Rais Magufuli amteua Dkt. Willibrod Peter Slaa kuwa Balozi

Coco wewe unampongeza lakini ccm inazidi kupata nyufa kubwa.. Kumbuka kuna maelfu ya wanachama n na viongozi waliokipigania chama kufa na kupona leo wameachwa na kuchukuliwa mapandikizi.... Najua hii yote ni kwa ajili ya kuikomoa CHADEMA lakini mchezo huo ni hatari kwa chama chako
Kama watu hawaonekani unafkiri JPM atafanyaje mkuu? Huo n usajili mkuu Mechi si 2020 saivi tuko ktk usajili ulio makini.Staki kuamini kama ccm hamna mtu ila CV ya Slaaa sidhan kama yupo Mtu ambae yupo ccm ana CV ya dzaini hyo halafu yupo yupo tu mkuu??

Labda unipe mfano n kichwa gani kina madini ya slaa alaf kimekaa bila kazi CCM?? hamna mkuu kila mtu anakitengo chake na Kwa slaa napo hii lazima tukubali mkuu JPM kalamba JOKA,utakua ni ujinga kuacha mchezaji kama slaa akikosa TIMU wakati bado unajua bila wachezaji makini,Ushindi tutausikia bombani.

Sina tatizo na Baba Jesca...
 
Bado Lowassa na Sumaye...huwezi nambia Vyuma kama hivi eti leo ni Chadema haiji akilini,tukae kimyaaaa zipite chaguzi za uraisi kama mbili tu,utasikia kaanza Sumaye badae anafata Lowassa.

Hamna damu ya chadema kwa hawa watu mi ndo siwaamini kbsa ipo siku tu kazi zao walizotumwa huko chadema zikiisha watarudi..

OGOPA CCM kama Ukoma Utawaona wajinga leo ila kesho ushindi wao,kuna mijitu ipo ndani ya chama inaona miaka 10 mbele,haiangaliii hapa.Hiyo ndio SI SI EM
 
Baada ya kuona amechemka, Rais John P.Magufuli amemteua Dr.Wilbrod Slaa kuwa Balozi. Baada ya uteuzi huo, hiyo ni safari ya kurudi ndani chama cha mapinduzi. Kumbukeni ni huyo Slaa aliwahi kusema nina kadi ya CCM nimelipia ada miaka Kadhaa, alikili hayo akiwa Katibu mkuu wa CHADEMA.

Je alitumwa kwa kazi maalum? inaweza kuja propaganda eti naye amesamehewa kama Sofia Simba, maana yake amekuwa mwanaccm toka alivyokuwepo CHADEMA ni kama akina Masha.

Sitashanga Mkutano mkuu ujao atateuliwa kuvaa buti za A. Kinana, akiwa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.
 
Utabiri wako unaweza kuwa wa kweli maana bwana yule hakuwahi kurudisha kadi ya ccm, siku ikitokea hii ntakusaidia kufukua makaburi ya kuleta huu uzi tena.
 
Rais John Pombe Magufuli amemteua Dr. Slaa kuwa Balozi muda huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Novemba, 2017 amemteua Dkt. Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi.

Dr Willibrod Slaa ataapishwa baada ya taratibu kukamilika.
View attachment 636496

Dk Slaa azungumza na Azam Tv kutoka Canada

Amesema ameona taarifa hiyo na pia ametumiwa tarifa rasmi na anashukuru Mungu kwa kuteuliwa



HISTORIA YAKE
View attachment 636514
Dakitari Willbrod Peter Slaa, alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hadi 2015 alipojiuzulu. Hotuba ya Dr. Slaa kwa Watanzania toka Hoteli ya Serena - Tarehe 1 Septemba, 2015. Slaa alizaliwa Oktoba 29, 1948 kijijini Kwermusi, Wilaya ya Mbulu. Slaa alisoma Shule ya Msingi Kwermusi iliyoko wilayani Mbulu mwaka 1958-1961 na baadaye Shule ya Kati (Middle School) ya Karatu kati ya mwaka 1962-1965.

Baada ya darasa la nne, Dk Slaa alijiunga na Seminari ya Dung’unyi mkoani Singida mwaka 1966-1969 na kusoma sekondari, kisha akaendelea na masomo ya juu ya sekondari katika Seminari ya Itaga mkoani Tabora mwaka 1970 na 1971, alikohitimu kidato cha sita.

Alipomaliza kidato cha sita katika Seminari ya Itaga alikuwa amekwishafanya maamuzi ya kufanya utumishi wa kanisa. Alijiunga na Seminari ya Kibosho mwaka 1972-1973 na kupata stashahada ya Falsafa iliyompa sifa ya kudahiliwa na Seminari Kuu ya Kipalapala iliyoko Tabora kati ya mwaka 1974 na 1977 na alipata fursa ya kubobea zaidi katika masomo ya falsafa na theolojia, huku pia akisoma Stashahada ya Theolojia katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.

Dk Slaa alianza kuwa kiongozi tangu alipokuwa mwanafunzi pale Kipalapala ambapo alichaguliwa kuwa Rais wa Wanafunzi, mapadri nilioongea nao wanasema alikuwa mmoja wa viongozi wazuri sana kupata kuongoza Kipalapala.

Baada ya safari ndefu ya kuusaka “utumishi wa Mungu” Slaa alipadirishwa (alipewa upadri rasmi) mwaka 1977 na baada ya utumishi wa miaka michache alijiunga na Chuo Kikuu cha Pontifical Urbaniana nchini Italia akisomea udaktari wa Sheria za Kanisa maarufu kama J.C.D. (Juris Canonici Doctor ) au I.C.D. (Iuris Canonici Doctor) kati ya mwaka 1979 na 1981. Katika mfumo wa Kanisa Katoliki, (J.C.D au I.C.D) ndiyo shahada ya juu kabisa katika masomo ya sheria ya kanisa.

Dk Slaa amefanya kazi mbalimbali katika taasisi za Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Amewahi kuwa Msaidizi wa Askofu na Mkurugenzi wa Maendeleo katika Jimbo la Mbulu. Amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa muda wa miaka tisa (mihula yote mitatu). TEC ndiyo chombo cha juu cha usimamizi wa mambo ya Kanisa Katoliki hapa Tanzania.

Kwa mujibu wa Profesa Kitila Mkumbo, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, katika utafiti wake juu ya Dk Slaa, anasema “…Dk. Slaa anaelezwa kama Katibu Mkuu mwenye ufanisi mkubwa zaidi tangu TEC ianzishwe. Miundombinu mingi ya Kanisa Katoliki nchini ilianzishwa na kukamilishwa katika kipindi ambacho Dk Slaa alikuwa Katibu Mkuu wa TEC.”

Dk Slaa alijitoa kwenye upadri mwaka 1991. Kwa mujibu wa taarifa za maaskofu kadhaa nilioongea nao, wanasema “Dk Slaa lifanya hivyo kwa kufuata taratibu kamili ndani ya Kanisa Katoliki na aliacha yeye mwenyewe bila kushinikizwa, kufukuzwa au kupewa onyo”.Mara kadhaa Dk Slaa alipoulizwa kwa nini aliamua kuachana na upadri, amekuwa akikaririwa akisema kwamba “kuna mambo ambayo alidhani dhamira yake ilipingana nayo na akaona asingeliweza kuendelea, japokuwa anasisitiza kuwa masuala hayo ni binafsi zaidi.”

Ndani ya Chadema amewahi kushikilia wadhifa wa Makamu Mwenyekiti, kabla hajachaguliwa kuwa Katibu Mkuu katika mwaka ambao Freeman Mbowe alichaguliwa kuwa mwenyekiti na wameendelea kuongoza kwa pamoja hadi hivi sasa.

Dk Slaa ni mwandishi mzuri wa vitabu, ameandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and Exigency Liturgical Legislation (1981). Pia, kiongozi huyu anazungumza lugha nane kwa ufasaha; Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.

Dk Slaa aliwahi kumuoa Rose Kamili na kuzaa naye watoto wawili, Emiliana Slaa na Linus Slaa lakini waliachana muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Hivi sasa anaishi na “mchumba wake” Josephine Mushumbushi na wamepata mtoto mmoja.

Mbio za ubunge

Dk Slaa aliingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 1995, akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa jimbo la Karatu mkoani Arusha kwa tiketi ya CCM na alishinda kwenye kura za maoni za chama hicho. Vikao vya CCM vilipokutana Dodoma vikamuengua na kumuweka mbunge aliyekuwa anamaliza muda wake, Patrick Qorro. Wananchi wa Karatu wameniambia kuwa iliwapasa wamshinikize Dk Slaa kuchukua fomu na kugombea ubunge kupitia chama kingine. Bahati ikakidondokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Dk Slaa alipambana na wagombea kutoka vyama vinne; CCM, UDP, CUF na NCCR na aliwashinda wote kwa kupata asilimia 52.6, akifuatiwa na Patrick Qorro wa CCM aliyepata asilimia 44.1. Kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, Dk Wilibrod Slaa alishiriki kwenye uchaguzi akigombea kutokea Chadema kwa mara pili na kupata ushindi mkubwa zaidi kuliko mwaka 1995 na aliongoza hadi mwaka 2000. Na kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 pia aligombea ubunge kwa mara ya tatu jimboni Karatu na kushinda kwa asilimia 50.65 dhidi ya asilimia 49.0 za Patrick Tsere wa CCM.

Kati ya mwaka 2005– 2010 naweza kusema kuwa Dk Slaa ndiye alikuwa shujaa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na namuona kama mbunge aliyefanya kazi kubwa kitaifa na kimataifa kushinda mbunge mwingine yeyote. Huu ndiyo wakati ambapo yeye na Zitto Kabwe na wabunge wengine wachache walikuwa mwiba usioshikika bungeni. Hoja zao nzito kuhusu ufisadi, rushwa, uwajibikaji duni wa serikali vilimfanya kila Mtanzania aone nini maana na umuhimu wa Bunge la Wananchi.

Mbio za urais

Dk Slaa aliteuliwa na Chadema kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010. Kwa sababu ya umahiri wake wa kujenga hoja na kuonyesha kuwa ana uwezo wa kipekee, aliibuka katika nafasi ya pili, akipata asilimia 27.05 za kura zote, kwa kuachwa na Jakaya Kikwete wa CCM aliyeongoza kwa kupata asilimia 62.83.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015, Dk Slaa ni mmoja wa wanasiasa mahiri kutoka ndani ya vyama vya upinzani ambao wanatajwa kuwa na sifa, uwezo na vigezo vya kuongoza nchi.

Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sheria ya Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia ana stashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.

Pamoja na kwamba hakusoma katika mfumo wa kiserikali zaidi hapa Tanzania na amekuwa “Padri” katika kanisa, kwa kiasi kikubwa masuala ambayo ameyasimamia kutokana na elimu yake yamekuwa ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kimataifa zaidi. Mapadri wengi husoma falsafa na hawana tofauti yoyote na wasomi wa kawaida wanaosoma falsafa vyuoni na baadaye kuajiriwa katika kazi za kawaida.

Dk Slaa ana sifa kubwa sana katika kufanya kazi kwa juhudi “kuchapa kazi”.
Nimeshuhudia namna ambavyo hawezi hata kutoka nje kunyoosha mgongo kama mko vikaoni, mnaweza kujadiliana kutwa nzima na mkatoka hapo kukimbizana mahali kuhutubia wananchi asinywe hata maji. Slaa ana uwezo mkubwa sana kwenye eneo hili na kwa hakika nadhani nchi inahitaji Rais anayechapa kazi kufa au kupona.

Slaa ni kiongozi muadilifu. Dk Slaa amewahi kufanya kazi katika maeneo mengi tu tangu akiwa Padri wa Kanisa Katoliki, hadi amekuwa mbunge kwa miaka 15 huku akiongoza Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa. Hata mara moja hatukuwahi kusikia harufu, tuhuma au maneno kuwa amekwapua “senti” za umma au amechukua fedha za rushwa mahali. Kazi alizofanya ni safi na salama na zinampa “mamlaka ya kimaadili” (moral authority) kusimama hadharani na kusema kuwa atapambana na rushwa na ufisadi. Naamini, watu wa aina yake, kwa sasa ni muhimu sana katika nchi na uongozi wa nchi.

Slaa anaheshimika pia ni maarufu. Dk Slaa ni mmoja wa viongozi Waliokuwa upinzani wanaoheshimika na kufahamika sana hapa nchini Tanzania. Lakini pia sifa hizo zinavuka mipaka ya Tanzania ambako nako amefanya kazi za utumishi muda mrefu huku akiendelea kupata mialiko mikubwa ya nchi kama Marekani, nchi za Ulaya, ambako amekaribishwa katika vyuo vikuu bora kabisa duniani na kutoa mihadhara.

Kwa hiyo anatambulika na kuheshimika kama mmoja wa Waafrika wanaotoa mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya jamii zao.
Hongera Mheshimiwa Rais wetu Mr Magufuli Kwa kumchagua Dr.Slaa Kuwa Balozi wa Tanzania nchini kanada. Huyu ndio Rais mchapa kazi asiye na ubaguzi wa chama Dini na wala ukabila.

 
Ufisadi haupingwi majukwaani!Kama mtu ni fisadi mpeleke mahakamani akaulipie ufisadi wake.Kinyume na hapo ni siasa za unafiki zilizojaa ghiliba,visasi,roho mbaya,unafiki na uchumia tumbo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom