analyst na baadae akapelekwa nje kuwa undercover officer na baadae kuwa RSO.

Kama utaratibu wa kupandisha maofisa ukifuatwa basi kutakuwepo na mori ya kazi na mashindano baina ya maofisa na tutapata vijana makini kwenye kazi.

Ukiwa unawatumia watu kutoka sehemu nyingine unakuwa unawachanganya maana hata bosi wao ni Tanzania tu anatembea na misafara.

Bosi unakaa mahala kila siku kuangalia picha kubwa ukutani ya hali halisi ya taifa.
Ndani ipi unayozungumzia
 
Sema wakat wa ACACIA.....yaani miaka ya 2016-2018 pamekuwa pamoto sanaa hapa kwetu. Mara akina Lissu, mara Mange Kimambi....anyway ni changamoto sanaa. Ametimiza wajibu wake, akatulie wafanye kaz wengne.....
Huyu demu Mange Kimambi wallahi ataingia kwenye world guines book
 
Ni vyema ukafika ofsini kwake uka muuliza mambo ya familia yake

Public figure huyo, kila mwenye swali akimfuata ofisini kwake patatosha kweli?

Halafu, unaanzaje kwenda usalama wa taifa kuomba kumwuliza boss mkubwa swali kama hili? Eeh?

Fikra zako si za kibaharia?
 
Siyo kweli. Ni mtu wa itelligence tu, tena ambaye ni mjanja sana kwenye maswala ya IT, kama vile alivyo Snowden, anayeweza akasurvive kwenye mtandao for some FEW HOURS, anapost vitu, pasipo kujulikana! Otherwise ukiona ana-survive for at least A DAY OR SO and under the rumour kwamba HAJULIKANI, jua kuwa hiyo ni SYSTEM ya Nchi. Napenda kukuhakikishia kuwa 99% ya raia wa kawaida duniani, hawajui namna mawasiliano ya kwenye mitandao yanavyofanyika. Kwa hiyo hayupo mtu anayeweza akatumia mawasiliano ya mtandao na asijulikane, unless ni system yenyewe, kwa sababu hata tuseme, mtu mjanja aliye-default kutoka kwa watu wa intelligence, lazima ajulikane na hawezi kujificha., sasa ije iwe layman tu kama mimi hapa? Thubutu!
Acha kumfananisha snowden na vitu vya kipumbafu, it bongo?!
 
Labda tukumbushane ivi Nape akat anaomba msamaha aliongea nini zaidi.
Si Alitoboa siri ! Unadhani iweje tena wakati anjikomba?
Mpango mzima kaumwaga mezani na alioshirikiana nao,hivi unadhani hili linahitaji upembuzi?
 
daaah . . . huwa nafadhaika sana tukianza kuhesabu viongozi wetu kutokana na kanda anayotokea au dini yake. Nachukia sana
Pole sana mkuu, ni katika kumjibu huyo mheshimiwa aliyetaka kuonyesha kwamba awamu hii inapendelea ukristo.

Rais JPM ameweza mpak kushiriki mashindano ya kuhifadhi kuran pale uwanja wa Taifa, RIP Nyerere na Mkapa hawakuwahi kufanya hivyo.
 
Hata mwalim wa shule ya msingi Tandahimba anaweza kuwa wakala wa TISS lkn hayuko kwenye utendaji wa kila siku!

Kinachowasumbua ni kwamba hamjui kuwa hawa jamaa wana ofisi, wanaenda kila siku kazini kama watumushi wengine wa umma, wana vikao vya menejiment idara n.k..sasa hao ndio nawazugumzia

Sio hao wapeleka umbeya!
Yule alikuwa zaidi ya informer ndio maana umeambiwa alikuwa na cheo cha juu huko TISS tangu akiwa jeshi la polisi. Na kazi zake za mwisho akiwa Polisi zilikuwa za Intelligence.

Muwe mnasoma na kufuatilia na zingine, mfano Israel wengi wa watumishi wa Mossad wametoka majeshi mbalimbali sio kwamba walianzaia ajira Mossad tu.

USA watu wa CIA wengi wametokea majeshi mbali.
 
Nimeota maxence melo ameomba msamaha kwa jiwe nikataka kujinyonga kamba ikakatika nikaamka
 
Ndioooo,wewe hapo utakuwa na kazi moja tu kulipoti katika kituo chako ulipotolewa utakuwa ukifika ofisini hufanyi yoyote zaidi ya kusoma magazeti,kukaa nyuma ya keybody ikifika saa 9 kamili unarudi zako nyumbani,maisha yanaendelea mpaka muda wa kupangiwa kazi nyingine utakapofika ama kustaafu
mbona poa tu
 
Balaa sanaa..Hapa tunaandika tu Meko sijui Jiwee...Ukikutana nae live dadeki unaweza msujudiaa
Kwanini umsujudie? Yaani kikundi cha watu milion 55 wamekutana wakachagua kiongozi awaongoze halafu wewe umgeuze MUNGU umsujudie? Na kwanini anatisha? Anatisha sababu mmekubaliana kwenye hicho kikundi cha watu mil55 kuwa aliyechaguliwa akitoa amri lazima ifuatwe? Amini nakwambia ukichunguza ulimwengu, ukachunguza dunia ilivyo halafu ukachunguza namna unavyolala halafu unaamka bila wewe kuamua sasa naamka utamwogopa zaidi anayesababisha hayo yatokee na kamwe huwezi kuwaza kumsujudia mwanadamu. Pia utaheshimu sana uumbaji wake na kuheshimu viumbe vyake. Hutawadharau binadamu wake kwa kuwaita majina yasiyo yao kama jiwe n.k
 
Hakuna tatizo kuhusu kapilimba umri wa kustaafu umefika mkuu ni vile tumezoe mzee baba akiteua tu basi kuna mtu katumbuliwa...
Sasa tangazo si lingesema kastaafishwa kwa mujibu wa sheria? Kuliko tunaambiwa ametenguliwwa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom